Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kufadhili mustakabali bora kwa wote: Mambo 5 ya kujua kuhusu jukwaa la ufadhili wa Maendeleo

Wanaume na wanawake wa kiasili wa Nuñoa huko Puno, Peru, wakisuka mavazi kulingana na nyuzi za alpacas..
SGP-GEF-UNDP Peru/Enrique Castro-Mendívil
Wanaume na wanawake wa kiasili wa Nuñoa huko Puno, Peru, wakisuka mavazi kulingana na nyuzi za alpacas..

Kufadhili mustakabali bora kwa wote: Mambo 5 ya kujua kuhusu jukwaa la ufadhili wa Maendeleo

Ukuaji wa Kiuchumi

Huku uchumi wa dunia ukiendelea kuathiriwa na mfululizo wa migogoro, maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa na wawakilishi wa serikali wanakutana kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, katika jaribio la kubadilisha mfumo wa fedha wa kimataifa, na kurejesha ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 iliyokubaliwa kimataifamkwenye mstari unaostahili.

Kuna mizozo mingi sana, majanga ya kibinadamu, mabadiliko ya tabianchi na misukosuko ya kiuchumi inayotokea ulimwenguni kote, na hivi sasa neno jipya linalotumiwa kuelezea hali ya mambo ya sasa ni "polycrisis" au kiama.

Neno hilo lilishuhudiwa mwaka 2022, mwaka ambao ulianza kwa matumaini ya muda kwamba uchumi wa dunia utaanza kuimarika kutokana najanga kubwa la COVID-19, lakini hivi karibuni dunia imetawaliwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Katikati ya migogoro hii yote inayoshindana, nchi nyingi hazina rasilimali za kuwekeza katika kujikwamua, hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, na maendeleo endelevu.

Haya ndiyo mazingira yenye changamoto ambapo Jukwaa la Ufadhili wa Maendeleo la 2023 (FfD) linafanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, kuanzia leo tarehe 17 hadi 20 Aprili, lenye lengo la kusukuma mbele sera za kushughulikia masuala ya kimaendeleo ya kimataifa, kuanzia madeni yanayodumaza, hadi maendeleo duni, na. uhaba wa chakula.

Mambo Matano ya kufahamu kuhusu jukwaa la FfD

1) Kwa nini Jukwaa la mwaka huu ni muhimu?

Wanajamii wa eneo la Quelimane, Msumbiji, wakirejesha misitu ya mikoko ili kuzuia mafuriko.
© FAO/Mani Tese/Leonel Raimo
Wanajamii wa eneo la Quelimane, Msumbiji, wakirejesha misitu ya mikoko ili kuzuia mafuriko.

2023 unaonekana kuwa wakati muhimu kwa maendeleo endelevu. Mwaka huu ni ishara ya katikati kati ya 2015, ambayo ilishuhudia kuzinduliwa kwa Ajenda ya Maendeleo Endelevu na mwaka 2030, tarehe ya mwisho ya kukamilika kwa ajenda ya Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Umoja wa Mataifa unapanga kuongeza kasi mpya ya kufikia Malengo hayo katika mkutano mkuu wa SDGs utakaofanyika  mwezi Septemba.

Hata hivyo, hakuna maendeleo yatakayopatikana bila ufadhili mkubwa

Mwezi Februari, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amekiri kwamba malengo ya SDGs yanakwenda kombo na ndio maana, amezindua mpango wa kuchochea utimizaji wa SDG, ambao unatoa wito kwa nchi tajiri kuchangia dola bilioni 500 kila mwaka kwa ajili ya kufadhili SDGs.

Amesema "Kuwekeza katika SDGs ni jambo sahihi na la busara. Ni mafanikio kwa ulimwengu, kwani viwango vya kijamii na kiuchumi vya kurrejea kwenye maendeleo endelevu katika nchi zinazoendelea ni vya juu sana."

Mpango huo wa kichocheo pia unatoa wito kwa mfumo wa fedha wa kimataifa kubadilishwa, ili kwamba mizigo inayolemea ya madeni ya nchi zinazoendelea ipunguzwe, na upatikanaji wa ufadhili kurahisishwa. Kufanya mabadiliko haya kuwa kweli ni moja ya ajenda ya Jukwaa la FfD la mwaka huu.

Wanawake wakikagua kahawa huko Addis Ababa, Ethiopia.
© FAO/Eduardo Soteras
Wanawake wakikagua kahawa huko Addis Ababa, Ethiopia.

2) Masuala makuu ni yapi?

Kulingana na Ripoti ya ufadhili wa maendeleo endelevu ya 2023, idadi ya watu wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula imeongezeka mara mbili, ikilinganishwa na viwango vya kabla ya janga la COVID-19 kutoka watu milioni 135 mwaka 2019 hadi watu milioni 345 mwaka 2023.

Vita nchini Ukraine imesababisha bei ya juu ya vyakula, ambayo imepanda kwa asilimia 50 mwaka 2022 ikilinganishwa na mwaka 2019.

Ukuaji wa viwanda wa nchi zenye maendeleo duni na nchi nyingi za Afrika hauendelei kama ilivyotarajiwa.

Ajenda ya 2030 inatoa wito wa kuongezeka maradufu kwa thamani ya viwanda katika nchi za Kiafrika ifikapo mwishoni mwa muongo huu.

Hiyo inamaanisha kutengeneza na kuuza bidhaa nyingi badala ya kuuza malighafi kwa nchi zingine.

Kwa kweli, thamani iliyoongezwa ilishuka kutoka karibu asilimia 10 ya Pato la Taifa mwaka 2000 hadi asilimia tisa mwaka 2021. Ulipaji wa madeni pia unasumbua mataifa maskini zaidi mathalani mwaka 2022, nchi 25 zinazoendelea zililazimika kutoa zaidi ya moja ya tano ya mapato yao yote ili kulipa madeni ya nje ya umma.”

Na ukosefu wa usawa wa kijinsia unasalia kuwa kikwazo kikubwa katika maendeleo, katika nchi 115 wanawake hawawezi kuendesha biashara kwa njia sawa na wanaume.

Wafanyakazi wa kizimbani wakishusha mizigo kutoka kwa meli jijini Dar es Salaam, Tanzania.
© ILO/Marcel Crozet
Wafanyakazi wa kizimbani wakishusha mizigo kutoka kwa meli jijini Dar es Salaam, Tanzania.

 3) Ni suluhu gani zitakazotajadiliwa?

Ajenda ya jukwaa itajikita zaidi na matokeo ya ripoti ya ufadhili wa Maendeleo Endelevu ya 2023, iliyotolewa tarehe 5 Aprili, ambayo inataka mifumo thabiti ya kodi, uwekezaji zaidi wa kibinafsi na wa umma kwa maendeleo endelevu, na mageuzi ya mfumo wa fedha wa kimataifa ili kuruhusu zaidi rasilimali zitakazopatikana.

Ripoti hiyo pia inasema kwamba uwekezaji mkubwa unahitajika haraka ili kuharakisha mabadiliko katika maeneo kama vile usambazaji wa umeme, viwanda, kilimo, usafirishaji na majengo, ili kuleta zama mpya za viwanda."

Ukuaji wa viwanda mara nyingi huhusishwa na uchafuzi wa mazingira na taka, lakini kihistoria umekuwa injini ya maendeleo. "Ukuzaji wa viwanda unaojali mazingira uliopendekezwa katika Ripoti unahusisha kusaidia kupunguza hewa ukaa, ikijumuisha vyanzo vya nishati mbadala kama vile upepo na jua, uchumi wa kidijitali, na uundaji wa sera zinazoongoza kwa uwekezaji katika shughuli endelevu, huku ikipunguza athari mbaya ya mazingira ya viwanda.”

Kuna dalili chanya kwamba ujumbe unaanza kukamilika, matumizi ya kimataifa katika mpito wa kuhamia kwenye nishaji jadidifu yaliongezeka hadi kufikia rekodi ya juu ya dola trilioni 1.1 mwaka 2022, na kwa mara ya kwanza kupita uwekezaji wa mfumo wa mafuta kisukuku duniani, na sekta ya uchumi wa kijani imekuwa ya tano kwa ukubwa ikiwa na thamani ya soko, la dola trilioni  7.2 mwaka 2021.

Mtoto mvulana akibeba maji katika kambi ya wakimbizi huko Cox's Bazar, Bangladesh.
© UNICEF/Patrick Brown

 4) Je, kuna hatari gani za kutochukua hatua?

Pengo kati ya matajiri na maskini linazidi kuwa kubwa, na, bila kufanyiwa marekebisho kamili ya uchumi wa dunia, inatarajiwa kwamba watu milioni 574 karibu asilimia saba ya watu duniani bado watakuwa wanaishi katika umaskini uliokithiri mwaka 2030.

Katika hali hii, mahitaji ya ufadhili wa nje kwa nchi zenye maendeleo duni au LDCs na nchi nyingine zenye kipato cha chini yanatarajiwa kuongezeka kutoka dola bilioni 172 hadi dola bilioni 220 katika miaka minne ijayo.

Miongoni mwa mapendekezo ni onyo, ikiwa mageuzi yaliyopendekezwa ni ya sehemu ndogo, hayajakamilika, au yatashindwa kutilia maanani SDGs, maendeleo endelevu hayatafikiwa, na hivyo kuweka Ajenda ya 2030 na shabaha za kupambana na mabadiliko ya tabianchi nje ya msitari wa kufikiwa.

Fundi akifanya kazi kwenye viombo vya nishati ya upepo mashariki mwa Quebec, Kanada.
© Climate Visuals Countdown/Joan Sullivan
Fundi akifanya kazi kwenye viombo vya nishati ya upepo mashariki mwa Quebec, Kanada.

5) Nini kinafuata?

Hakuna asiyetambua kwamba kazi iliyo mbele yetu ni kubwa na wataalam wanakubali kwamba maendeleo endelevu ya muda mrefu yatakosekana katika mazingira ambapo migogoro ya kibinadamu inaendelea.

Hatimaye, wanauchumi wa Umoja wa Mataifa wanataka mchakato wa FfD kusababisha mageuzi ya kina ya taasisi za kimataifa ambazo zinashughulikia vyema mahitaji ya haraka ya nchi zinazoendelea.

Zaidi ya jukwaa la FfD

• Majukwaa ya FfD ni ufuatiliaji wa kila mwaka wa kongamano la tatu la kimataifa la maendeleo ya ufadhili, ambalo lilitoa Agenda ya Hatua ya Addis Ababa, mfumo uliobuniwa ili kuhakikisha kuwa fedha zinakwenda kuboresha jamii, uchumi na mazingira.

• Maamuzi yaliyofanywa katika jukwaa hilo yataingia kwenye Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu maendeleo endelevu, mkutano katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mwezi Julai ambao unakagua maendeleo ya Ajenda ya 2030, hasa SDG17, ambayo inahusika na kujenga ushirikiano ili kusaidia Malengo.

SDG17 inahusika na kujenga ushirikiano ili kusaidia Malengo
United Nations
SDG17 inahusika na kujenga ushirikiano ili kusaidia Malengo

 • Maamuzi hayo katika HPLF pia yatatoa msingi wa mikutano mingine mingi muhimu ya ngazi ya juu, kama vile mkutano wa SDG, majadiliano ya ngazi ya juu ya Baraza Kuu kuhusu ufadhili wa maendeleo, mkutano wa mawaziri juu ya mkutano wa kilele wa wakati ujao na toleo la kwanza linalowezekana la mkutano wa kilele wa miaka miwili kati ya G20, ECOSOC, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na wakuu wa taasisi za fedha za kimataifa mwaka 2024.

• Matukio haya yataunda uwezekano wa kongamano la nne la Ufadhili wa maendeleo, ambalo nchi wanachama ziliamua kufikiria kuitishwa mwaka wa 2025.