Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi wanachama zimeweka mkakati wa kimataifa kuilinda dunia dhidi ya dharura za mjanga ya afya :WHO

Utoaji wa chanjo ya COVID-19 umepungua katika nusu ya nchi za Afrika.
WHO
Utoaji wa chanjo ya COVID-19 umepungua katika nusu ya nchi za Afrika.

Nchi wanachama zimeweka mkakati wa kimataifa kuilinda dunia dhidi ya dharura za mjanga ya afya :WHO

Afya

Nchi wanachama wa shirika la Afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO zimepanga jinsi mazungumzo kuhusu makubaliano ya kimataifa ya kuzuia majanga ya kiafaya, utayari na hatua yatakavyo songa mbele kwa nia ya kuwasilisha rasimu ya makubaliano ya kupitishwa na Baraza Afya duniani hapo mwezi Mei 2024.

Majadiliano yaliyoamalizika jana Alhamisi kuhusu rasimu ya makubaliano ya majanga ya kiafya yalifanyika wakati wa mkutano wa tano wa jumuiya ya majadiliano ya kiserikali (INB), ambayo yanajumuisha nchi 194 wanachama wa WHO.

Katika majadiliano hayo Bi. Precious Matsoso, mwenyekiti-mwenza wa ofisi ya INB, kutoka Afrika Kusini, alisema “Nchi kutoka sehemu zote za dunia ziliweza kujadili mawazo, changamoto na mapendekezo yao katika kongamano kwa ajili ya nchi zote kusikiliza na kuzingatia.”

Nchi zilikubali kuweka dirisha wazi kwa mapendekezo ya ziada yaliyoandikwa hadi tarehe 22 Aprili na kwamba mapendekezo hayo yatakusanywa pamoja na mengine yote yaliyotolewa katika wiki za hivi karibunina kuwekwa kwenye kifurushi kitakachopatikana kwa washiriki wote wa kikundi cha kuandaa rasimu.

Kisha ofisi ya INB itatoa, ifikapo tarehe 22 Mei, pamoja na kifurushi hiki, itazingatia mapendekezo ya kikundi yakijumuisha chaguo inapowezekana, kulingana na mawasilisho yote yaliyopokelewa na kujumuishwa katika hati ya utungaji wa rasimu na kundi hilo litakutana tena mwezi Juni kuendelea na majadiliano.

Naye mwenyekiti mwenza wa INB bwana Roland Driece wa Uholanzi alisema "Ulimwengu unatambua kwamba kile tunachotaka na tunahitaji kufikia makubaliano ambayo yatatusaidia kutorudia makosa ya kukabiliana na janga la coronavirus">COVID-19. Kuna mapendekezo mengi na mapendekezo ya kujengayaliyowasilishwa mezani ya jinsi ya kufanya hivyo.”

Mwanamke kijana akichunguzwa katika tovuti ya Hargele IDP nchini Ethiopia, ambako UNICEF inasaidia timu za afya na lishe zinazotembea.
© UNICEF Ethiopia/Mulugeta Ayen
Mwanamke kijana akichunguzwa katika tovuti ya Hargele IDP nchini Ethiopia, ambako UNICEF inasaidia timu za afya na lishe zinazotembea.

Mapendekezo ya rasimu kufikiriwa kwenye Baraza la afya la 77

Kulingana na mchakato uliokubaliwa na serikali katika kikao maalum cha Baraza la afya ulimwenguni mwishoni mwa mwaka 2021, mazungumzo juu ya rasimu ya makubaliano kuhusu majanga yatalenga kutoa rasimu ya mwisho ya itakayozingatiwa na kikao cha  77  cha Baraza la Afya Ulimwenguni mwezi Mei 2024.

Sambamba na majadiliano ya makubaliano ya majanga ya afya, serikali pia zinajadili marekebisho zaidi ya 300 ya kanuni za afya za kimataifa  zilizopitishwa mwaka 2005 (IHR) katika juhudi za kuimarisha kanuni hizo na kuifanya dunia kuwa salama dhidi ya magonjwa ya kuambukiza huku yakihakikisha usawa zaidi katika hatua za kimataifa. kwa dharura za afya ya umma.

Serikali zimekuwa zikifanya kazi ili kuhakikisha uthabiti na upatanishi katika michakato ya INB na IHR.

Marekebisho ya IHR yaliyopendekezwa pia yatawasilishwa kwa Baraza la Afya duniani mwaka 2024, na kwa pamoja, kwa makubaliano ya siku zijazo ya majanga, yatatoa picha kamili, inayosaidia, na ya usawa ya makubaliano ya afya ya kimataifa.