Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CSW67 yakunja jamvi kwa kukiri teknolojia ndio mkombozi kwa wanawake na wasichana

Carine. mhandisi wa programu za kompyuta akiwa nyumbani kwao Kigali nchini Rwanda akitumia kishkwambi kukamilsha programu yake iitwayo Save and Save.
© UNICEF/Mary Gelman
Carine. mhandisi wa programu za kompyuta akiwa nyumbani kwao Kigali nchini Rwanda akitumia kishkwambi kukamilsha programu yake iitwayo Save and Save.

CSW67 yakunja jamvi kwa kukiri teknolojia ndio mkombozi kwa wanawake na wasichana

Wanawake

Mkutano wa 67 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW67 umekunja jamvi usiku wa kuamkia leo tarehe 18 mwezi Machi mwaka 2023 kwa kusisitiza dhima ya teknolojia, ugunduzi na elimu kwenye zama za kidijitali katika kuchagiza kasi ya usawa kijinsia.

Tweet URL

Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini New York, Marekani na shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake, UN Women ambalo ndio lililikuwa mwenyeji wa mkutano huo ulioanza tarehe 6 mwezi huu wa Machi na kutakiwa kumalizika tarehe 17 lakini ukasonga hadi manane ya tarehe 18 kutokana na mijadala kutoka kwa washiriki.

Mwishoni mwa mjadala huo nchi wanachama zilipitisha nyaraka ya makubaliano ya mustabali huo, nyaraka iliyoridhiwa na wadau wakiweom serikali, sekta binafsi, mashirika ya kiraia na vijana kwa lengo la kusongesha ushiriki kamilifu na sawa na uongozi wa wanawake na wasichana katika kuunda, kurekebisha na kujumuisha teknolojia za kidijitali na michakato yote ya ugunduzi inayokidhi haki za binadamu na mahitaji ya wanawake na wasichana.

Tutafsiri makubaliano kivitendo – Bi. Bahous

Akizungumza mwishoni mwa mashauriaon hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women Sima Bahous ameesma “makubaliano ya mahitimisho ya mwaka huu ni ya kuleta mabadiliko makubwa na yanatusogeza katika dira yetu ya kuwa na dunia iliyounganika zaidi kwa wanawake na wasichana kutoka maeneo mbali mbalia. Ni kazi yetu tunapoondoka hapa kutafsiri makubaliano haya kuwa vitendo."

Amesema mafanikio ya makubaliano hayo ni zaidi ya hitimisho la mwisho wa kikao na kwamba “tutashirikiana pamoja kuyasongesha mbele. Yanatutuletea dira ya dunia yenye usawa zaidi. Hebu na tuyatafsiri kivitendo kwa maslahi ya wanawake na wasichana.”

CSW67 imesisitiza umuhimu kwa wasichana na wanawake kushiriki kikamilifu kwenye uongozi katika sayansi, teknolojia na ugunduzi na kuelezea hofu ya maendeleo yenye ukomo katika kuziba pengo la kijinsia katika kupata na kutumia teknolojia.

Halikadhalika hofu ya kuunganishwa na teknolojia, mitandao, elimu ya kidijitali na elimu ya kawaida bila kusahau uhusiaon kati ya ghasia au ukatili nje na ndani ya mtandao.

Balozi Mathu Joyini, (wa pili kutoka kulia) akifunga rasmi mkutano wa CSW67, anayemfuatia mwenye koti la buluu ni Mkuu wa UN Women, Bi. Sima Bahous
UN Women/Ryan Brown
Balozi Mathu Joyini, (wa pili kutoka kulia) akifunga rasmi mkutano wa CSW67, anayemfuatia mwenye koti la buluu ni Mkuu wa UN Women, Bi. Sima Bahous

CSW67 wa kwanza kufanyika kwa  ukamilifu ukumbini tangu COVID-19

Mkutano wa mwaka huu ulikuwa ni wa kwanza kufanyika kikamilifu ukumbuni katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa tangu janga la coronavirus">COVID-19 litangazwe kuwa janga la afya ya umma duniani mwaka 2020.

Zaidi ya washiriki 7,000 walijisajili kushiriki mkutano huo wakiwemo wakuu 4 wa nchi na serikali, mawaziri 116, matukio ya kando ya mkutano mkuu 205 yaliyofanyika ndani ya UN bila kusahau mashirika ya kiraia 700 yaliyokuwa na matukio yake kandoni.

Kwa mara ya kwanza, CSW ilikuwa na kikao cha vijana kikileta vijana, wawakilishi wa vijana na mashirika ya kiraia, mashirika ya Umoja wa MAtaifa wakishiriki katika mijadala na kutoa mapendekezo ya jinsi gani kuhakikisha wanawake na wasichana wanakuwa sehemu ya marekebisho ya kidiijtali.

Mwanafunzi Nina nchini Brazil akiwa anafanyia kazi roboti yake aliyotengeneza akiipatia jina Ere nyumbani kwao Rio de Janeiro.
© UNICEF/Mary Gelman
Mwanafunzi Nina nchini Brazil akiwa anafanyia kazi roboti yake aliyotengeneza akiipatia jina Ere nyumbani kwao Rio de Janeiro.