Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wengine 10 wauawa na wengine kutekwa DRC mwishoni mwa wiki: UN

Mtoto akiwa ameshikilia sufuria ya nzige katika kambi ya wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
© UNICEF/Olivia Acland
Mtoto akiwa ameshikilia sufuria ya nzige katika kambi ya wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Raia wengine 10 wauawa na wengine kutekwa DRC mwishoni mwa wiki: UN

Amani na Usalama

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Condo DRC umesema kundi la watu wenye silaha wameendesha msururu wa mashambulizi usiku kucha siku ya Jumamosi kuamkia Jumapili katika maeneo ya Kivu Kaskazini na Ituri na kusababisha raia wengi kufunghasha virago na kukimbia.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini New York Marekani msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema “Katika Kijiji cha Nguli Kivu Kaskazini wapiganaji wanaoshukiwa kuwa ni wa kundi la ADF wamewaua raia 10 na kuwateka wengine watatu. Na siku hiyohiyo wakikabiliana na mashambulizi hayo MONUSCO na jeshi la serikali ya Congo walizindua doria ya pamoja katika barabara ya Beni kuelekea Butembo na kushirikiana na mamlaka za maenmeo hayo na jamii katika maeneo ambako wapiganaji wa ADF wako.”

Kwa mujibu wa MONUSCO tangu Machi 6 mwaka huu mashambulkizi yanayofanywa na kundi la ADF yalisababisha vifo vya raia 118.

Huko Ituri, takriban raia 11 walikufa, wakiwemo wanawake wawili na watoto wawili, katika mashambulizi yaliyofanywa na kundi lenye silaha la CODECO katika vijiji kadhaa katika eneo la Mahagi wakati mmoja na mashambulizi ya ADF.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa walituma doria kuelekea kijiji cha Ngote ili kuwalinda watu wanaokimbia ghasia na kuunga mkono juhudi za jeshi la taifa ili kurejesha utulivu katika maeneo hayo.