Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Burundi yatangaza mlipuko wa polio Type 2: WHO

Burundi yatangaza mlipuko wa polio type 2.
© WHO
Burundi yatangaza mlipuko wa polio type 2.

Burundi yatangaza mlipuko wa polio Type 2: WHO

Afya

Mamlaka ya afya nchini Burundi leo imetangaza mlipuko na kusambaa kwa virusi vya polio Type 2 baada ya wagonjwa wanane kuthibitishwa, ikiwa ni mara ya kwanza kuthibitishwa kwa virusi hivyo baada ya zaidi ya miongo 3 kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO.

Taarifa ya WHO iliyotolewa mjini Bunjumbura na Brazzaville imesema virusi hivyo vimethibitishwa kwa mtoto wa kiume wa umri wa miaka minne katika wilaya ya Isale Magharibi mwa Burundi ambaye hajawwahi kupewa chanjo ya polio na pia kwa Watoto wengine wawili waliokutana na mvulana huyo.

Pia shitika hilo limeongeza kuwa sampuli tano kutoka kwenye mazingira yam aji machafu zimethiribisha uwepo wa kusambaa kwa virusi hivyo vya polio Type 2.

Akizungumzia mlipuko huo wa polio mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshidiso Moeti amesema “ Kubainika kusambaa kwa vitusi hivyo vya polio Burundi kunadhihirisha ufanisi ya mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa. Polio inaambukiza sana na kuchukuliwa hatua kwa wakati ni muhimu katika kuwalinda watoto kupitia chanjo inayofaa. Tunaunga mkono juhudi za kitaifa za kuongeza chanjo ya polio ili kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anayekosa na hakabiliwi na hatari ya kupooza inayotokana na athari za polio.”

Mtoto akipokea chanjo ya polio nchini Burundi. (Maktaba)
© UNICEF Burundi
Mtoto akipokea chanjo ya polio nchini Burundi. (Maktaba)

Serikali ya Burundi ambayo imetangaza mlipuko wa virusi hivyo kuwa ni dharura ya kitaifa ya afya ya umma inapanga kutekeleza kampeni ya chanjo ya kukabiliana na polio katika wiki zijazo, inayolenga kuwalinda watoto wote wanaostahiki wenye umri wa miaka 0 hadi 7 dhidi ya virusi hivyo.

Mamlaka za afya, kwa msaada kutoka kwa WHO na washirika wa kimataifa wa mradi wa kutokomeza polio (GPEI), pia wameanza uchunguzi zaidi wa magonjwa, ikiwa ni pamoja na tathmini za hatari ili kubaini ukubwa wa mlipuko huo.

Burundi inaimarisha zaidi ufuatiliaji wa polio, huku wataalam wa WHO katika uwanja huo wakiunga mkono ukusanyaji wa sampuli za ziada pamoja na kutathmini uwezekano wa kufunguliwa kwa maeneo mapya ya uchunguzi wa mazingira kwa ajili ya kugunduliwa mapema kwa virusi vya polio vinavyosambaa kimya kimya.

Polio Type 2 ni virusi vinavyopatikana sana Afrika na kuripotiwa zaidi ambapo kumekuwa na wagonjwa 400 walioripotiwa katika nchi 14 kwa mwaka 2022 pekee.