Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulanguzi wa kokeni umeongezeka baada ya kupungua kwa COVID-19:UNODC

Kiasi kikubwa cha cocane kilichokamatwa
UNODC
Kiasi kikubwa cha cocane kilichokamatwa

Ulanguzi wa kokeni umeongezeka baada ya kupungua kwa COVID-19:UNODC

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na dawa za kulevya na uhalifu UNODC imesema leo katika ripoti mpya kwamba kupitia vituo vipya na mitandao iliyopanuliwa ya wahalifu, ulanguzi wa mihadarati aina ya kokeni umerejea kwa kasi kufuatia kupungua kiasi hapo awali na ulanguzi huo kulikosababishwa na kuibuka kwa janga la COVID-19

"Kuongezeka kwa usambazaji wa cocaine duniani kunapaswa kutuweka sote katika hali ya tahadhari," amesema mkurugenzi mtendaji wa UNODC Ghada Waly na kuongeza kuwa "Uwezo wa soko la cocaine kupanuka barani Afrika na Asia ni ukweli mchungu na wa hatari."

Mahitaji na usambazaji wa hali ya juu

Ripoti hiyo ya kimataifa ya UNODC kuhusu mihadarati aina ya cocaine 2023 inasema “Mitandao ya uhalifu sasa inatofautiana na kupanua wigo ikiambatana na viwango vya kutisha vilivyovunja rekodi vya uzalishaji, hasa sasa baada ya janga la COVID-19 duniani kupungua kwani janga hilo lilionekana kupunguza biashara hiyo haramu kwa muda.”

Ili kupambana vyema na changamoto hiyo ya hatari Bi. Waly amezihimiza serikali na wengine kuchunguza kwa karibu matokeo ya ripoti hiyo ili kubaini jinsi tishio hili la kimataifa linavyoweza kukabiliwa na hatua za kimataifa kwa kuzingatia uhamasishaji, uzuiaji, na ushirikiano wa kimataifa na kikanda.

Cocaine inaingia Afrika na Asia

Ripoti hiyo inaeleza jinsi kilimo cha coca kilivyoongezeka kwa asilimia 35 kutoka 2020 hadi 2021, ikiwa ni rekodi ya juu na ongezeko kubwa zaidi la mwaka hadi mwaka tangu 2016.

Mihadarati iliyopatina Nchini South Africa :UNODC
UNODC
Mihadarati iliyopatina Nchini South Africa :UNODC

Kwa mujibu wa ripoti “Kupanda huko kunatokana na kupanuka wigo wa kilimo cha coca na kuboreshwa kwa mchakato wa kubadilisha coca kuwa cocaine hydrochloride, dawa ambayo inauzwa mitaani.”

Ripoti imeendelea kuainisha kwamba ongezeko la ugavi linalingana na ukuaji mkubwa wa mahitaji, huku maeneo mengi yakionyesha kuongezeka kwa kasi kwa watumiaji wa cocaine katika muongo mmoja uliopita.

Wakati soko la cocaine likisalia kujikita zaidi katika maeneo ya Amerika na sehemu za Ulaya, ripoti inaonya kwamba “kuna uwezekano wa upanuzi mkubwa wa soko katika bara la Afrika na Asia.”

Ripoti hiyo inachunguza kuibuka kwa vituo vipya vya ulanguzi wa cocaine ikibainisha kuwa nchi za Kusini Mashariki mwa Ulaya na Afrika hasa zile za Afrika Magharibi na Kati zinazidi kutumika kama vituo muhimu vya kupitisha mihadarati hiyo.

Bandari kwenye Bahari ya Kaskazini kama vile Antwerp, Rotterdam, na Hamburg, wakati huo huo, zimezipita sehemu za jadi za nchini Uhispania na Ureno, kwa kuingizia cocaine inayowasili Ulaya Magharibi.

UNODC inasema wasafirishaji haramu pia wanabadilisha njia zao za Amerika ya Kati kwa kutuma cocaine zaidi na zaidi Ulaya, pamoja na Amerika ya Kaskazini.

Rekodi ya kupindukia ya kukamatwa cocaine

Madawa ya kulevya aina ya Cocaine
UNODC/Ioulia Kondratovitch
Madawa ya kulevya aina ya Cocaine

Kwa mujibu wa ripoti kiwango cha kukamatwa na kukamata mihadarati hiyo pia kimeongezeka sana.

Uingiliaji wa usafirishaji wa cocace na vyombo vya sheria kote ulimwenguni kulifikia rekodi ya juu sana ya karibu tani 2,000 mwaka 2021.

Ripoti inaonyesha hali ya uhalifu iliyogawanyika katika mitandao mingi ya ulanguzi.

Ikichunguza mbinu za vikundi hivi, ripoti imegundua wafanyabiashara wapya wakiziba mapengo na safu ya wale wanaoitwa watoa huduma za mnyororo wa huduma kwa ada ya aina fulani.

“Kwa mfano, kuondolewa kwa wapiganaji kutoka jeshi la mapinduzi la Colombia (FARC), ambalo hapo awali lilikuwa limedhibiti maeneo mengi yanayolima coca nchini Colombia, kulizua mwanya kwa wengine kuingilia. Hii inajumuisha wasambazaji wapya wa ndani, wapiganaji wa zamani wa FARC , na vikundi vya kigeni kutoka Mexico na Ulaya” ripoti hiyo ilionyesha.

Coca ikikua katika mji wa Cauca Colombia , katika picha hii iliyopigwa toka angani
© UNODC
Coca ikikua katika mji wa Cauca Colombia , katika picha hii iliyopigwa toka angani

Kufuatilia mienendo

Angela Me, mkuu wa kitengo cha utafiti na uchambuzi cha UNODC, amesema ripoti hiyo ina tarifa nyingi zaidi kuhusu jambo hilo.

"Pamoja na maarifa na mienendo yake ya hivi karibuni juu ya njia, mbinu, na mitandao inayotumiwa na wahalifu, ni matumaini yangu kwamba ripoti itaunga mkono mikakati ya msingi ya ushahidi ambayo itakuwa mbele ya maendeleo ya siku zijazo katika uzalishaji wa cocaine, usafirishaji haramu wa binadamu, na matumizi ya mihadarati hiyo."

Ameongeza kuwa kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya cocaine ni changamoto kubwa ya kimataifa, hivyo kufikiria upya njia ambazo nchi zinaweza kufanya kazi pamoja ili kukabiliana na tatizo hilo kunahitajika sana.

"Ushahidi unaonyesha kwamba tatizo la cocaine ni tatizo la kimataifa linalovuka mipaka ya Atlantiki,"