Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulinzi wa raia unasalia kuwa ndoto Syria: Tume ya uchunguzi ya UN

Watoto wakilala katika msikiti ulioko katika wilaya ya Al-Midan ya Aleppo, Syria
© UNHCR/Hameed Maarouf
Watoto wakilala katika msikiti ulioko katika wilaya ya Al-Midan ya Aleppo, Syria

Ulinzi wa raia unasalia kuwa ndoto Syria: Tume ya uchunguzi ya UN

Amani na Usalama

Ripoti mpya iliyotolewa leo na tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi nchini Syria inasema pande zote katika mzozo unaondelea nchini humo zimetekeleza ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na ukatili katika miezi ya kuelekea tetemeko kubwa la ardhi kuwahi kushuhuduwa kwa zaidi ya karne katika ukanda huo, na kuendeleza muongo ulioghubikwa na mwenendo wa kushindwa kuwalinda raia wa Syria.

Ripoti inasema hatua za karibuni  za kukabiliana na athari za tetemeko hilo zilighubikwa na changamoto zaidi za kuwaangusha watu wa syria za kushindwa kufikisha msaada wa haraka na wa kuokoa Maisha Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Kushindwa huku kunahusisha pande nyingi ikiwemo serikali na wadau wengine katika mzozo huopamoja na jumuiya ya kimataifa na Umoja wa Mataifa.

Ripoti inasema “Pande hizo zilishindwa kupata muafaka kuhusu usitishaji mara moja wa uhasama, pia zilishindwa kuruhusu na kuwezesha msaada wa kuokoa maisha kuingia kupitia njia yoyote ile, ikiwemo timu za uokozi na vifaa katika wiki ya kwanza ambayo ni muhimu sana baada ya tetemeko hilo. Wasyria walijihisi wametelekezwa na kupuuzwa na wale ambao wanahitaji kuwalinda katika wakati wa uhitaji mkubwa. Sauti nyingi sasa zinatoa wito wa uchunguzi na uwajibikaji.”

Ukiukwaji wa haki na ukatili vinaendelea Syria

Leo hii tume hiyo ya uchunguzi kuhusu Syria imezindua ripoti yake mpya muda muda mfupi kabla ya kumbukumbu ya miaka 12 ya vita inayoendelea Syria, ikiorodhesha ukiuwaji mkubwa wa haki za binadamu unaoendelea katika taifa hilo la Mashariki ya Kati, ukiukwaji wa shria za kibinadamu nchi nzima katika miezi sita ya mwishoi yam waka 2022 ikiwemo hali mbaya ya Wasyria walio katika msitari wa mbele wa mapigano Kaskazini na Kaskazini Magharibi.

Mwenyekiti wa tume hiyo ya uchunguzi Paulo Pinheiro amesema “Ingawa kulikuwa na vitendo vingi vya kishujaa katikati ya madhila , pia tumeshuhudiwa kushindwa kwa serikali na jumuiya ya kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka kuelekeza msaada wa kibinadamu wa kuokoa Maisha kwa Wasyria walio kuwa na mahitaji ya dharura . Wasyria hivi sasa wanahitaji usitishwaji uhasama wa kina ambao unaheshimiwa, ikiwemo wahudumu wa misaada kuwa salama, hasa kutokana na ukatili wa nbaadhi ya pande katika mzoZo huo , na sasa tunachunguza mashambulizi mapya hata katika maeneo yaliyoathirika na matetemko ya ardhi.”

Ameongeza kuwa mashambulizi haya yanajumuisha mashambulizi ya anga yaliyoripotiwa wiki iliyopita kufanywa na Israel kwenye uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Aleppo uwanja ulio muhimu sana kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.

Serikali na upinzani wote wanahusika

Kwa mujibu wa ripoti mara baada ya matetemeko ya ardhi iliichukua serikali ya Syria wiki nzima kukubali kutoa fursa ya kupitisha misaada ya kuokoa Maisha kwenye mpaka.

Na zaidi ya hapo serikali na upande wa upinzani SNA wote walikuwa kikwazo cha ufikishakji misaada kwa jamii zilizoathirika wakati Hayat Tahrir al Sham HTS Kaskazini Magharibi waligoma kuruhusu misaada kuingia kutoka Damascus.

Mjumbe wa tume hiyo Hanny Megally amesema “Hivi sasa tunachunguza madai kadhaa ya pande zote katika mzozo kuzuia kwa makusudi misaada kuingia kwa jamii zilizoathirika . Na kwa kuwa wakati huu sasa misaada inaongezeka ni muhimu sana kuliko wakati mwingine wowote waruhusu japo kiasi misaada ya kibinadamu kufikishwa bila masharti au vikwazo kuweza kuwafikia wenye uhitaji iwe kupitia njia za mpakani au kwenye msitari wa mbele wa mapambano.”

Ripoti inasisitiza kuwa jamii nzima imeathirika huku Umoja wa Mataifa ukikadiria kwamba takriban watu milioni 5 wanahitaji mahitaji ya msingi ya malazi na vifaa visivyo chakula lkatika neo lililoathirika na tetemeko nchini Syria na kabla ya tetemeko, Wasyria zaidi ya milioni 15 walikuwa wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Ukiukwaji wa haki uliotendeka

Ripoti hiyo imeainisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa na pande zote katika mzozo dhidi ya raia wa Syria.

Kwa upande unaodhibitiwa na serikali tume imesema kuna ongezeko la kutokuwa na usalama hasa katika maeneo ya Dara’a, Suwayda’ na Hama na watu kukamatwa na kufungwa, utesaji, udhalilishaji na kutoweshwa.

Pia kuna ukiukwaji wa haki za umiliki wa mali ikiwemo kupokonywa mali hizo, kupigwa mnada na kuzuiwa fursa za kuingia kwenye nyumba na biashara zao.

Pia tume imebaini kwamba mazingira ya kurejea kwa usalama na kiutu bado hayapo na baadhi ya Wasyria walikataliwa kurejea , wengine walikamatwa au kuzuiliwa kuingia kwenye nyumba zao katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali katika kipindi cha ripoti hii.

Katika upande wa Kaskazini Mashariki kunakodhibitiswa na kikosi vya Kikurdi vya Syrian Democratic Forses (SDF) wanaendelea kuwashikilia kinyume cha sheria watu 56,000 wengi wakiwa ni wanawake na watoto , kwa shuku za baadhi ya wanafamilia kuwa na uhusiano na wapiganaji wa Da’esh katika kambi za Al-Hawal na Roj ambako hali inazidi kuwa mbaya.

Na tume hiyo inasema “Ina sababu za kuamini kwamba madhila wanayowapa watu hao huenda yakawa uhalifu wa vita kwa kutekeleza udhalilishaji wa utu na kutoa wito wa watu kuhamishwa kutekelezwa haraka”

Wadau wengine wanaokiuka haki

Mjumbe mwingine Lynn Welchman kwa upande wake amesema “Zaidi ya hayo makundi yenye silaha kwenye maeneo yaliyoathirika na tetemko la ardhi mara kwa mara yamekuwa yakizuia haki za wanawake na wasichana. Leo wengi wa wale wasio na malazi katika maeneo hayo ni wanawake na wasichana na wengi wao ndio wanaoendesha familia zao, hivyo usaidizi wa kibinadamu ni lazima uangalie suala athari za kijinsia katika mzozo.”

Ripoti imeendelea kusema kwamba serikali na wadaua wengine katika mzozo wameendelea kwa makusudi kuongeza mud awa madhila kwa maelfu ya familia kwa kuzuia taarifa kuhusu hatma ya wale waliotoweka kwa muda mrefu.

“Huu ni lazima uwe ni wito wa kuchukua hatua  kwani suala hili linawaathiri watu katika nyanja zote za kisiasa na kijiografia Syria na taarifa ijayo ya Katibu Mkuu lazima iwe na mwongozo wa hatua bila kuchelewa.” Amesema

Tume hiyo itawasilisha ripoti yake kwenye Baraza la haki za Binadamu mjini Geneva Uswis 21 Machi.