Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utapiamlo umeongezeka kwa asilimia 25 kwenye nchi zenye migogoro na kuweweka wanawake na watoto hatarini: UNICEF

Mama kijana mjamzito mdogo akionekana kufanyiwa uchunguzi wa kina katika kituo cha afya katika jimbo la Kassala, Sudan.
© UNICEF/Mojtba Moawia Moawi
Mama kijana mjamzito mdogo akionekana kufanyiwa uchunguzi wa kina katika kituo cha afya katika jimbo la Kassala, Sudan.

Utapiamlo umeongezeka kwa asilimia 25 kwenye nchi zenye migogoro na kuweweka wanawake na watoto hatarini: UNICEF

Wanawake

Wakati nusu ya watoto wote wa chini ya umri wa miaka 2 waliodumaa wakati wa ujaizito au wa chini ya umri wa miezi sita wako katika nchi zenye mizozo ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF iliyotolewa leo inasisitiza haja ya kuwekeza katika program za lishe kwa wasichana vigori na wanawake.

Ripoti hiyo imeonya kwamba idadi ya wanawake na wasichana vigori wenye ujauzito na wanaonyonyesha ambao wanaugua utapiamlo imeongezeka kutoka milioni 5.5 hadi milioni 6.9 tangu mwaka 2020 ikiwa ni sawa na asilimia 25 katika nchi 12 zilizoathirika sana na mgogoro wa kimataifa wa chakula na lishe.

Nchi hizo 12 zinajumuisha Afghanistan, Burkina Faso, Chad, Ethiopia, Kenya, Mali, Niger, Nigeria, Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Yemen zikiwakilisha kitovu cha mgogoro wa kimataifa wa lishe ambao umechochewa na vita ya Ukraine, ukame unaoendelea na changamoto ya usalama katika baadhi ya nchi.

Ripoti hiyo “Lishe duni na kupuuzwa: Mgogoro wa lishe duniani kwa wanawake na wasichana vigori” ambayo imetolewa kabla ya siku ya kimataifa ya wanawake  inaonya kwamba “migogoro inayoendelea, inayochochewa na ukosefu wa usawa wa kijinsia unaoendelea, inazidisha mgogoro wa lishe kati ya wasichana na wanawake ambao tayari walikuwa wameonyesha maendeleo kidogo miongo miwili iliyopita.”

Mwanamke kijana akichunguzwa katika tovuti ya Hargele IDP nchini Ethiopia, ambako UNICEF inasaidia timu za afya na lishe zinazotembea.
© UNICEF Ethiopia/Mulugeta Ayen
Mwanamke kijana akichunguzwa katika tovuti ya Hargele IDP nchini Ethiopia, ambako UNICEF inasaidia timu za afya na lishe zinazotembea.

Njaa inasukumua wengi katika utapiamlo

Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Catherine Russell "Mgogoro wa njaa duniani unasukuma mamilioni ya akina mama na watoto wao kwenye njaa na utapiamlo mkali. Bila ya hatua za haraka kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, matokeo yanaweza kudumu hadi kwa vizazi vijavyo."

Kulingana na ripoti hiyo mtazamo wa kina wa hali ya lishe ya wasichana vigori na wanawake duniani kote “zaidi ya wasichana na wanawake bilioni moja wanakabiliwa na utapiamlo ikiwa ni pamoja na uzito mdogo usioendana na urefu, upungufu wa virutubisho muhimu, na upungufu wa damu hali ambayo ina matokeo mabaya kwa maisha na ustawi wao.”

Lishe duni kwa wasichana vigori na wanawake wakati wa maisha yao inaweza kusababisha kinga dhaifu, athari ya utambuzi duni, na kuongezeka kwa hatari ya matatizo ya kutishia maisha ikiwa ni pamoja na wakati wa ujauzito na kujifungua na matokeo ya hatari na yasiyoweza kurekebishwa kwa maisha ya watoto wao, ukuaji wao, kujifunza kwao, mustakbali wao na uwezo wao wa kupata kipato.

Watoto milioni 51 wamedumaa duniani

Ulimwenguni kote watoto milioni 51 walio chini ya umri wa miaka 2 wana udumavu ikimaanisha kuwa ni mfupi sana kulingana na umri wao kutokana na utapiamlo.

Miongoni mwao karibu nusu ni huwa na wasiwasi wakati wa ujauzito na miezi sita ya kwanza ya Maisha ya watoto wao, ambacho ni kipindi cha siku 500 wakati mtoto anategemea kikamilifu lishe ya mama, kulingana na uchambuzi mpya katika ripoti hiyo.

"Ili kuzuia utapiamlo kwa watoto, lazima pia tushughulikie utapiamlo kwa wasichana vigori na wanawake," Russell aliongezea.

Asia ya Kusini na Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara zinabaki kuwa kitovu cha changamoto ya lishe miongoni mwa wanawake na wasichana vigori, n ani maskani ya wanawake na wasichana vigori  2 kati ya 3 wanaougua tatizo la uzito mdogo duniani, na wanawake na wasichana 3 kati ya 5 walio na upungufu wa damu. Wakati huo huo, wasichana na wanawake kutoka kaya masikini zaidi wana uwezekano wa kuteseka na uzani Zaidi ya wale wanaotoka katika kaya tajiri zaidi.

Migogoro ya kimataifa inaendelea kuvuruga ufikiaji wa wanawake kwa msaada wa chakula chenye lishe.

Mwaka 2021, kulikuwa na wanawake milioni 126 walikabiliwa na ukosefu wa chaka kuliko wanaume, na ni idadi ambayo ilikuwani ongezeko la watu milioni 49 zaidi ukilinganisha na mwaka 2019, hali ambayo inazidisha pengo la jinsia la ukosefu wa chakula.

Mama akiwa na binti yake mwenye umri wa miezi 9 akipata msaada kutoka kwa diwani katika Jimbo la Kassala, Sudan.
© UNICEF/Mojtba Moawia Moawi
Mama akiwa na binti yake mwenye umri wa miezi 9 akipata msaada kutoka kwa diwani katika Jimbo la Kassala, Sudan.

UNICEF inaongeza juhudi za msaada

Tangu mwaka jana UNICEF imekuwa ikiongeza msaada wake katika nchi zilizoathirika vibaya na mgogoro wa kimataifa wa lishe zikiwemo Afghanistan, Burkina Faso, Chad, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Ethiopia, Haiti, Kenya, Madagascar, Mali, Niger, Nigeria, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, na Yemen, kwa moango maalum wa kuzuia, kubaini na kutibu uzito mdogo wa kupindukia miongoni mwa wanawake na watoto.

Ripoti inatoa wito kwa serikali , wadau wa maendeleo na misaada ya kibindamu na wahisani , jumuiya za kiraia  na wadau wa maendeleo kubadili mifumo ya chakula, afya na hifadhi ya jamii kwa wanawake na wasichana.