Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CSW67 yafungua pazia, Mwenyekiti asema hitimisho litakuwa la kijasiri

Kikundi kinachojulikana kama ROTECH kilibuni kifaa cha umeme cha bei nafuu cha matumizi ya nyumbani kinachoitwa "Energyce
© UNECA/Abel Akara Ticha
Kikundi kinachojulikana kama ROTECH kilibuni kifaa cha umeme cha bei nafuu cha matumizi ya nyumbani kinachoitwa "Energyce

CSW67 yafungua pazia, Mwenyekiti asema hitimisho litakuwa la kijasiri

Wanawake

Mkutano wa 67 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW umeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ukileta pamoja wawakilishi kutoka serikali, mashirika ya kiraia yanayotambuliwa na Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC pamoja na vijana.

Mwenyekiti wa mkutano huo Balozi Mathu Joyini ambaye ni Mwakilishi wa kudumu wa Afrika Kusini kwenye Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi wa habari kuwa washiriki ni wanawake kutoka kona mbali mbali za dunia pamoja na vijana na zaidi ya yote na maudhui ni mabadiliko ya ugunduzi na teknolojia na nafasi yake katika zama hizi za kidijitali ili kufanikisha usawa na jinsia na uwezeshaji wanawake na maudhui yamekuja wakati muafaka.

"Teknolojia za kidijitali zinaleta fursa za kipekee katika kuwezesha wanawake na wasichana. Lakini vilevile  zinaleta changamoto mpya kubwa kwa haki za wanawake na wasichana. Teknolojia inaenda kwa kasi lakini mfumo wa maadili duniani bado haujarekebishwa."  

Hivyo amesema, "Tunatumaini kuwa na hitimisho la kijasiri ambalo linaweza maadili na viwango vya kusongesha mbele ili kuhakikisha wanawake wanawakilishwa kwenye nyanja ya teknolojia. Elimu ambayo inawaruhusu kushiriki katika ubunifu, mifumo anuai iliyoko, na kwamba wanawake na wasichana wanapatiwa furs aya kubuni, kuendeleza na kutumia teknolojia."

Mkutano huo ulioanza leo tarehe 6 Machi utamalizika tarehe 17 mwezi huu wa Machi ambapo pia wajumbe watatathmini changamoto na fursa za kufikia usawa wa kijinsia kwa wanawake na wasichana wa vijijini, maudhui yatokanayo na mkutano wa 62 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW62.