Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za LDCs zaadhinisha miaka 50 ya uungwaji mkono na UN

Rabab Fatima nwakilishi wa nchi za maendeleo duni, nchi zinazoendelea zisizo na bahari na za mataifa ya visiwa vidogo yanayoendelea OHRLLS akitoa hotuba yake wkati wa maadhimisho ya miaka 50 mataifa ya maendeleo duni LDCs
UN Photo/Evan Schneider
Rabab Fatima nwakilishi wa nchi za maendeleo duni, nchi zinazoendelea zisizo na bahari na za mataifa ya visiwa vidogo yanayoendelea OHRLLS akitoa hotuba yake wkati wa maadhimisho ya miaka 50 mataifa ya maendeleo duni LDCs

Nchi za LDCs zaadhinisha miaka 50 ya uungwaji mkono na UN

Ukuaji wa Kiuchumi

Mara baada ya ufunguzi, sherehe yakumbukumbu ilifanyika katika kituo cha mikutano cha kitaifa cha Qatar kusherehekea mafanikio tangu kuundwa kwa kitengo cha LDC mwaka 1971 na kuweka upya dhamira ya kuzichukua nchi za LDCs 46 zilizoorodheshwa hivi sasa katika safari ya mageuzi kuelekea ukuaji wa haraka wa uchumi na maendeleo endelevu.

Juhudi za mfumo wa Umoja wa Mataifa za kkubadili mwelekeo wa kuziacha nyuma nyuma nchi za LDCs katika uchumi wa dunia na kuziweka kwenye njia ya ukuaji endelevu na maendeleo zilianza miaka ya 1960.

Tangu wakati huo, Umoja wa Mataifa umelipa kipaumbele maalum kwa kuzitambua nchi za LDCs, kama zilizo hatarini zaidi katika jumuiya ya kimataifa.

Kwa kutambua mara kwa mara LDCs na kuangazia matatizo yao ya kimuundo, Umoja wa Mataifa unatoa umeweka bayana kwa jumuiya ya kimataifa kuhusu hitaji la makubaliano maalum katika kuunga mkono nchi LDCs.

"Historia ya LDCs sio moja tu ya ugumu. Pia ni historia ya jitihada za binadamu kupitia changamoto, mapambano, na mafanikio, dhidi ya uwezekano huo,” amesema Rabab Fatima, Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Nchi zenye maendeleo duni ambazo ziunaendelea zsizo na bandari na na nchi zinazoendelea visiwa vidogo (UN-OHRLLS).

“Kwa kutekeleza DPoA, tunaweza kufanya zaidi kutoa fursa sawa kwa wote, na kufanya mafanikio kuwa rahisi kupatikana,” ameeleza Bi Fatima, ambaye pia ni katibu mkuu wa mkutano wa LDC5.

Amesisitiza kuwa LDC5 inatoa fursa nzuri ya kufanya malengo ya mpango kazi kufikiwa. "Hebu sote tuchukue wakati huu na tuanze safari hiyo, sasa, hapa Doha. Safari kutoka kwa uwezo hadi ustawi."

Hafla hiyo pia ilishirikisha wanamuziki kutoka Yemen na Nigeria, pamoja na wacheza densi kutoka Tanzania, ambao waliwasilisha maonyesho yao ya kikabila, wakionyesha utofauti wa kitamaduni na uhai wa LDCs.

Katika muda wa siku tano zijazo mjini Doha, karibu wawakilishi 5,000 kutoka serikali, sekta binafsi, mashirika ya kiraia, wabunge na vijana watatathmini utekelezaji wa mpango wa utekelezaji wa Istanbul, uliopitishwa katika mkutano uliopita wa Umoja wa Mataifa huko Uturuki mwaka 2011, na kuhamasisha, msaada wa ziada wa kimataifa na hatua kwa nchi 46 zenye maendeleo duni zaidi duniani.