Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya mlo shuleni Afrika yakumbatia uzuri wa chakula kinacholimwa nyumbani: WFP

Mpango wa kuzalisha chakula nyumbani wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) unaboresha lishe ya watoto wa shule na kukuza uchumi wa ndani.
WFP/Nyani Quamyne
Mpango wa kuzalisha chakula nyumbani wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) unaboresha lishe ya watoto wa shule na kukuza uchumi wa ndani.

Siku ya mlo shuleni Afrika yakumbatia uzuri wa chakula kinacholimwa nyumbani: WFP

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Leo ni siku ya mlo shuleni barani Afrika, mlo ambao kwa mamilioni ya watoto ndio mlo pekee wanaoupata kwa siku.

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP linaloshirikiana na serikali za Afrika na wadau mbalimbali kuendesha program za mlo shuleni mwaka huu linatilia mkazo umuhimu wa chakula kinachozalishwa nyumbani katika kufanikisha mlo shuleni. 

Darfur, magharibi mwa Sudan ni moja ya maeneo ambako kuna chagizo kubwa la uzalishaji wa chakula kinachutumika kwa ajili yam lo shuleni ambako shule za msingi zinalima viazi, nyanya na mchicha kwenye ardhi maalum iliyotengwa na serikali.  

Mboga wanazolima hukatwakatwa, kuchemshwa na kukipikwa na kisha zinajumuishwa kwenye sahani za wanafunzi wakati wa chakula. 

Hameed Nuru wa WFP akiwa na wanafunzi darfur, Sudan, walipokuwa wakifurahia chakula kilichopikwa kwa viungo kutoka bustani yao ya shule. Ziara hiyo ilifanyika wakati Nuru alikuwa Mkurugenzi wa Nchi wa WFP Sudan.
© WFP/Sudan
Hameed Nuru wa WFP akiwa na wanafunzi darfur, Sudan, walipokuwa wakifurahia chakula kilichopikwa kwa viungo kutoka bustani yao ya shule. Ziara hiyo ilifanyika wakati Nuru alikuwa Mkurugenzi wa Nchi wa WFP Sudan.

"Watoto wanapokuwa likizoni, walimu huuza mavuno ili kununua vitu kama vile vitabu vya shule. Na sasa unaona watoto wakiingia kwenye kilimo", anasema Hameed Nuru, mkurugenzi wa zamani wa WFP nchini Sudan, ambaye leo anaongoza ofisi ya kimataifa ya  kimataifa ya WFP kwenye Muungano wa Afrika AU mjini Addis Ababa.  

Malipo ya vyakula vvinavyozalishwa nyumbani vinavyoungwa mkono na WFP  kutoka kwa wakulima wadogo wa ndani na bustani za shule kama zile za Sudan yameangaziwa Machi  katika mazungumzo ya ngazi ya juu huko Addis Ababa na Marrakech, Morocco, wakati wakuu wa serikali za Afrika na mawaziri wamekutana kwa ajili ya maadhimisho ya 8 ya ya siku yam lo shuleni Afrika. 

Kwa mujibu wa WFP leo hii mlo shuleni unawafikia watoto milioni 66 katika nchi zote 54 za Afrika.  

Takriban kila sahani au asilimia 84 ya programu za mlo shuleni unaotokana na uzalishaji wa ndani hufadhiliwa na bajeti za ndani.  

Changamoto za kiuchumi za hivi karibuni barani Afrika zimeongeza mvuto katika harakati na hitaji la kufikiria uzalishaji wa ndani wa chakula cha mlo shuleni haswa katika bara ambalo kilimo kinasalia kuwa chanzo kikuu cha mapato na ajira, hasa kwa wanawake. 

Mboga safi kutoka bustani ya shule katika mkoa wa Darfur nchini Sudan - zilizopandwa na mfumo wa kusukuma maji wa jua wa WFP. Watoto wanapokuwa likizo, walimu huuza mazao kununua vitabu vya shule.
© WFP/Sudan

Afrika imejikuta kuwa katika  hatarini zaidi kwa sababu ya kufungwa kwa kila kitu wakati wa janga COVID-19 na sasa mzozo wa Ukraine ambao umesababisha bei ya chakula duniani kupanda mwaka jana, anasema Nuru na kuongeza kuwa  "Hii imeangaza mwanga mpya juu ya ulishaji wa watoto shuleni na hitaji la kuuboresha kwa kiasi kikubwa, mfumo ili tuweze kupunguza hatari yetu katika siku zijazo." 

Mlo shuleni husaidia kupambana na njaa 

Matokeo muhimu ya utafiti mpya wa WFP yanaonyesha kuwa mlo shuleni husaidia kupambana na njaa, upungufu wa vitamini na madini, upungufu wa damu na unene uliokithiri au utipwatipwa.  

Pia unasaidia kuboresha usajili wa Watoto shuleni, kusaidia kujenga mnepo wa ndani, na chakula kinapokuzwa kwa njia endelevu, kinaweza kuchukua jukumu muhimu katika kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi.  

Milo inayozalishwa kutoka ndani ya nchi au nyumbani pia husaidia kuelimisha kizazi kipya cha viongozi. 

Lakini pamoja na mafanikio hayo, matokeo hayo ya karibuni ya utafiti pia yanaonyesha idadi ya watoto wenye umri wa kwenda shule wanaopokea mlo shuleni barani Afrika kile kinalochalishwa nyumbani na kutoka nje imepungua kwa kiasi katika miaka ya hivi karibuni hadi asilimia 31 mwaka 2022, kutoka asilimia 33 mwaka 2020.  

Kupungua huko kunasisitiza haja ya kuongeza juhudi za kutoa mlo shuleni wito ambao unasikika kwa viongozi wengi wa Afrika, amesema  Nuru.  

Chakula cha shule kinachopatikana kusini magharibi mwa Ethiopia. Chakula kinachozalishwa nyumbani shuleni chaanza Afrika.
© WFP/Michael Tewelde
Chakula cha shule kinachopatikana kusini magharibi mwa Ethiopia. Chakula kinachozalishwa nyumbani shuleni chaanza Afrika.

"Wakuu wa nchi na mawaziri wanaona faida ya kufanya hivyo ni kama uwekezaji," Nuru ameongeza, akibainisha kuwa baadhi ya maafisa wa ngazi za juu wa serikali walikula chakula cha mlo shuleni cha WFP walipokuwa watoto. 

"Wanajua jinsi inavyokuwa kwenda shuleni na njaa na kupata mlo. Hilo ndilo lililowasukuma." amesema.  

Kwa njia isiyo ya moja kwa moja, mlo shuleni unaozalishwa nyumbani hutoa faida mengine zinazoonekana.  

Pato la taifa la Afrika linaweza kuwa mara mbili na nusu zaidi ikiwa viwango vya afya na elimu vitafikiwa, kulingana na ripoti ijayo ya WFP ya “Hali ya mlo shuleni,” ambayo itachapishwa baadaye mwezi huu. 

Tayari, wakuu wa nchi kama vile Rwanda, Senegal na Benin wameweka fedha na nguvu za kisiasa kuunga mkono mlo shuleni katika nchi zao, katika kile Nuru anachokifananisha na athari ya mpira wa theluji. 

"Inazidi kuwa kubwa zaidi," anasema. "Nchi zaidi zinajiunga." 

Jumuiya za wenyeji ndizo za kwanza kufaidika haswa wakati chakula kinachotumisha shuleni kinalimwa nyumbani. 

Wanafunzi wa shule ya msingi wanaosoma katika makazi ya wakimbizi ya Mantapala, kaskazini mwa Zambia, ambayo imenufaika na ulishaji wa shule unaoungwa mkono na WFP.
© WFP/Vincent Tremeau
Wanafunzi wa shule ya msingi wanaosoma katika makazi ya wakimbizi ya Mantapala, kaskazini mwa Zambia, ambayo imenufaika na ulishaji wa shule unaoungwa mkono na WFP.

Nuru anasema kwa kutoa mlo shuleni "Unaunda mfumo mzima wa ikolojia ambapo walimu na wazazi wanakusanyika kupanda, na ambapo una ununuzi wa ndani ambao unachochea uchumi wa ndani. Kwa sababu mara nyingi ni wazazi hususan akina mama ndio wanaosambaza au kupika chakula shuleni. Ni mzunguko kamili." 

Miongozo iliyoundwa 

Mwaka jana, WFP na Muungano wa Afrika AU walizindua miongozo mipya ya kusaidia serikali na walimu kuanzisha milo ya watoto shuleni peke yao, na kutoa chaguzi mbalimbali ili kuendana na bajeti wanazoweza kumudu.  

Miongozo hiyo ni pamoja na aina za chakula cha kutumia, jinsi ya kukipata na jinsi ya kupata upendeleo wa kisiasa kwenye programu za milo. 

Katika makazi ya wakimbizi ya Mantapala kaskazini mwa Zambia, chakula kinachozalishwa nyumbani ni kichocheo kwa wanafunzi wadogo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambao wazazi wao wakati mwingine wanatatizika kulisha familia zao. 

"Tumeona kuwa watoto wengi wa shule hawaendi darasani wakati wa siku ambazo hawapewi chakula," anasema mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kasanda Chalawe. 

Mwanamke akipika chakula kilichopandwa nyumbani katika kambi ya wakimbizi ya Mantapala kaskazini mwa Zambia, ambako wakimbizi wengi wanatoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mbali na kusaidia usalama wa chakula, chakula cha nyumbani shuleni husaidia kuj…
© WFP/Vincent Tremeau
Mwanamke akipika chakula kilichopandwa nyumbani katika kambi ya wakimbizi ya Mantapala kaskazini mwa Zambia, ambako wakimbizi wengi wanatoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mbali na kusaidia usalama wa chakula, chakula cha nyumbani shuleni husaidia kujenga dhamana za jamii.

Nuru anachukulia nchi yake ya Botswana kuwa katika “kiwango cha dhahabu cha kulisha watoto wa shuleni kwa kutumia chakula kinachozalishwa nyumbani.” 

 Nchi imekuwa ikiendesha programu yake kwa miongo kadhaa. Leo, wanafunzi wa shule za msingi hula sio mlo mmoja bali miwili ya chakula cha shule kilichozalishwa nyumbani kila siku ya shule. 

"Hii imebadilisha sana mtazamo na tija ya watu," anasema. 

Lakini nchi nyingine zinaendelea kupiga hatua hasa linapokuja suala la kulisha watoto shuleni. 

"Nadhani ndani ya miaka 10 ijayo, nchi za Afrika zitakuwa zikifanya hivyo zenyewe," anasema Nuru akiongeza kuwa "Jambo ambalo ni zuri kwa sababu WFP inaweza kurudi nyuma na kuelekea katika awamu inayofuata ya kile tunachohitaji kufanya barani Afrika."