Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji ya maangamizi makubwa yalikuwa kilele cha miongo ya chuki dhidi ya wayahudi: Guterres

Wayahudi kutoka Subcarpathian Rus wanakabiliwa na mchakato wa uteuzi kwenye ramp huko Auschwitz-Birkenau, Poland.
US Holocaust Memorial Museum/Yad Vashem
Wayahudi kutoka Subcarpathian Rus wanakabiliwa na mchakato wa uteuzi kwenye ramp huko Auschwitz-Birkenau, Poland.

Mauaji ya maangamizi makubwa yalikuwa kilele cha miongo ya chuki dhidi ya wayahudi: Guterres

Haki za binadamu

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya waathitrika wa mauaji ya maangamizi makubwa au Holocaust Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres amesema mauaji hayo yalikuwa ni malimbikizo ya miongo ya chuki dhidi ya wayahudi ndio maana sasa ni wakati wa kuhakikisha chuki za aina yoyote ile zinakomeshwa duniani.

Katika ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu Antonio Guterres amesema ni siku ya kuwaenzi na kuwakumbuka wayahudi miltoni 6 watoto, wanawake na wanaume lakini pia , waroma na wasinti , watu wenye ulemavu na wengine wasiohesabika ambao walipoteza maisha katika ukatili huo. Hivyo ameongeza kuwa, “Tunatafakari maisha ya mamilioni ya watu yaliyokatizwa, mamilioni ya mustkbali wa watu ulioibwa. Tunapoomboleza kupotea kwa watu wengi na mambo mengi, tunatambua pia kwamba mauaji ya maangamizi hayakuwa yasiyoyakuepukika kama ilivyokuwa mauaji ya kimbari.Ilikuwa ni kilele cha miongo ya chuki dhidi ya wayahudi” 

Ujumbe huo wa Bwana Guterres umeendelea kueleza kwamba Manazi waliweza tu kusonga mbele na ukatili huo uliopangwa kutoka na ubaguzi wa Wayahudi uliokuwa Ulaya hadi kuangamizwa kwao kwa sababu wachache sana walisimama kupinga na wengi waliangalia tu. 

“Ilikuwa ni ukimya wa uziwi wa ndani na nje ya nchi  uliowatia moyo amesema kwani kengele za hatari zilikuwa zikilia tangu mwanzo, mmatamshi ya chuki na habari potofu.” 

Na zaidi ya hayo ameongeza ni “Kudharau haki za binadamu na utawala wa sheria. Kushabikia machafuko na hadithi za kutukuza rangi pia kudharau demokrasia na utofauti. Tunapokumbuka mauaji ya Holocaust tunatambua vitisho dhidi ya uhuru, utu na ubinadamu ikiwemo katika wakati wetu.” 

Amesema katika wakati huu ambao dunia inakabiliwa na changamoto zinazoongezeka za kiuchumi , na kisiasa, kuendelea kutukuza ugaidi wa walio weupe na kuongezeka kwa chuki na ubaguzi wa kidini ni lazima kuwa wawazi zaidi kuliko wakati mwingine wowote. “Hatupaswi kamwe kusahau wala kuruhusu wengine kusahau, kupotosha au kukataa mauaji ya Holocaust. Leo na kila siku, tuazimie kutonyamaza tena wakati wa uovu na kutetea daima utu na haki za wote.”