Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa wito wa hatua za haraka kuhakikisha maji salama na usafi duniani kote

Msichana akinywa maji katika  bustani wa shule yake huko Goré, kusini mwa Chad.
© UNICEF/Frank Dejongh
Msichana akinywa maji katika bustani wa shule yake huko Goré, kusini mwa Chad.

WHO yatoa wito wa hatua za haraka kuhakikisha maji salama na usafi duniani kote

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kwa ushirikiano na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya maji UN Water, shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO limechapisha utafiti kuhusu hatua za kuhakikisha lengo la maendeleo endelevu kuhusu maji SDG 6 zinahitaji kuharakishwa kwani ni 25% tu ya nchi zilizofanyiwa utafiti zinatarajiwa kufikia malengo ya usafi wa mazingira, mabadiliko ya tabianchi na majanga lazima yazingatiwe katika kuunda mifumo yenye mnepo. 

WHO, inasema kwamba hatua za haraka lazima zitekelezwe ili kuhakikisha maji, usafi wa mazingira na kujisafi duniani kote.  

Ripoti hiyo mpya pia inaeleza kuwa usimamizi endelevu wa rasilimali hiyo ni muhimu ili kuepusha madhara kwa afya ya mamilioni ya watu. 

Hitimisho la utafiti huo, kwa kuzingatia uchanganuzi wa UN Water, linaonyesha kuwa kuharakishwa kwa hatua hizi ni muhimu ili kufikia Lengo la 6 la Maendeleo Endelevu, la upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira kwa wote ifikapo mwaka 2030. 

Mwanamke akichota maji ya kutoka kwenye kisima
© WHO/Rob Holden
Mwanamke akichota maji ya kutoka kwenye kisima

Malengo ya usafi wa mazingira 

Ripoti inasema wakati asilimia 45% ya nchi ziko kwenye njia ya kufikia malengo yao ya kitaifa ya upatikanaji wa maji ya kunywa, lakini ni asilimia 25% tu ndio wako kwenye njia ya kufikia malengo ya msingi ya usafi wa mazingira. 

Chini ya theluthi moja wanasema wana rasilimali watu zinazohitajika kutekeleza kazi kubwa za maji ya kunywa, usafi wa mazingira na usafi, unaojulikana kwa kifupi WASH. 

Utafiti huo uliochapishwa na WHO na UN Water unaelezea hali ya iliyopo ya, mifumo ya WASH katika zaidi ya mataifa 120 na ndio mkusanyiko mkubwa zaidi wa takwimu kutoka kwa idadi kubwa zaidi ya nchi hadi sasa. 

Uwekezaji katika maji ya kunywa, usafi wa mazingira na usafi 

Kulingana na utafiti huo, ingawa uwekezaji katika maji safi, usafi wa mazingira na usafi umeongezeka katika baadhi ya maeneo ya dunia, zaidi ya asilimia 75 ya mataifa yaliyohojiwa yaliripoti ukosefu wa fedha za kutosha kutekeleza mipango na mikakati yao. 

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus ameonya kuhusu mgogoro wa dharura wa "upatikanaji duni wa maji safi ya kunywa, vyoo na usafi wa mazingira ambao unafupisha maisha ya mamilioni ya watu duniani kila mwaka.” 

Anasema kuwa kadri majanga ya asili yanayohusiana na hali ya hewa yanavyozidi kuongezeka na kukithiri, na vivyo hivyo kuna kuongeza kwa ugumu wa kutoa huduma salama. 

Wanawake na watoto wakitoka kuchota maji nchini Zambia
© UNICEF/Karin Schermbrucke
Wanawake na watoto wakitoka kuchota maji nchini Zambia

Ushiriki wa kitaifa na mabadiliko ya tabianchi 

Mkuu huyo wa WHO pia ametoa wito kwa serikali na washirika wa maendeleo kuimarisha mifumo na uwekezaji katika huduma za maji safi ya kunywa na vyoo kwa wote ifikapo mwaka 2030. 

Takwimu zinaonyesha kwamba sera na mipango mingi ya maji ya kunywa, usafi wa mazingira na usafi haishughulikii hatari za mabadiliko ya tabianchi, wala mnepo wa janga hilo wa teknolojia na mifumo ya usimamizi wa sekta. 

Zaidi ya theluthi mbili ya nchi tu ndizo zina hatua za kufikia idadi ya watu walioathiriwa na mabadiliko ya tabianchi, na theluthi moja tu ndio inayofuatilia maendeleo na kuwekeza katika idadi ya watu hawa. 

Mbali na SDG 6 

Rais wa UN Water na mkurugenzi mkuu wa shirika la kazi duniani ILO wameonya kwamba “ulimwengu uko nje ya mwelekeo wa kufikia SDG 6". 

Gilbert F. Houngbo ameongeza kuwa ukosefu wa uwekezaji huwaacha mabilioni ya watu wakikabiliwa na magonjwa ya kuambukiza, hasa baada ya majanga ya asili. 

Kwake, data hizi mpya zinaelekeza kwenye ahadi za hiari ambazo jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya katika mkutano wa maji wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwaka 2023 ili kujumuisha jumuiya zilizo hatarini zaidi na kutatua mgogoro wa maji na usafi wa mazingira duniani kote. 

Mkutano huo, ambalo unapendekeza mapitio ya hatua za muongo wa Umoja wa Mataifa wa hatua kuhusu maji na usafi wa mazingira, kuanzia 2018 hadi 2028, utafanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, kuanzia Machi 22 hadi 24 mwaka 2023. 

Mtoto akinywa maji kutoka kwa chanzo pekee cha maji safi katika Kambi ya Hesbi huko Saida, Lebanon.
© UNICEF/Fouad Choufany
Mtoto akinywa maji kutoka kwa chanzo pekee cha maji safi katika Kambi ya Hesbi huko Saida, Lebanon.

Uharaka na fursa 

Ripoti inasema mkutano huo utakuwa ni fursa ya kwanza katika kipindi cha miaka 50 kwa jumuiya ya kimataifa kukagua maendeleo na kutoa ahadi thabiti za kuchukua hatua mpya kuhusu maji na usafi wa mazingira na viongozi wa kimataifa. 

Kulingana na WHO, matokeo ya mabadiliko ya tabianchi na hali mbaya ya hewa huleta umakini zaidi kwa maswala haya, ikionyesha hitaji la haraka la mtazamo wa jamii nzima na ushirikiano wa kimataifa kuchukua hatua kwa pamoja. 

Utafiti huu unaonyesha kuwa nchi zinazoendelea zimeonyesha kiwango cha juu cha utashi wa kisiasa na uwekezaji katika uboreshaji na usalama wa maji ya kunywa, mifumo ya vyoo na usafi wa mazingira. 

Pamoja na ripoti hiyo, WHO na UN Water wanatoa wito kwa serikali zote na wadau kuongeza usaidizi wa utoaji huduma kwa kuimarishwa kwa utawala bora, ufadhili, ufuatiliaji, udhibiti na kujenga uwezo.