Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yachagiza huduma za afya kwa wote katika mkesha wa nusu fainali za kombe la dunia

WHO yachagiza huduma za afya kwa wote katika mkensha wa nusu fainali za kombe la dunia
Picha: WHO
WHO yachagiza huduma za afya kwa wote katika mkensha wa nusu fainali za kombe la dunia

WHO yachagiza huduma za afya kwa wote katika mkesha wa nusu fainali za kombe la dunia

Afya

Leo ni siku ya huduma za afya kwa wote ambayo kila mwaka huadhimishwa Desemba 12, na mwaka huu shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO linaadhimisha siku hiyo nchini Qatar katika mkesha wa nusu fainali za za mwaka huu za kombe la dunia la la shirikisho la soka duniani FIFA kwa kampeni maalum ya kuhamasisha umma kufanya mazoezi kwa ajili ya afya zao. 

Tukio la kampeni hiyo “Be Active: Bring the Moves for Health For All” linalofanyika sanjari na michuano ya kombe la dunia limeandaliwa na FIFA,wakfu wa Elimu zaidi ya yote na wizara ya afya ya umma ya Qatar (MoPH), na linashirikisha wasanii mbalimbali mashuhuri wakiwemo wa dansi, muziki na wasakata kabumbu. 

Lengo kubwa la kampeni hiyo ni kuhagiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs ya Umoja wa Mataifa na hasa lengo la afya kwa wote. 

Sherrie Silver akitoa mafunzo kwa wakulima vijana kijijini Cameroon kwa ajili ya video ya muziki kuchagiza wakulima vijana.
©IFAD/DavidPacqui
Sherrie Silver akitoa mafunzo kwa wakulima vijana kijijini Cameroon kwa ajili ya video ya muziki kuchagiza wakulima vijana.

Washiriki wa kampeni 

Kampeni hiyo inayoungwa mkono na mshidi wa tuzo ambaye ni mchaza densi na nguli wa kufundisha mitindo mbalimbali raia wa Rwanda Sherrie Silver inajumuisha nyota wengine kama mwanamuziki The Mad Stuntman, aliyeimba kibalo kilichovuma kimataifa I Like to Move It, Move It, kibao ambacho ndio maudhui ya kampeni hiyo ya FIFA na WHO ya Bring The Moves

Na wengine wanaoshiriki ni mabalozi wema wa WHO ambao ni wasakata gozi nyota Didier Drogba kutoka Côte d’Ivoire and na golikipa wa Brazil Alisson Becker. 

Sherrie Silver amesema . "Siwezi kusubiri kuhamasisha kwenye tamasha hili la mashabiki wa FIFA na na kutimiza sehemu ya wajibu wangu wa kutangaza afya kwa wote katika siku hii ya huduma za afya kwa wote kwa niaba ya Rwanda na kuunga mkono Wakfu wa Elimu Zaidi ya Yote. dansi imekuwa chanzo si cha furaha na shauku kwangu tu, bali pia kuwa na afya njema, kimwili na kiakili.” 

Kuchagiza umuhimu wa afya 

Tukio hilo linaadhimisha umuhimu wa afya kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na: 

• Kuadhimisha kampeni ya kila mwaka ya siku ya huduma za afya kwa wote UHC, inayoongozwa na WHO na washirika wa kimataifa, ili kukuza na kuharakisha mafanikio ya upatikanaji wa huduma za afya zilizo nafuu, sawa na zinazofaa kote ulimwenguni 

• Kutoa wito wa maendeleo kuhusu lengo la maendeleo endelevu  namba 3 la afya na ustawi, kama sehemu ya kampeni ya #ScoringForTheGoals inayoongozwa na EAAF/UN na 

• Kuhamasisha kuongeza mazoezi ya viungo kupitia dansi itakayoshirikika watu wengi inayofanyika siku moja kabla ya kuanza kwa kampeni ya afya ya “Be Active: Bring The Moves” wakati wa nusu fainali za kombe la dunia zinazofanyika 13-14 Desemba. 

Msanii wa dansi na mwimbaji nyota The Mad Stuntman kwa upande wake amesema: “Nimefurahi sana kuona mashabiki wa soka wakija na kucheza wimbo wangu wa I Like to Move It kwa ajili ya afya, wakati wa kombe la dunia. Siwezi nina shauku ya kuona hatua kwa macho yangu leo 12 Disemba ninakapoungana na Sherie Silver na wapenzi wa soka kutoka kote ulimwenguni kwenye tamasha la mashabiki wa FIFA tunapojiunga na vuguvugu la kimataifa la Afya kwa Wote katika siku ya huduma za afya kwa wote.” 

Balozi Mwema wa WHO Didier Drogba, mpiganaji wa kampeni ya #BringTheMoves, ambayo inahimiza vijana kufanya mazoezi.
© WHO
Balozi Mwema wa WHO Didier Drogba, mpiganaji wa kampeni ya #BringTheMoves, ambayo inahimiza vijana kufanya mazoezi.

Kauli za wanasoka nyota  

Mwanasoka nguli wa FIFA Didier Drogba, ambaye ni balozi mwema wa amesema “Tunaweza kujishughulisha kwa ajili ya afya kwa njia nyingi, kwa kuhama kutoka kwenye kuchagiza kwa ajili ya siha hadi kwenye wito wa kupata huduma za afya kwa wote. Ninajivunia kutoa sauti yangu kwa wote katika siku hii muhimu ya huduma za afya kwa wote hapa Doha." 

Naye Alisson Becker, kipa wa Brazil na Liverpool, na balozi wa mwema wa WHO kwa ajili ya kuhamasisha afya meongeza kuwa "Katika siku ya huduma za afya kwa wote hebu sote tuwe watendaji na kutekeleza jukumu letu kufanya afya kwa wote ndio lengo letu.” 

Maudhui ya siku ya huduma za afya kwa wote UHC kwa mwaka 2022 ni "Jenga dunia tunayoitaka, mustakabali wenye afya kwa wote," lengo lake ni kutoa wito wa kuwa na mifumo thabiti ya afya inayojitolea kwa usawa, uaminifu, mazingira mazuri, uwekezaji na uwajibikaji. 

Kampeni ya  Scoring 4 the Goals Campaign inalenga kuchagiza, kuelimisha na kutoa wito wa kuchukua hatua ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs ambayo ni ajenda ya kimataifa ya kuleta maendeleo na mustakbali wa usawa kwa wote. 

Ushirikiano baina ya WHO, FIFA na wizara ya afya Qatar  

WHO na wizara ya afya ya Umma, Qatar, wakishirikiana kwa karibu na FIFA, walizindua ushirikiano wa miaka mitatu wa michezo kwa afya mwaka 2021 kwa malengo ya kuchagiza maisha yenye afya, usalama wa afya na ustawi wa mwili na kiakili kwenye kombe la dunia la FIFA Qatar mwaka 2022 na kutumia mashindano hayo  kama fursa ya kuonyesha mbinu bora za matumizi ya mashinadano kuimarisha afya katika hafla kuu za michezo ulimwenguni kote. 

WHO na FIFA zilitia saini mkataba wa maelewano mwaka 2019 ili kuhamasisha maisha yenye afya bora kupitia soka.  

Mashirika hayo yameshirikiana katika kampeni nyingi za afya, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na mashabiki wa soka na umma kwa kiasi kikubwa kuhusu hatua za kuimarisha shughuli za kimwili, afya ya akili, udhibiti wa matumizi ya tumbaku na kuzuia janga la COVID-19

WHO na Kombe la dunia la FIFA Qatar 2022 katika kampeni ya #Scoring4theGoals
Picha: WHO
WHO na Kombe la dunia la FIFA Qatar 2022 katika kampeni ya #Scoring4theGoals

EAAF na Umoja wa Mataifa walizindua, mwanzoni mwa Kombe la dunia la FIFA Qatar 2022, kampeni ya #Scoring4theGoals ili kuchagiza ufikiaji wa malengo ya maendeleo endelevu.