Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO na ofisi ya haki za binadamu kuchunguza machafuko ya Kishishe DRC 

Wapiganaji wa M23 wakielekea Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC
MONUSCO/Sylvain Liechti
Wapiganaji wa M23 wakielekea Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC

MONUSCO na ofisi ya haki za binadamu kuchunguza machafuko ya Kishishe DRC 

Amani na Usalama

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO kwa kushirikiano na ofisi ya pamoja ya aki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini humo, wametuma timu ya haki za binadamu kufanya uchunguzi wa awali kuhusu ghasia dhidi ya raia zinazodaiwa kutekelezwa wakati wa mapigano kati ya kundi la wapiganaji la M23 na Mai-Mai huko Kishishe 

Kishishe ipo katika eneo la Rutshuru jimbo la Kivu Kaskazini Mashariki mwa DRC, na tukio hilo lilifanyika mwishoni mwa mwezi uliopita.  

Timu hiyo kwa sasa iko uwanjani ikiwasiliana na mamlaka za mitaa na kufanya mahojiano na mashahidi na waathiriwa ili kujua idadi ya majeruhi huko Kishishe, eneo ambalo bado liko bado ya udhibiti wa M23. 

Ujumbe huo pia umetoa ulinzi na kuwahamisha raia ambao walikuwa wametafuta hifadhi katika kituo cha MONUSCO huko Rwindi, ingawa ukosefu wa utulivu katika eneo hilo unaendelea kutatiza ufikiaji wa waathyirika.  

Ujumbe  wa MONUSCO unasisitiza wito wa kukomesha uhasama, pamoja na uungaji mkono kamili kwa mipango ya kikanda ya kurejesha hali ya utulivu.