Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sehemu kubwa ya dunia ilighubikwa na ukame kuliko kawaida mwaka 2021: WMO

Msichana akimwagilia miche eneo la Merea ziwa Chad
UNDP/Jean Damascene Hakuzimana
Msichana akimwagilia miche eneo la Merea ziwa Chad

Sehemu kubwa ya dunia ilighubikwa na ukame kuliko kawaida mwaka 2021: WMO

Tabianchi na mazingira

Sehemu kubwa ya dunia ilikuwa kavu kuliko kawaida mwaka 2021, na kusababisha athari kubwa za za uchumi, mifumo ya ikolojia na maisha yetu ya kila siku, limesema leo shirika la hali ya hewa duniani (WMO). 

Kulingana na ripoti ya kwanza ya shirika hilo kuhusu rasilimali za maji duniani, iliyotolewa mjini Geneva Uswis maeneo ambayo yalikuwa makavu isivyo kawaida ni pamoja na Rio de la Plata la Amerika Kusini, ambapo ukame unaoendelea umeathiri eneo hilo tangu 2019. 

Barani Afrika, mito mikuu kama vile Niger, Volta, Nile na Congo ilikuwa na mtiririko wa chini wa wastani wa maji mwaka wa 2021.  

Pia ripoti imeongeza kuwa hali kama hiyo imeshuhudiwa pia katika mito sehemu za Urusi, Siberia Magharibi na Asia ya Kati. 

Kwa upande mwingine, ripoti imeeleza kuwa kulikuwa na wingi wa mito iliyokuwa na kiwango cha  juu ya kawaida cha maji katika baadhi ya mabonde ya Amerika Kaskazini, Amazon Kaskazini na Afrika Kusini, na pia katika bonde la mto Amur nchini China, na kaskazini mwa India. 

Katika bara la Afrika, mito kama vile Niger, Volta, Nile na Congo ilikuwa na maji ya chini ya kiwango cha kawaida mwaka 2021, pamoja na sehemu za Urusi, Siberia Magharibi na Asia ya Kati. 

WMO ilisema kuwa watu bilioni 3.6 hawana maji ya kutosha angalau mwezi mmoja kwa mwaka na kwamba hii inatarajiwa kuongezeka hadi zaidi ya watu bilioni tano ifikapo 2050. 

Mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi 

"Athari za mabadiliko ya tabianchi mara nyingi huonekana kupitia maji, ukame mkali zaidi na wa mara kwa mara mafuriko makubwa zaidi, mvua za msimu zisizo na uhakika na kasi ya kuyeyuka kwa barafu na athari mbaya kwa uchumi, mifumo ya ikolojia na nyanja zote za maisha yetu ya kila siku", amesema katibu mkuu wa WMO Profesa Petteri Taalas. 

Ameongeza kuwa "Na bado, hakuna uelewa wa kutosha wa mabadiliko katika usambazaji, wingi, na ubora wa rasilimali za maji safi". 

Ripoti hito ya hali ya rasilimali za maji duniani "inalenga kuziba pengo hilo la maarifa na kutoa muhtasari wa jumla wa upatikanaji wa maji katika sehemu mbalimbali za dunia", ameongeza Taalas na kuendfelea kusema kwamba  

"Hii itafahamisha kuhusu mabadiliko ya tabianchi na uwekezaji wa kukabiliana na hali hiyo pamoja na kampeni ya Umoja wa Mataifa ya kuhakikisha katika miaka mitano ijayo watu wote duniani wanafikiwa na fursa ya kupata tahadhari za mapema za hatari kama vile mafuriko na ukame". 

Maji yakiwa ziwa yakiwa yamefurika katika wilaya ya Kousseri katika jimbo la Far kaskazini mwa Cameroon
© UNHCR/Moise Amedje Peladai
Maji yakiwa ziwa yakiwa yamefurika katika wilaya ya Kousseri katika jimbo la Far kaskazini mwa Cameroon

Maji, maji kila kona 

Kati ya mwaka 2001 na 2018, UN Water iliripoti kwamba asilimia 74 ya majanga yote ya asili yanahusiana na maji. 

Mkutano wa hivi karibuni wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP27, uliofanyika nchini Misri, ulihimiza serikali kujumuisha zaidi maji katika juhudi za kukabiliana na hali hiyo, maji kwa mara ya kwanza yamerejelewa katika hati ya matokeo ya COP kwa kutambua umuhimu wake, limebainisha shirika la WMO. 

Toleo la kwanza la ripoti linaangalia mtiririko wa maji,  ujazo wa maji yanayotiririka kupitia mkondo wa mto wakati wowote na pia kutathmini uhifadhi wa maji ya nchi kavu kwa maneno mengine, maji yote kwenye uso wa ardhi na chini ya uso wa ardhi na maji yaliyogandishwa. 

Ripoti inaangazia tatizo la msingi ambalo ni ukosefu wa takwimu za utaalam wa maji zilizothibitishwa. 

Sera ya takwimu iliyounganishwa na WMO inalenga kuharakisha upatikanaji na ushirikishwaji wa takwimu za utaalam wa maji, zikijumuisha utiririshaji wa mito na taarifa za mabonde ya mito ya kuvuka mipaka. 

Ardhi imeghubikwa na ukame 

Kando na tofauti za mtiririko wa mito, hifadhi ya jumla ya maji ya nchi kavu iliainishwa kuwa chini ya kiwango cha kawaida kwenye pwani ya magharibi ya Marekani, katikati mwa Amerika Kusini na Patagonia, Afrika Kaskazini na Madagasca, Asia ya Kati na Mashariki ya Kati, Pakistani na Kaskazini mwa India. 

Pia ripoti imebainisha kuwa kiwangi kilikuwa juu ya kawaida katika maeneo ya Afrika ya Kati, kaskazini mwa Amerika Kusini haswa bonde la Amazon na kaskazini mwa Uchina. 

"Kwa ujumla mielekeo hasi ina nguvu zaidi kuliko ile chanya", imeonya ripoti hiyo ya WMO, huku ikiongeza kuwa maeneo kadhaa mengine yakijitokeza ikiwa ni pamoja na Patagonia, mito ya Ganges na Indus, pamoja na kusini magharibi mwa Marekani. 

Glaciers nchini Chile na Argentina zimepungua sana katika miongo miwili iliyopita.
WMO
Glaciers nchini Chile na Argentina zimepungua sana katika miongo miwili iliyopita.

Ulimwengu uliofunikwa na barafu 

Eneo lililofunikwa yaani na barafu, kufunikwa na theluji, na ambapo sasa, kumefunikwa na mvuke ndio hifadhi kubwa zaidi ya asili ya maji safi ulimwenguni kwa mujibu wa ripoti. 

"Mabadiliko ya rasilimali za maji katika maeneo ya milimani yanaathiri uhakika wa chakula, afya ya binadamu, uadilifu na matengenezo ya mfumo ikolojia, na kusababisha athari kubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii", limesema shirika laWMO, na kuongeza kuwa wakati mwingine kunasababisha mafuriko ya mito na mafuriko kutokana na kuyeyuka kwa barafu. 

Makadirio ya muda mrefu ya kuyeyuka na kutoweka kwa barafu na muda wa kilele cha maji, ni nyenzo muhimu kwa maamuzi ya muda mrefu ya maamuzi ya kujenga mnepo kukabiliana na hali hiyo imesema ripoti hiyo ya WMO.