Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asante UNICEF kwa kutuwezesha kufanya mtihani- Wanafunzi Uganda

Rahima Nakacwa, mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Green Valley huko Kampala, ananawa mikono baada ya kufanya Mtihani wake wa Kiingereza wa PLE mnamo Novemba 2022.
UNICEF./ Uganda Rahima Nakacwa, mwanafunzi wa darasa la 7 shule ya msingi Green Valley jijini Kampala nchini Uganda akinawa mkono baada ya kumaliza mtihani wa kuhitimu darasa la 7 Novemba 2022.

Asante UNICEF kwa kutuwezesha kufanya mtihani- Wanafunzi Uganda

Utamaduni na Elimu

Nchini Uganda shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limewezesha wanafunzi wa shule moja ya msingi nchini humo kufanya mtihani wa kuhitimu shule ya msingi baada ya shule hiyo kulazimika kufungwa na wanafunzi kuwekwa karantini kufuatia mwanafunzi mmoja kupata maambukizi ya Ebola. 

T

Mwalimu mkuu wa shule, Grace Nakkazi, akiwagawia wanafunzi chakula na vinywaji katika Shule ya Msingi ya Green Valley huko Kampala, Uganda. Mandhari inamuonyesha akiandaa milo mezani nje ya shule, huku chupa za juisi zikiwa karibu.
© UNICEF/Uganda Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Green Valley iliyoko Masanafu kwenye mji mkuu wa Uganda, Kampala, Grace Nakkazi akiandaa mlo uliofadhiliwa na UNICEF kwa ajili ya wanafunzi waliokuwa wanafanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi pamoja na walimu wao.

Tarehe 20 mwezi Septemba mwaka huu wa 2022, Wizara  ya Afya nchini Uganda ilitangaza mlipuko wa Ebola, mlipuko ambao ulihatarisha kuvuruga mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi kwa wanafunzi wa darasa la saba. 

Shule ya msingi ya Green Valley kwenye mji mkuu Kampala ilikuwa hatarini zaidi kwa sababu mwanafunzi mmoja aliambukizwa Ebola hivyo  madarasa matatu yalifungwa na shule ikafungwa ili ifanyiwe usafi.  

Mpaka Katula ni Mkurugenzi wa Shule ya msingi Ya Green Valley anasema, “uhai wa walimu wangu, wanafunzi wangu na wangu mwenyewe ulikuwa hatarini, ningaliweza kuachia shule, kwa hiyo kufunga shule lilikuwa ni jambo dogo.” 

Shule hiyo ilifungwa wiki tatu kabla ya kufanyika kwa mtihani ambapo Ian Mugisha mmliki wa shule ya msingi Green Valley anafafanua kwamba, hii mitihani hufanyika katika siku maalum iliyopangwa. Usipofanya siku hizo, hutaweza kufanya tena, lazima usubiri mwaka unaofuatia. Kwa maajabu Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na Bodi ya Taifa ya mitihani Uganda, walishirikiana kuona wanafunzi wanafanya mitihani na UNICEF ikasaidia.” 

Mwanamume aliyevaa sare ya kijani anaingia kwenye basi dogo jeupe la Toyota lililokuwa limeegeshwa mbele ya jengo la shule ya kijani huko Kampala, Uganda. Gari hilo ni sehemu ya usafiri unaotolewa na UNICEF kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Green Valley.
UNICEF/ Uganda Wanafunzi wa darasa la 7 wa shule ya msingi Green Valley jijini Kampala nchini UGanda wakipanda mabasi yaliyofanikishwa na UNICEF ili kwenda kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi baada ya shule yao kufungwa kutokana na Ebola.

Jane, jina lake hili si rasmi ni mmoja wa wanafunzi 30 waliokuwa karantini na anasema, “UNICEF imenisaidia vifaa vya kufanyia mtihani, mlo wa mchana na usafiri kutoka nyumbani hadi hapa. Nilifanya mitihani ya kuhitimu darasa la Saba nikiwa karantini na nina imani nimefanya vizuri.” 

Na Bwana Katula anarejea na shukrani akisema, “sijui hii shule ingalifanya bila UNICEF kuingilia kati. Lakini kile ninachoweza kusema, asante UNICEF.” 

Kwa  ujumbe UNICEF zaidi ya wanafunzi 170 waliokuwa kwenye karantini walipatiwa msaada wa kisaikolojia pamoja na vitabu vya kiada na vifaa vingine vya shule na kufanyia mtihani, bila kusahau mlo wakati wa kipindi cha mtihani.