Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mji wa Libiąż, Poland wanuia kutokomeza makaa ya mawe licha ya bei ya nishati duniani kupanda

Uchimbaji wa makaa ya mawe nje ya Samaca, Colombia.
World Bank
Uchimbaji wa makaa ya mawe nje ya Samaca, Colombia.

Mji wa Libiąż, Poland wanuia kutokomeza makaa ya mawe licha ya bei ya nishati duniani kupanda

Tabianchi na mazingira

Mji wa Libiąż, kusini mwa Poland uko katika harakati mabadiliko. Kwa karne kadhaa, Libiąż umekuwa mji wa uchimbaji makaa ya mawe. 

Kama inavyofahamika, makaa ya mawe yanachangia sana katika uzalishaji wa hewa chafuzi ambazo zinachochea mabadiliko ya tabianchi. 

Na matumizi ya makaa ya mawe kwa ajili ya kupata joto la majumbani nchini Poland, kunachangia katika uchafuzi wa hew ana hivyo kusababisha kila mwaka vifo vya mapema 46,000 na hasara ya kiuchumi ya dola bilioni 38 hadi dola bilioni 40.  

Kwa sababu hiyo mji huu sasa kwa msaada wa Benki ya Dunia, uko katika mchakato kwa ajili ya mstabali bora wa siku zijazo kwa kutafuta njia mbadala ya muda mrefu ya kuhamia katika vyanzo vya nishati safi lakini kupanda kwa gharama ya nishati kunafanya mchakato kuwa mgumu. Jacek Latko ni Meya wa mji huu wa Libiąż anasema, “Janga la sasa la nishati linaleta kutokuwa na uhakika. Watu wetu hawawezi kununua makaa ya mawe ya kupasha joto nyumba zao wakati wa baridi.” 

Kuachana na makaa ya mawe kinasalia kuwa kipaumbele kama asemavyo kiongozi mwingine Jozef Gawron wa ofisi ya serikali inayohusika na viwanda….anasema, “tunataka kuunga mkono kila kitu kinachohusiana na nishati safi. Huu ndio mstakabali wetu.” 

Libiaz sasa inafanya kuibadilisha ardhi iliyokuwa machimbo ya makaa ya mawe na kuwapa mafunzo wafanyakazi kwa ajili ya kazi mbadala. Jadwiga Bochenek ni Mkuu wa shule ya ufundi ya Libiąż anasema,  “Wakati hali ya soko ilipobadilika, na vyanzo zaidi vya nishati rafiki kwa mazingira vikapewa kipaumbele zaidi, pamoja na kufundisha mbinu za uchimbaji za siki zijazo, pia tulianza kufundisha wataalamu wa nishati.” 

Mipango ya ndani ya jamii inaboresha maisha ya jamii. Na hapa Meya Jacek Latco anarejea akiseama, “Ni wajibu wetu kuhakikisha watu wetu wanaishi katika hali nzuri. Na tunawekeza sana katika miundombinu ikiwa ni pamoja na hivi karibuni tumefungua bwawa la kuogelea, viwanja vya mpira wa miguu vyenye nyasi bandia, kituo bora cha utamaduni na maktaba. Tunazifanya shule na Kindergarten kuwa za kisasa. Tunachofanya ni kutengeneza hali nzuri ya kuishi.”  

TAGS: Tabianchi na mazingira, Benki ya Dunia, Poland, mabadiliko ya tabianchi, makaa ya mawe