Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuzo ya mazingira ya UNEP 2022 yawaenzi warejesha mifumo ya ikolojia

Tuzo ya mazingira ya UNEP 2022 yawaenzi warejesha mifumo ya ikolojia
UNEP/Duncan Moore
Tuzo ya mazingira ya UNEP 2022 yawaenzi warejesha mifumo ya ikolojia

Tuzo ya mazingira ya UNEP 2022 yawaenzi warejesha mifumo ya ikolojia

Tabianchi na mazingira

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP leo limetangaza washindi wa tuzo yake kubwa kabisa ya mazingira Champion of the Earth 2022 ikiwaenzi mhifadhi wa mazingira, mfanyabiashara, mwanauchumi, mwanaharakati wa haki za wanawake, na mwanabiolojia wa wanyamapori kwa hatua zao za kuleta mabadiliko ya kuzuia, kusitisha na kubadili uharibifu wa mfumo ikolojia. 

Tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 2005, tuzo ya kila mwaka ya Mabingwa wa dunia imetolewa kwa wanaharakati walio mstari wa mbele katika juhudi za kulinda ulimwengu wetu wa asili.  

Ni heshima ya juu zaidi ya mazingira ya Umoja wa Mataifa. Hadi sasa, tuzo hiyo imewatambua washindi 111 wakiwemo viongozi wa dunia 26, watu binafsi 69 na mashirika 16.  

Mwaka huu ulivunja rekodi kwa mapendekezo 2,200 kutoka kote ulimwenguni yaliyopokelewa. 

Mkurugenzi mtendaji wa UNEP Inger Andersen amesema "Mifumo yenye afya, inayofanya kazi ni muhimu ili kuzuia dharura ya mabadiliko ya tabianchi na upotezaji wa bioanuwai kutokana na kusababisha uharibifu usioweza kurekebishwa kwa sayari yetu. Mabingwa wa dunia wa mazingira mwaka huu wanatupa matumaini kwamba uhusiano wetu na asili unaweza kurekebishwa. Mabingwa wa mwaka huu wanaonyesha kwamba kufufua mifumo ikolojia na kuunga mkono uwezo wa asili wa kufufua upya mifumo ya ikilojia ni kazi ya kila mtu, serikali, sekta ya kibinafsi, wanasayansi, jamii, NGOs na watu binafsi.” 

Mabingwa wa dunia 2022

  • Taasisi ya Arcenciel kutoka nchini Lebanon, taasisi inayoheshimiwa na inayoongoza ya mazingira ambayo kazi yake ya kuunda mazingira safi na yenye afya imeweka msingi wa mkakati wa kitaifa wa kudhibiti taka nchini humo. Leo, Arcenciel husafisha zaidi ya asilimia 80 ya taka za hospitali zinazoweza kusababisha maambukizi Lebanon kila mwaka. Leo, Arcenciel husafisha zaidi ya asilimia 80 ya taka za hospitali zinazoweza kusababisha maambukizi Lebanon kila mwaka.

 

  • Constantino Tino Aucca Chutas kutoka nchini Peru, pia ametunukiwa katika katika kitengo cha uchagizaji na hatua, ameanzisha mradi wa jamii wa upandaji miti unaoendeshwa na jamii na ja,mii za asili, ambao umesababisha miti milioni tatu kupandwa nchini Peru. Pia anaongoza juhudi kabambe za upandaji miti katika nchi zingine za Andean.

 

  • Sir Partha Dasgupta kutoka nchini Uingereza, aliyetunukiwa katika kitengo cha sayansi na ubunifu, ni mwanauchumi mashuhuri ambaye ukaguzi wake wa kihistoria kuhusu uchumi wa bayoanuwai unatoa wito wa kutafakari upya kwa msingi kuhusu uhusiano wa binadamu na ulimwengu wa asili ili kuzuia mifumo muhimu ya ikolojia kufikia kiwango cha hatari.

 

  • Dkt. Purnima Devi Barman kutoka nchini India, ametunukiwa katika kitengo cha maono ya ujasiriamali, ni mwanabiolojia wa wanyamapori ambaye anaongoza jeshi la Hargila, ambalo ni la harakati za uhifadhi wa wanawake watupu katika ngazi ya chini kabisa inayojitolea kulinda Ndege aina ya Stork Adjutant dhidi ya kutoweka. Wanawake hawa hutengeneza na kuuza nguo zenye michoro ya ndege hao, na kusaidia kuongeza ufahamu kuhusu aina hiyo ya ndege huku wakijikwamua kifedha.

 

  • Cécile Bibiane Ndjebet kutoka nchini Cameroon, aliyetunukiwa katika kitengo cha uchagizaji na hatua, ni mtetezi asiyechoka wa haki za wanawake barani Afrika katika kupata umiliki wa ardhi, ambayo ni muhimu ikiwa wanataka kuchukua jukumu katika kurejesha mifumo ya ikolojia, kupambana na umaskini na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Pia anaongoza juhudi za kushawishi sera kuhusu usawa wa kijinsia katika usimamizi wa misitu katika nchi 20 za Afrika.

 

Kuzuia na kubadili mifumo ya ikolojia 

Kufuatia kuzinduliwa kwa muongo wa Umoja wa Mataifa wa kurejesha mfumo wa Ikolojia kwa mwaka (2021-2030), tuzo za mwaka huu zinaangazia juhudi za kuzuia, kusitisha na kubadili uharibifu wa mfumo ikolojia duniani kote. 

Kwa mujibu wa UNEP mifumo ya ikolojia katika kila bara na katika kila bahari unakabiliwa na vitisho vikubwa.  

Kila mwaka, sayari hupoteza msitu unaolingana na ukubwa wa nchi ya Ureno. Bahari inavuliwa kupita kiasi na kuchafuliwa, huku tani milioni 11 za plastiki pekee zikiishia katika mazingira ya baharini kila mwaka.  

Aina milioni moja za viumbe ziko katika hatari ya kutoweka huku makazi yao yakitoweka au kuchafuliwa. 

Marejesho ya mfumo wa ikolojia ni muhimu kwa kuhakikisha ongezeko la joto duniani linasalia chini ya nyuzi joto 2°C na kusaidia jamii na uchumi kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.  

Pia ni muhimu katika kupambana na njaa, urejeshaji kupitia kilimo mseto pekee una uwezo wa kuongeza uhakika wa chakula kwa watu bilioni 1.3.  

UNEP imesema kurejesha asilimia 15 tu ya ardhi iliyobadilishwa kunaweza kupunguza hatari ya kutoweka kwa viumbe kwa asilimia 60.  

Urejeshaji wa mfumo ikolojia utafaulu tu ikiwa kila mtu atajiunga na harakati za #GenerationRestoration. 

Kuhusu tuzo ya UNEP ya mabingwa wa dunia 

Tuzo ya UNEP ya mabingwa wa dunia hutunuku watu binafsi na mashirika ambayo vitendo vyao vina athari nzuri za mabadiliko katika mazingira. Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka ya mabingwa wa dunia ni tuzo ya juu zaidi ya Umpoja wa Mataifa ya mazingira. Inatambua viongozi bora kutoka serikalini, mashirika ya kiraia, na sekta binafsi.