Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya #BringTheMoves kuhamasisha watoto kufanya mazoezi

Balozi Mwema wa WHO Didier Droger, mpiganaji wa kampeni ya #BringTheMoves, ambayo inahimiza vijana kufanya mazoezi.
© WHO
Balozi Mwema wa WHO Didier Droger, mpiganaji wa kampeni ya #BringTheMoves, ambayo inahimiza vijana kufanya mazoezi.

Kampeni ya #BringTheMoves kuhamasisha watoto kufanya mazoezi

Afya

Shirikisho la soka duniani FIFA na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kwa kushirikiana na wizara ya afya ya Qatar na kamati kuu ya uwasilishaji na historia  SC leo wamezindua kampeni ya #BringTheMoves challenge, ikiwachagiza wasakata kabumbu kwenye mashindano ya kombe la dunia la mwaka huu linaloanza jumapili Novemba 20 kutimiza changamoto waliyopewa kwenye mitandao ya kijamii  na mashabiki wao ya kuwachagiza Watoto na vijana kufanya mazoezi.

Rais wa FIFA Gianni Infantino amesema “ Tunafahamu athari mbaya za kiafya za kutofanya mazoezi kwa watoto na soka inaweza kutumia jukwaa hili la kombe la dunia kusambaza ujumbe huu muhimu na kuwashirikisha wote.” 

Hamasa hii inayotolewa si tu itawaleta karibu watoto na mashujaa wao wacheza soka mashuhuri duniani bali pia itatumia fursa ya kutangazwa mtandaoni kwa kombe la dunia kutuma ujumbe kwa kila mtu kuwa ni vyema kufanya mazoezi.

“Italeta kwa wazazi kwamba watoto wanatakiwa kufanya mazoezi kwa dakika 60 kila siku. Kwa sasa hili halifanyiki kwa kuzingatia takwimu zinazoonesha vijana barubaru asilimia 80 ulimwenguni kote hawafanyi mazoezi.”

Mali (13) na Dieumerci Mbokani  wa timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwenye mafunzo ya haki za mtoto kupitia soka.
© UNICEF/UN0658457/Josue Mulala
Mali (13) na Dieumerci Mbokani wa timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwenye mafunzo ya haki za mtoto kupitia soka.

Kuhusu #BringTheMoves

Katika Michuano hii ya kombe la dunia la FIFA mwaka 2022 watoto waliopo majumbani wanahamasishwa kutoangalia mpira pekee bali nao kushiriki kwa kucheza kwa namna mbalimbali na kisha waweke video zao kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia #BringTheMoves na wawaaambie wale wanasoka wanao wapenda nao wacheze kama walivyocheza wao/ wawaige.

Mcheza soka mashuhuri wa zamani raia wa Côte d’Ivoire na sasa ni Balozi mwema wa WHO Didier Drodba naye amehamasisha kampeni hii kabambwe ambayo lengo lake ni kujengea watoto utamaduni wa kufanya mazoezi na kusema kuwa

“Kampeni ya #BringTheMoves challenge inaleta faida nyingi kwa kila mtu, hasa kwa watoto wakiwa wanakuwa wanakuwa kimwili, kiakili na kijamii. Kufanya mazoezi ni kuzuri kwa mwili na akili na kunafanya kuwa na afya bora.”

Mwanasoka mwingine aliyezungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ni Golikipa Alisson Becker, naye ni Balozi Mwema wa WHO na atakuwepo nchini Qatar akichezea timu yake ya Taifa ya Brazil. Anasema anataka kutumia muda huu ambao macho na masikio ya kila mtu duniani yakiwa yameelekezwa kweney Kombe la Dunia la FIFA kuwahamasisha vijana chipukizi ku #BringTheMoves na kuwa wakakamavu.

“Naiunga mkono kampeni hii ya Bring the Moves kwasababu ninaamini watoto nivyema wawe wanajishughulisha. Wanahitajika kuwa wakakamavu kwa ajili ya Maisha bora ya baadae wakiwa wakubwa, ninaona wacheza mpira wanaweza kuwa wanawapa hamasa kubwa. Kwahiyo kama tukiwa tunafurahi nao na kuchezesha kidogo miili yetu vile wanavyotuambia, sote tutakuwa na furaha.”

Watoto wakiwa kwenye kituo rafiki huko kaskazini-kati mwa Burkina Faso.
© UNICEF/UN0640703/FrankDejongh
Watoto wakiwa kwenye kituo rafiki huko kaskazini-kati mwa Burkina Faso.

Uzinduzi wa App ya GenMove

Kampeni hii pia inawahamasisha watoto kupakua App ya GenMove ambayo inatumia akili bandia AI kuhamasisha watoto kuwa wanashughulisha mwili kila siku katika kipindi chote cha Kombe la dunia la FIFA.

Awamu ya kwanza ya GenMove itazinduliwa tarehe 19 Novemba  na waziri wa Afya ya Umma wa Qatar Dkt.Hanan Mohamed Al Kuwari na Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt.Tedros Ghebreyesus huko Qatar katika matembezi yaliyopewa jina la Okea kuhusu kutembea- Afya kwa wote.

Mpira wa Miguu, Musiki na furaha ni kiungo muhimu cha kuwafanya watu kuelekea kwenye afya bora. Amesema Dkt Tedrso na kuongeza kuwa “Wadau waetu Kombe la Dunia la FIFA na Wizaraya Afya ya Qatar katika kampeni hii ya Bring the Moves wote wanaleta pamoja watu mashuhuri wa kombe hili na watoto duniani kote, ili waweze kujishughulisha kokote walipo ulimwenguni na wawe na afya njema baadae.

Kampeni hii inayofanyika kwa ushirikiano wa WHO, FIFA na Wizara ya afya ya  Qatar inalenga kuonesha nguvu ya mpira wa miguu katika kulinda na kuhamasisha afya bora.

Soma zaidi kuhusu kampeni hiyo hapa.