Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yataka uwekezaji katika suluhu ya kwanza ya ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi inayolenga Watoto

Vanessa Nakate, Balozi mwema wa UNICEF, akiwa ziarani Turkana nchini Kenya alitembelea hospitali ya rufaa ya Lodwar na hapo anazungumza na mtoto Eunice Asukuku ambaye alifikishwa hospitali kwa tatizo la utapiamlo mkali, kuvimba mwili na ukosefu wa damu. …
© UNICEF/Translieu/Nyaberi
Vanessa Nakate, Balozi mwema wa UNICEF, akiwa ziarani Turkana nchini Kenya alitembelea hospitali ya rufaa ya Lodwar na hapo anazungumza na mtoto Eunice Asukuku ambaye alifikishwa hospitali kwa tatizo la utapiamlo mkali, kuvimba mwili na ukosefu wa damu. Chanzo cha matatizo ni uhaba wa chakula utokanao na ukame uliosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.

UNICEF yataka uwekezaji katika suluhu ya kwanza ya ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi inayolenga Watoto

Tabianchi na mazingira

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF leo limezindua mradi mpya wa ufadhili dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ili kuimarisha mnepo wa nchi dhidi ya janga hilo na kujiandaa kwa majanga mengine hususan kwa watoto na vijana na pia kuimarisha ulinzi kwa watoto kutokana na athari za majanga yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi kwa siku zijazo. 

Mradi huo uliopewa jina “Leo na Kesho” umezinduliwa mjini Sharm el-Sheikh Misri kunakofantika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP27 na ni suluhu jumuishi ya kifedha ya mabadiliko ya tabianchi ambayo, kwa mara ya kwanza, inachanganya ufadhili wa programu za haraka za kujenga mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kuzuia hatari kwa watoto leo, na matumizi ya ubunifu ya fedha za kuhamisha hatari zinazotolewa na soko la bima kwa majanga ya vimbunga kesho. 

Mradi huo unajikita nan chi 8 kwanza zilizoathirika Zaidi na vimbunga katika kanda mbalimbali ukiw ni jukwaa laufadjhili wa dola milioni 30 ili kuwasaidia watoto, vijana na wanawake milioni 15 kwa muda wa kuanzia  wa majaribio wa miaka 3.   

Jukwaa hilo la pamoja la ufadhili limeundwa ili kusaidia nchi kushughulikia athari za sasa na zinazoongezeka za changamoto  huku zikijiandaa kwa dharura za siku zijazo na kukabiliana nazo haraka zinapotokea. 

Hatari za mabadiliko ya tabianchi tayari tunaishi nazo 

"Hatari za mabadiliko ya tabianchi sio za nadharia tena tuko nazo. Na hata wakati tunafanya kazi ya kujenga mnepo wa jamii dhidi ya majanga ya mabadiliko ya tabianchi, tunapaswa kuwa na mbinu bora zaidi katika kuzuia hatari kwa watoto wetu. Tunajua maafa zaidi ya mabadiliko ya tabianchi yanatokea. Hatujui yatapiga wapi au lini.” Amesema Karin Hulshof, naibu mkurugenzi mtendaji wa UNICEF wa masuala ya ushirikiano. 

Watoto na vijana ni kundi la watu walio katika mazingira magumu sana ambalo ni miongoni mwa walioathirika zaidi na hatari za maafa na mabadiliko ya mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni pamoja na athari za matukio mabaya ya hali ya hewa kama vile vimbunga.  

UNICEF inakadiria kwamba mwaka jana, ilikuwa ni kielezo cha hatari ya mabadiliko ya tabianchi kwa watoto ilikadiria kwamba watoto milioni 400 (karibu mtoto 1 kati ya 6 ulimwenguni kote) kwa sasa wanakabiliwa na vimbunga. 

Katika majaribio yake ya awali ya miaka mitatu, mradi wa UNICEF wa “Leo na Kesho” utajikita na nchi nane katika maaeneo manne yanayoathirika sana na  vimbunga duniani  ambazo ni Bangladesh, Comoro, Haiti, Fiji, Madagascar, Msumbiji, Visiwa vya Solomon na Vanuatu.  

Ili kusongesha juhudi hizi mbele, UNICEF inachangisha dola milioni 30 kwa ajili ya mpango huo na inatoa wito kwa washirika wa ziada wa  sekta kibinafsi na wa sekta za umma kuchukua hatua na kujiunga na UNICEF katika kusaidia kuziba pengo linaloongezeka la ufadhili wa kibinadamu kwa ajili ya ulinzi wa maafa kwa watoto na vijana. 

Miale ya jua  ikipiga juu ya maji ya bahari ni alama ya matumaini kwamba bado watu wanaweza kubadili athari za mabadiliko ya tabianchi.
UN News/ Anton Uspensky
Miale ya jua ikipiga juu ya maji ya bahari ni alama ya matumaini kwamba bado watu wanaweza kubadili athari za mabadiliko ya tabianchi.

Athari za mabadiliko ya tabianchi kwa watoto ni za muda mrefu 

Madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwa wtoto hudumu maisha yao yote na kuendeleza ongezeko la pengo la usawa na umaskini katika vizazi hadi vizazi.  

Hata hivyo,UNICEF inasema mahitaji ya kipekee ya watoto “hayashughulikiwi moja kwa moja na mifumo iliyopo ya kupambana na hatari za mabadiliko ya tabianchi. Hii inaacha pengo la kimataifa la ufadhili wa kibinadamu, au pengo la ulinzi wa mtoto ambalo linajumuisha mamia ya mamilioni ya watoto na vijana duniani.” 

Mradi wa UNICEF wa “Leo na Kesho” ni utaratibu wa kwanza wa kufadhili hatari ya maafa ya mabadiliko ya tabianchi uliopangwa kwa msingi wa matukio ambao unalenga pengo hili la ulinzi wa mtoto, kwa msaada kamili wa sehemu ya chombo cha kudhibiti hatari, kinachoungwa mkono na setrikali za Ujerumani na Uingereza chini ya mwamvuli mpya uliozinduliwa nan chi za G7 uitwao V20 Global Shield wa kulinda Watoto dhidi ya hatari za mabadiliko ya tabianchi. 

"Tunafuraha kuiunga mkono UNICEF katika kuendeleza zana ya kwanza duniani ya ulinzi wa kifedha unaozingatia maslahi ya mtoto kwa hatari zinazohusiana na mabadiliko ya tabianchi na kuonyesha G7/V20 Global Shield  dhidi ya majanga ya mabadiliko ya tabianchi inafanya kazi," amesema Heike Henn, mkurugenzi katika wizara ya Ujerumani ya masuala ya anga, ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo (BMZ).  

Ameongeza kuwa "Tunatarajia kwamba mpango wa UNICEF wa Leo na Kesho utajikita katika maeneo matatu, mosi, kuongezeka kwa matumizi ya ufumbuzi wa zamani wa ufadhili  dhidi ya hatari unaofanywa na serikali kupitia kubadilishana ujuzi na kuongezeka kwa ujuzi na vyombo vya ufadhili dhidi ya hatari, pili, kuboreshwa kwa mnepo dhidi ya mshtuko wa kitaasisi na kiutendaji wa taasisi za maendeleo, na tatu na muhimu zaidi, kuziba pengo la ulinzi wa hatari za maafa kwa watu walio hatarini zaidi, haswa watoto na akina mama.” 

Naye Andrew Mitchell, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo wa Uingereza  amesema "Uingereza inajivunia kuwa mshirika katika Global Shield dhidi ya hatari za mabadiliko ya tabianchi na majanga, na kufadhili kwa pamoja kituo cha ufadhili cha Global Shield." 

Amesisitiza kuwa “Tunaunga mkono kwa dhati ufadhili huu uliopangwa mapema na wa msingi kwa sekta ya kibinadamu, na ninafurahi kwamba kituo kitapanua wigo wa kazi yake kama sehemu ya ngao, ikiwa ni pamoja na ruzuku hii mpya kwa UNICEF ili kuwawezesha kulinda hadi watoto milioni 15, vijana na familia zao kote barani Afrika, Caribbea, Asia na Pasifiki na kuchukua hatua haraka iwapo vimbunga vya kitropiki vitatokea."