Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfuko wa Udhamini wa UN: Jinsi biashara mpya zinaleta ustawi kwa walioathiriwa na unyanyasaji wa kingono

Mwanamke mwenye nywele zilizopambwa anaonekana kutoka nyuma, ameketi kwenye mashine ya kushona na akifanya kazi na kitambaa.
Trust Fund in Support of Victims Mfuko wa Ufadhili wa Kusaidia Waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia, SEA hutoa rasilimali na huduma kwa waathiriwa, pamoja na watoto waliozaliwa kwa sababu ya unyanyasaji na unyanyasaji wa kijinsia.

Mfuko wa Udhamini wa UN: Jinsi biashara mpya zinaleta ustawi kwa walioathiriwa na unyanyasaji wa kingono

Masuala ya UM

Kama yatima, nilikuwa na maisha mabaya. Sikuwa na baba wala mama. Nilianza kazi ya kujiuza nikiwa na umri mdogo sana, ni maneno ya mwanamke mmoja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye amepewa jina la bandia, ‘R’ ili kuhifadhi utu wake. 

Mwanamke huyu ni mmoja wa waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kingono ambao unafanywa na watu mbalimbali wakiwemo watumishi wa Umoja wa Mataifa wanaokuwa wametumwa kufanya kazi katika maeneo kama hayo ambako leo la Umoja wa Mataifa ni kwenda kuwasaidia watu walioko katika matatizo kama vile vita na majanga mengine.  

Mnamo Machi mwaka 2016, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliunda Mfuko wa Udhamini wa Kusaidia Wahathiriwa wa Unyonyaji na Unyanyasaji wa kijinsia, kama ilivyooneshwa katika ripoti yake kuhusu hatua Maalum za ulinzi dhidi ya unyanyasaji na unyanyasaji wa kijinsia (A/69/779). Mfuko huo unasaidia mashirika na mashirika ya Umoja wa Mataifa na yasiyo ya Umoja wa Mataifa ambayo hutoa usaidizi wa waathiriwa na huduma za usaidizi 

Delu Lusamba ni mmoja wa wadau ambao Umoja wa Mataifa wanashirikiana nao kupitia mfuko huo wa Umoja wa Mataifa anasema, “wanakimbia vijiji vyao hadi mahali panapoonekana kuwa salama kama vile karibu na kambi za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO, na huko hawana chochote. Wamepoteza kila kitu, wameacha kila kitu. Na katika hali hizi, kwa bahati mbaya, wako katika hatari ya kudhurumiwa kingono na kunyanyaswa kijinsia.” 

Kusaidia waathiriwa wa unyanyasaji uliofanywa na  wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na walinzi wa amani Mfuko maalumu wa UN hufanya kazi na wadau wa ndani ili kujenga ujasiri kati ya wale walioathirika au walio katika hatari. 

Olivier Akili Muyindo, ni Afisa anayehusika na masuala ya tabia katika MONUSCO anaeleza namna wazo la miradi wanayoitekekeza watu kama ‘R’ lilivyokuja, “tuligundua kuwa itakuwa bora kuunda mradi ambao unaboresha ujuzi wao, ili wajifunze ufundi ambao utakidhi mahitaji yao ya kila siku.” 

‘R’ na wenzake waliichangamkia miradi hiyo inayofadhili na mfuko huo maalumu unaowalenga walioathiriwa na matendo hayo mabaya yasiyokubalika, “tukaanza kujifunza batiki,” anaeleza “R” akiongeza kwa kusema, “wakatufundisha jinsi ya kutengeneza rangi kutoka katika magamba ya miti.” 

‘R’ ni miongoni mwa wanufaika 400 walionufaika na mfuko wa UN nchini DRC na Haiti na anashukuru sana akisema, “ninashukuru Mungu kuona nilijifunza kutengeneza batiki. Hivi sasa ninaweza kufanya vitu viwili. Kushona na kutengeneza batiki. Inanisaidia ninaweza kuuza bidhaa zangu na silali njaa. Maisha yangu yamebadilika. Ninajisikia vizuri. Ninavaa vizuri. Watoto wangu hawatadharauliwa tena katika eneo hili.”