Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Njaa ikibisha hodi Somalia mkuu wa OCHA awasili Moghadishu kujionea hali halisi

Wanawake wanasubiri msaada wa chakula katika kituo cha usambazaji huko Afgoye, Somalia.
UN Photo/Tobin Jones
Wanawake wanasubiri msaada wa chakula katika kituo cha usambazaji huko Afgoye, Somalia.

Njaa ikibisha hodi Somalia mkuu wa OCHA awasili Moghadishu kujionea hali halisi

Msaada wa Kibinadamu

Mratibu mkuu wa masiuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths leo ameanza ziara nchini Somalia kushuhudia hali halisi ya njaa na kutathimini mahitaji ya walioathirika na hatua zinazochukuliwa kuwasaidia. 

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada yad harira OCHA karibu nusu ya Wasomali wote wanaokadiriwa kuwa watu milioni 7.8 wameathirika ukame mkali kuwahi kushuhudiwa kwa miongo minne na sasa katika miezi ijayo wanakabiliwa na msimu wa tano bila mvua. 

Shirika hilo limeongeza kuwa takriban Wasomali milioni 1 wametawanywa na ukame, na wengine Zaidi ya 213,000 wanakabiliwa na tishio kubwa la Maisha yao kwa sababu ya janga la kutokuwa na uhakika wa chakula. 

“Kuna hatari kubwa ya baa la njaa endapo uzalishaji wa mazao na mifugo utafeli. bei ya chakula inaendelea kupanda, na wale wenyeuhitaji zaidi hawapati msaada.” limesema shirika la OCHA. 

Mashirika ya misaada yaliyoko nchini humo yanafanya kila wawezalo kuokoa maisha na riziki za waathirika.  

“Hadi kufikia mwisho wa Julai, walikuwa wametoa msaada kwa watu milioni 5.3.” 

Mratibu huyo wa misaada ya dharura Bwana. Griffiths akiwa katika zira hiyo atakutana na jamii zilizoathirika, maafisa wa serikali na mashirika wadau. Pia atakagua juhudi za pamoja za kuongeza haraka operesheni za misaada na kujadili hatua zilizopigwa na changamoto.