Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa ridhieni Mkataba wa kufanya kazi na kikosi cha kukomesha utoweshwaji wa binadamu: Guterres

Janga la COVID-19 limezidisha athari kwa waathiriwa wa kutoweka kwa kulazimishwa na jamaa zao.
Unsplash/Tao Yuan
Janga la COVID-19 limezidisha athari kwa waathiriwa wa kutoweka kwa kulazimishwa na jamaa zao.

Mataifa ridhieni Mkataba wa kufanya kazi na kikosi cha kukomesha utoweshwaji wa binadamu: Guterres

Haki za binadamu

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kukumbuka manusura na waathirika wa vitendo cha kutoweshwa duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa mataifa yote duniani kuridhia Mkataba na kufanya kazi na Kamati ya Umoja wa Mataifa na Kikosi Kazi cha Kutoweshwa kwa Kulazimishwa.

Katika taarifa yake aliyoitoa leo jijini New York Marekani Guterres amesema anaamini kwa pamoja, inawezekana na ni lazima tukomeshwe upotevu wowote wa watu unaotekelezwa mahali popote .

“Kutoweshwa kwa kulazimishwa wakati kumepigwa marufuku kabisa chini ya sheria ya kimataifa ya haki za binadamu katika hali zote, kunaendelea kutumika kote ulimwenguni kama njia ya ukandamizaji, ugaidi, na kukandamiza upinzani. Chakushangaza, wakati mwingine hutumiwa kwa kisingizio cha kukabiliana na uhalifu au ugaidi. Wanasheria, mashahidi, upinzani wa kisiasa, na watetezi wa haki za binadamu wako hatarini.” Amesema Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.

Guterres ameeleza kuwa kutoweshwa kwa nguvu kunanyima familia na jamii haki ya kujua ukweli kuhusu wapendwa wao, uwajibikaji, haki na fidia.

“Janga la coronavirus">COVID-19 limeongeza machungu na maumivu makali kwa ndugu wa walioteweshwa kwa kulazimishwa, kwa kupunguza uwezo wa kuwatafuta watu waliopotea na kuchunguza madai ya kutoweka.” 

Amesisitiza kuwa mkataba wa Ulinzi wa Watu Wote dhidi ya kutoweshwa ni muhimu sana katika kusaidia kukabiliana na tabia hii ya woga.

“Lakini inahitaji utashi na kujitolea kwa wale walio na uwezo wa kufanya hivyo.” Amesisisiza Gutettes na kusema kuwa mataifa yote lazima yatimize wajibu wao wa kuzuia watu kutoweshwa kwa nguvu, kutafuta waathirika, na kuchunguza, kuwashtaki na kuwaadhibu wahusika.”