Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

‘Hakikisheni waathirika wa ugaidi hawasahauliki kamwe’: Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Masalia ya jengo la Hotel ya Canal huko Iraw lililolipuliwa mwaka 2003
UN News
Masalia ya jengo la Hotel ya Canal huko Iraw lililolipuliwa mwaka 2003

‘Hakikisheni waathirika wa ugaidi hawasahauliki kamwe’: Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Amani na Usalama

Hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa pongezi kwa wahanga wa ugaidi, kuadhimisha siku ya kimataifa iliyoanzishwa ili kuhakikisha kuwa "waathirika na walionusurika wanasikilizwa kila wakati na kamwe hawatasahaulika."

Kila mwaka, vitendo vya kigaidi vinadhuru na kuua maelfu ya watu wasio na hatia. Licha ya uangalizi wa kimataifa, walioathirika mara nyingi wanatatizika kupata huduma muhimu za kimwili, kisaikolojia, kijamii na kifedha.

Laura Dolci, mwathirika wa Mlipuko wa Bomu kwenye Hoteli ya Canal nchini Iraq mwaka 2003, ambapo wafanyakazi 22 wa Umoja wa Mataifa waliuawa, na zaidi ya 100 kujeruhiwa, aliripoti kwamba, "kuna maelfu ya waatharika wa ugaidi na familia zao waliotawanyika katika maeneo yote ya dunia, wakijitahidi kuishi katika upweke wao wakiwa na makovu ya kiwewe na majeraha.”

Kukumbuka na kutoa heshima kwa waathirika wa ugaidi kuna chukua jukumu kuu katika kuonyesha kwamba hali yao kama wathirika inaheshimiwa na kutambuliwa.

Siku ya mwaka huu inaenda sambamba na maadhimisho ya dunia kupiti lkutoka kwenye dharura ya afya ya umma iliyosababishwa na janga la COVID-19, mzozo ambao unaongeza mapambano ambayo tayari wanakabiliwa na waathirika wa ugaidi.

Kaulimbiu ya Siku ya mwaka huu, iliyochaguliwa kufuatia mashauriano na waathiriwa, ni "Kumbukumbu"; kumbukumbu huunganisha watu pamoja na kuashiria ubinadamu wetu wa kawaida. Kwa upande wa ugaidi, kumbukumbu za hasara na maumivu huunganisha jamii pamoja, kuruhusu kubadilishana mawazo na kutoa suluhu zinazolengwa.

Mtazamo wa Umoja wa Mataifa kuhusu matibabu ya waathiriwa wa ugaidi unawakilisha kipengele muhimu cha Mkakati wa Kimataifa wa Kupambana na Ugaidi wa shirika hilo. Waathiriwa wa ugaidi wana jukumu muhimu katika kukuza mshikamano wa kimataifa, kuzuia itikadi kali za kikatili, na kudumisha haki za binadamu.

Myazidi kutoka Sinjar  nchini Iraq ambaye alitekwa nyara na kikundi cha ISIL, hapa yuko kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani  ya Mamilyan  huko Akre, nchini Iraq
Giles Clarke/ Getty Images Reportage
Myazidi kutoka Sinjar nchini Iraq ambaye alitekwa nyara na kikundi cha ISIL, hapa yuko kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Mamilyan huko Akre, nchini Iraq

Katika mapitio ya 2021 ya Mkakati huu, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilibainisha jukumu muhimu la waathiriwa wa ugaidi katika kuunda sera zinazowalenga. Azimio lililopitishwa baada ya kuhitimishwa kwa tathmini hii, lilitaka Nchi Wanachama kuunda mpango wa kina wa usaidizi wa kitaifa kwa waathirika  wa ugaidi, haswa vikundi vilivyokandamizwa kihistoria.

Katika tafakari yake ya kuhitimisha lengo la Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu alisema lengo ni kuhamasisha, "Nchi Wanachama kutoa msaada wa kisheria, matibabu, kisaikolojia, au kifedha wanayohitaji [wahanga wa ugaidi] ili kuponya na kuishi kwa utu.”

Dolci vile vile alisema kwamba, "kusaidia waathirika wa ugaidi si tendo la hisani: inapaswa kuwa ushirikiano wa kimataifa, unaozingatia wajibu wa Marekani na kuungwa mkono kwa nguvu na Umoja wa Mataifa."