Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Napanda milima kuhakikisha mjukuu wangu anapata tiba ya Utapiamlo

Rahot akiwa na mjukuu wake, Hassan, kijijini ambako alihamia karibu na kituo cha lishe kinachoendeshwa na SCI na kufadhiliwa na SHF.
Sara Awad – Save the Children
Rahot akiwa na mjukuu wake, Hassan, kijijini ambako alihamia karibu na kituo cha lishe kinachoendeshwa na SCI na kufadhiliwa na SHF.

Napanda milima kuhakikisha mjukuu wangu anapata tiba ya Utapiamlo

Afya

Kila siku asubuhi na mapema kukipambazuka na jua kuchomoza Rahot mwenye umri wa miaka 55 huamka na kumbeba mgongoni mjukuu wake Hassan tayari kwakuaza safari ya takriban kilometa 20 yenye vilima kwenda kituo cha kumpatia lishe mjukuu huyo ili kuokoa maisha yake kutokana na kuwa na utapiamlo mkali. 

 

Mkazi huyu wa jimbo la Red Sea nchini Sudana anasema zoezi hili sasa amelizoea kwakuwani takriban miezi minne tangu familia yake kupata habari za tetesi za uwepo wa kituo kinachosaidia kupima watoto wanaumwa na kuwapatia matibabu na chakula cha kuboresha afya zao. 

Akisimulia historia ya mjukuu wake anakumbuka kipindi ambacho familia yao ilikuwa na wasiwasi na hali ya Hassan kwa mara ya kwanza “Alikuwa mgonjwa sana, amekonda na amedhoofika, afya yake ilikuwa imezorota” mjukuu huyo alikuwa na umri wa miezi 12. 

Anaendelea kusimulia kuwa “Tulikuwa tunaishi katika kijiji cha mbali zaidi. Kupitia taarifa za watu tulisikia kuhusu huduma za lishe kituoni hapa. Tuliamua kuhamia kijiji cha karibu na kituoni hapo ili iwe rahisi kumpeleka mtoto kituoni hapo.” Jukumu hilo akiwa nalo yeye huku binti yake aitwaye Fatima akibaki nyumbani na watoto wake wengine wanne wakati yeye akipanda vilima kumpeleka mtoto kituoni. 

Alipofika katika kituo hicho kinachosimamiwa na shirika la Save the Childrene SCI kwakushirikiana na Mfuko kwa kibadamu wa Sudan SHF, mtoto wake baada ya kupimwa aligundulika kuwa na tatizo la utapiamlo, kwa Sentimeta 10.2 hii ikimaanisha ni utapiamlo mkali kutokana na kuwa na kilo 5.7 na urefu wa Sentimenta 65.5. Bila kupoteza muda aliandikishwa kwenye programu ya wanaopokea chakula cha lishe kilicho tayari kutuika kwa matibabu.

Rekodi ya watu milioni 11.7, karibu robo ya wakazi wa Sudan, wanatarajiwa kukabiliwa na njaa katika kilele cha msimu wa mwambo mwezi Septemba.
©FAO/Ahmedalidreesy Adil
Rekodi ya watu milioni 11.7, karibu robo ya wakazi wa Sudan, wanatarajiwa kukabiliwa na njaa katika kilele cha msimu wa mwambo mwezi Septemba.

Njaa ndio sababu

Njaa hususan kwa watoto wadogo ina madhara makubwa kwa mtoto kwa Maisha yake ya sasa na baadae katika ukuaji wake huku ikiongeza vifo vya watoto wadogo, kuchelewesha ukuaji wao na hata kupata ulemavu. Pia njaa inahusishwa na matatizo ya utambuzi na tabia kwa watoto hasa hutokea watoto wangali wadogo. 

Akielezea historia ya familia yake wanayoishi katika jimbo la Red Sea nchini Sudan ambalo nalo limekumbwa na ukame mkali kama maenoe mengi ya Pembe ya Afrika anasema mara nyingi hawana fedha za kutosha kununua chakula kwa ajili yao na familia.

Baba yake Hassana alivyoona Maisha yanazidi kuwa magumu aliamua kuondoka nyumbani kwenda jimbo la Port Sudan katika mji mkuu kwa ajiku ya kutafuta ajira ili kujipatia kipato hata hivyo hutuma fedha mara chache kwa mwezi ambazo haziwatoshi kwa ajili ya chakula na mahitaji mengine ya familia. 

“Tunakula Kissra (Mkate mnene) na Aseeda (Uji) kila siku. Hatuli kitu kingine chochote. Pia vyanzo vya maji nivichache na vipo mbali na si mara zote tunapata maji masafi”. Alieleza Tahot 

Kwa mujibu wa takwimu za usalama wa chakula, zaidi ya theluthi moja wa wakazi wa jimbo la Red Sea wanakabiliwa na dharura ya chakula katika msimu muu wa mwambo kutokana na mvua mwaka jana kunyeesha katika kiwango kidogo na hivyo kushindwa kulima .

Hali hii ina maanisha kuwa familia nyingi zimegeukia katikakubuni mbinu za hatari za kukabiliana na hali hiyo kama vile kuwaoza Watoto wao wakiwa na umri mdogo, kuwapeleka kusaka ajira wangali Watoto au kupunguza kiasia na aina ya chakula wanachokula kwa viwango ambavyo havifai kwa afya. 

Kipimo cha Hassan sasa ni 12 cm, ikionesha utapiamlo wa wa wastani na hali inazidi kuimarika
Sara Awad – Save the Children
Kipimo cha Hassan sasa ni 12 cm, ikionesha utapiamlo wa wa wastani na hali inazidi kuimarika

Sasa mambo yamebadilika

Kwa saa Rahot na familia yake wanafarijika afya ya Hassan imeimarika kwa kiasi kikubwa tangu aanze kupata usaidizi wa kituo cha SCI na SHF. Matabiliko haya ya miezi minne tu yamemtoa Hassan kutoka katika mzunguko mwekundu hadi wa njayo wa utapiamlo sasa urefu wa kipimo ni Sentimenta 12 ikimaanisha ametoka kwenye utapiamlo mkali na sasa anaelekea kupona. 

Bibi yake Rahot bado anaendelea kujitolea kupanda vilima lakini ni safari ya kila wiki kwenda kituoni “Sitaki kukosa miadi yake yoyote, natamani kumuona mjukuu wangu akizidi kukuwa na nitaka kumuona akiwa mtu anayesoma. Watendaji wa kituoni pia wanatufafanulia ni aina gani za vyakula vinafaa kwa watoto na jisni ya kuwalisha ili wapate lishe bora” 

Kwa sasa Hassan anauzito wa Kg 7 na urefu wa 70 cm ingawa afya yake imeimarika bado anaendelea kupata lishe ya ziada hadi hapo atakapo pona kabisa. 

Kuhusu mradi

Shughuli za lishe zinafadhiliwa kupitia mradi wa sekta mbalimbali unaofadhiliwa na SHF, ambao ulianza mwezi Desemba 2021, unaohusu afya, lishe, ulinzi wa mtoto, maji, usafi wa mazingira na afua za usafi. Pesa za ziada zilipokelewa mwezi Mei 2022 kwa shughuli za lishe ili kushughulikia mahitaji yanayoongezeka.

Ili kuendeleza shughuli hizi, SCI ilipokea dola milioni 2  mwanzoni mwa mwezi huu wa mwezi Agosti 2022 kupitia Ugawaji wa Kawaida, ikijumuisha kipengele cha elimu ya ziada.