Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wapongeza wananchi wa Kenya kwakushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani

Shule na kituo cha Kakenya Dreams kilichoko nchini Kenya
Thelma Mwadzaya
Shule na kituo cha Kakenya Dreams kilichoko nchini Kenya

Umoja wa Mataifa wapongeza wananchi wa Kenya kwakushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza wananchi wa kenya kwa kupiga kura kwa amani wakati wa Uchaguzi Mkuu wan chi hiyo uliofanyika hapo jana Agosti 9, 2022

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu Stéphane Dujarric kutoka New York Marekani imesema Katibu Mkuu anatambua kazi muhimu iliyofanywa na mamlaka ya Kenya pamoja na mashirika mengi yote yanayohusika na usimamiz wa uchaguzi, ushirikishwaji wa wadau mbalimbali wa kitaifa na dhamira ya dhati isiyoyumbishwa ya wapiga kura kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura. 

“Katibu Mkuu ana imani wadau wote wa kisisasa na wananchi wa Kenya wataendelea kuonesha kiwango hicho hicho cha utulivu, Subira na heshima kwa mchakato huo wa uchaguzi wakati huu wakisubiri kutangazwa kwa matokeo ya kura kwa mujibu wa muda uliowekwa kisheria” amesema Dujarric 

Katibu Mkuu amesisitiza uwepo wa Umoja wa Mataifa kuendelea kuunga mkonoi juhudi zote zinazofanyw ana mamlaka ya nchi hiyo na wananchi wote wa Kenya ili kuhakikisha wanaendeleza mchakato wa kidemokrasia nchini humo.