Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WMO: Mwezi Julai ulirekodi joto kali, Ukame na Moto wa nyika kwa wakati mmoja

Ulimwenguni, mwezi Julai 2022 ulikuwa moja ya Julai tatu zenye joto zaidi kwenye rekodi.
Unsplash/Todd Kent
Ulimwenguni, mwezi Julai 2022 ulikuwa moja ya Julai tatu zenye joto zaidi kwenye rekodi.

WMO: Mwezi Julai ulirekodi joto kali, Ukame na Moto wa nyika kwa wakati mmoja

Tabianchi na mazingira

Huku kukiwa na joto kali, ukame na moto wa nyika, sehemu nyingi za dunia zilikuwa zimepitia mojawapo ya Julai tatu zenye joto zaidi katika rekodi, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa WMO hii leo.

Kulingana WMO, halijoto ilikuwa karibu na 0.4℃ juu ya wastani wa mwaka 1991-2020 kote Ulaya, huku kusini-magharibi na magharibi mwa Ulaya ikiwa maeneo ya juu zaidi ya wastani, kwa sababu ya wimbi la joto kali karibu katikati ya Julai.

"Hii ni licha ya tukio la La Niña ambalo linakusudiwa kuwa na ushawishi wa kupoa kwa hali ya hewa," alieleza msemaji wa WMO Clare Nullis.

"Tuliona hii katika baadhi ya maeneo, lakini si duniani kote," aliongeza, akibainisha kuwa ilikuwa "moja ya joto zaidi [Julai] kwenye rekodi, baridi kidogo kuliko Julai 2019, joto la mwaka 2016 lakini tofauti iko karibu sana".

Muonekano wa joto kwenye uso wa dunia
WMO
Muonekano wa joto kwenye uso wa dunia

Rekodi ya halijoto duniani

Nchi za Ureno, Ufaransa magharibi na Ireland zilivunja rekodi ya juu, huku Uingereza ikipata joto 40℃ kwa mara ya kwanza kabisa.

Rekodi za kitaifa za wakati wote za viwango vya juu vya joto vya kila siku pia zilivunjwa huko Wales na Scotland.

Hispania pia ilikuwa na mwezi wake wa joto zaidi katika rekodi mnamo Julai, na wastani wa halijoto ya kitaifa ya 25.6 ° C na wimbi la joto kutoka tarehe 8 hadi 26 Julai ambalo lilikuwa kali zaidi na lililodumu kwa muda mrefu zaidi kwenye rekodi.

Kwa kutumia takwimu kutoka Tume ya Ulaya ya Huduma ya Mabadiliko ya tabianchi ya Copernicus, Shirika hilo la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa lilithibitisha kuwa Ulaya ilikuwa na Julai ya sita kwa joto zaidi.

Joto hilo lilisafiri zaidi kaskazini na mashariki likileta halijoto ya juu sana katika nchi nyingine, ikijumuisha Ujerumani na sehemu za Skandinavia, huku rekodi za ndani za Julai na za wakati wote zikivunjwa katika maeneo kadhaa nchini Sweden.

Maelfu ya wanyama wameangamia kutokana na ukame uliokithiri unaoikumba Somalia na maeneo mengine ya Pembe ya Afrika.
IOM
Maelfu ya wanyama wameangamia kutokana na ukame uliokithiri unaoikumba Somalia na maeneo mengine ya Pembe ya Afrika.

Matatizo ya joto

Wakati huo huo, kutoka Pembe ya Afrika hadi kusini mwa India, na sehemu kubwa ya Asia ya kati hadi sehemu kubwa ya Australia ilikumbwa na halijoto ya chini ya wastani.
Isitoshe, halijoto kwa ujumla ilikuwa chini ya wastani nchini Georgia na sehemu kubwa ya Uturuki

Barafu ya mlima ambayo inapungua kwa sababu ya halijoto inayoongezeka na theluji kidogo katika Wilaya ya Kargil, India.
© UNICEF/Srikanth Kolari
Barafu ya mlima ambayo inapungua kwa sababu ya halijoto inayoongezeka na theluji kidogo katika Wilaya ya Kargil, India.

Kupungua kwa barafu 

Julai pia iliona barafu ya chini kabisa ya Bahari ya Antarctic kwenye rekodi, ikiwa ni asilimia saba chini ya wastani.

Barafu ya Bahari ya Arctic ilikuwa asilimia nne chini ya wastani, ikiorodheshwa katika nafasi ya 12 chini ya Julai kulingana na rekodi za satelaiti.

WMO ilitoa mfano wa Huduma ya Mabadiliko ya tabianchi ya Copernicus kwa kusema kwamba mkusanyiko wa barafu katika Bahari ya Arctic ulikuwa wa chini zaidi kwa mwezi Julai kwenye rekodi ya satelaiti, ambayo ilianza mwaka wa 1979, na barafu ya bahari ilikuwa ya 12 chini kabisa kuwahi kutokea.

Glaciers wameona "majira ya joto ya kikatili, kikatili sana," Nullis aliendelea. "Tulianza na theluji nyingi kwenye milima ya barafu, iliyoripotiwa na huduma za hali ya hewa, na sasa mawimbi ya joto yanayofuatana hii ni habari mbaya kwa barafu huko Ulaya. Picha ya barafu ya Greenland imechanganya zaidi, hata hivyo, kwani hakujawahi kuwa na joto lisiloisha”.

Katika hali ya joto, Katibu Mkuu wa WMO Petteri Taalas alisema katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 18 Julai, "aina hii ya wimbi la joto ni hali mpya ya kawaida".