Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei za vyakula zashuka katika soko la dunia kwa mwezi Julai

Bei ya ngano ilishuka mnamo Julai ikisukumwa na usambazaji mkubwa wa kimataifa na matarajio ya upatikanaji mwingi wa kuuza nje kutoka eneo la Bahari Nyeusi.
FAO/Danfung Dennis
Bei ya ngano ilishuka mnamo Julai ikisukumwa na usambazaji mkubwa wa kimataifa na matarajio ya upatikanaji mwingi wa kuuza nje kutoka eneo la Bahari Nyeusi.

Bei za vyakula zashuka katika soko la dunia kwa mwezi Julai

Ukuaji wa Kiuchumi

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO hii leo limetangaza bei za vyakula zilishuka kwa kiasi kikubwa mwezi Julai,2022 na kuashiria kushuka kwa mwezi wa nne mfululizo tangu zilipoweka rekodi ya juu zaidi mwanzoni mwa mwaka kufuatia vita ya Ukraine.

Taarifa ya FAO imeyotolewa leo kutoka Rome Italia imeeleza Fahirisi ya Bei ya Chakula inayokuwa ikisubiriwa kwa hamu, katika kipimo hiki ambacho taarifa za mabadiliko ya bei zimekuwa zikitolewa kila mwezi kwa kuangalia bei za kimataifa za bidhaa tano za vyakula ambazo ni: nafaka, mafuta ya kupikia, bidhaa za maziwa, nyama na sukari ilikuwa na ilikuwa na wastani wa pointi 140.9 mwezi Julai sawa na  pointi 8.6 chini ikilinganishwa na mwezi Juni. 

Kupungua huko kulitokana na kushuka kwa asilimia mbili kwa bei ya mafuta yakupikia lakini pia nafaka, huku makubaliano ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa kuhusu mauzo ya nafaka za Ukraine yakichangia punguzo hilo .

Nafaka. Ripoti mpya ya FAO inasema mataifa maskini hutumia pesa nyingi kununua chakula kidogo.
Picha: FAO/Danfung Dennis
Nafaka. Ripoti mpya ya FAO inasema mataifa maskini hutumia pesa nyingi kununua chakula kidogo.

Bei nzuri lakini tuchukue tahadhari

“Kushuka kwa bei za bidhaa za chakula kutoka viwango vya juu sana kunakaribishwa, hasa tukiutaza kwa jicho la upatikanaji wa chakula,” amesema Maximo Torero, Mchumi Mkuu wa FAO.

“Hata hivyo, mambo mengi ya kutokuwa na uhakika yameendelea kusalia, ikiwa ni pamoja na bei ya juu ya mbolea ambayo inaweza kuathiri matarajio ya uzalishaji wa siku zijazo na maisha ya wakulima, hali mbaya ya kiuchumi ya kimataifa, na mienendo thamani ya fedha kuyumba ambayo yote yanaleta matatizo makubwa kwa uhakika wa chakula duniani.”

Mwezi Julai, Fahirisi bei ya mboga ya FAO ilipungua kwa asilimia 19.2 ikilinganishwa na mwezi Juni, ikiashiria kiwango cha chini kwa miezi 10. Nukuu za kimataifa za aina zote za mafuta zilishuka, shirika hilo lilisema, huku bei ya mafuta ya mawese ikipungua kutokana na matarajio ya kupatikana kwa wingi kutoka kwenye nchi wazalishaji mfano Indonesia.

Bei ya mafuta ya alizeti pia ilishuka kwa kiasi kikubwa kutokana na kupungua kwa mahitaji ya uagizaji bidhaa duniani, licha ya kutokuwa na uhakika usafirishaji katika eneo la Bahari Nyeusi. Thamani za mafuta ya yakupikia pia zilishushwa na bei ya chini ya mafuta ya kisukuku.

Shehena ya kwanza ya tani 26,000 ikiwa na nafaka kutoka Ukraine ikipita Bahari Nyeusi kuelekea kuuzwa soko la kimataifa huko Lebanon
© UNOCHA
Shehena ya kwanza ya tani 26,000 ikiwa na nafaka kutoka Ukraine ikipita Bahari Nyeusi kuelekea kuuzwa soko la kimataifa huko Lebanon

Mpango wa kuuza nje wa Bahari Nyeusi

Fahirisi ya bei ya nafaka pia ilionesha kupungua kwa asilimia 11.5 mwezi uliopita, ingawa ilibaki asilimia 16.6 zaidi ya Julai 2021. Bei za nafaka zote kwenye fahirisi zilipungua, zikiongozwa na ngano.

Bei ya ngano duniani ilishuka kwa kiasi cha asilimia 14.5, FAO ilisema, kwa kiasi fulani kutokana na makubaliano ya Urusi na Ukraine kuhusu mauzo ya nafaka kutoka bandari kuu za Bahari Nyeusi, na pia kwa sababu ya kupatikana kwa msimu kutokana na mavuno yanayoendelea katika mataifa ya ulaya.

Mwezi Julai pia ilishuka kwa asilimia 11.2 kwa bei mbaya ya nafaka. Mahindi yalipungua kwa asilimia 10.7, tena kutokana na Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi na kuongezeka kwa upatikanaji wa msimu nchini Argentina na Brazil. Zaidi ya hayo, bei ya mchele wa kimataifa pia ilipungua kwa mara ya kwanza mwaka huu.

Habari Njema

Fahirisi ya bei ya Sukari ilishuka kwa karibu asilimia nne, huku kukiwa na wasiwasi juu ya matarajio ya mahitaji kutokana na matarajio ya kudorora zaidi kwa uchumi wa dunia, kudhoofika kwa sarafu ya Brazili, bei ya chini ya ethanoli na kusababisha uzalishaji mkubwa wa sukari kuliko ilivyotarajiwa hapo awali.

Hali ya kushuka pia iliathiriwa na dalili za mauzo ya nje na matarajio mazuri ya uzalishaji nchini India. Wakati huo huo, hali ya hewa ya joto na kavu katika nchi za Umoja wa Ulaya pia ilizua wasiwasi juu ya mavuno ya miwa yakutengeneza sukari na kuzuia kupungua kwa kasi.

FAO iliripoti zaidi kwamba Fahirisi ya Bei ya Maziwa ilipungua kwa asilimia 2.5 “huku kukiwa na shughuli duni ya biashara”, lakini bado ilikuwa wastani wa asilimia 25.4 juu ya Julai 2021.

Wakati bei za unga wa maziwa na siagi zilipungua, bei ya jibini ilibakia kuwa tulivu, ikiongezwa na mahitaji katika maeneo ya utalii ya Ulaya.

Nyama ikiwa katika soko la Hamarwayne, Mogadishu Somalia.
AMISOM/Omar Abdisalan
Nyama ikiwa katika soko la Hamarwayne, Mogadishu Somalia.

Bei ya nyama ni juu chini

Bei ya nyama pia iliendelea kudorora, ikishuka kwa nusu asilimia kuanzia Juni kutokana na kudhoofika kwa mahitaji ya kuagiza bidhaa kutoka nje. 

Hata hivyo, bei ya kuku ilifikia kiwango cha juu zaidi, ikichochewa na mahitaji ya uagizaji bidhaa na ugavi wa kutosha kutokana na milipuko ya homa ya mafua ya ndege katika ulimwengu wa kaskazini.

Fahirisi ya Bei ya Nyama ya FAO pia ilipungua mwezi Julai, kwa asilimia 0.5 kuanzia Juni, kutokana na kudhoofika kwa mahitaji ya kuagiza nguruwe na nyama nyingine.

Kinyume chake, bei ya nyama ya kuku ya kimataifa ilifikia kiwango cha juu kabisa, ikichagizwa na mahitaji ya kimataifa ya uagizaji bidhaa na usambazaji mdogo kutokana na milipuko ya mafua ya ndege katika ulimwengu wa kaskazini.