Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yawaleta pamoja wadau kujadili ubora wa udongo kwa mustakabali wa chakula bora

Mwanamke akivuna majani ya chai katika eneo la Mto Tana nchini Kenya
© CIAT/Georgina Smith
Mwanamke akivuna majani ya chai katika eneo la Mto Tana nchini Kenya

FAO yawaleta pamoja wadau kujadili ubora wa udongo kwa mustakabali wa chakula bora

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO linaendesha kongamano la siku nne kwa njia ya mtandao kujadili masuala mbalimbali kuhusu udongo na mchango wake katika kuhakikisha jamii inapata lishe bora kutokana na mazao yalimwayo kwenye udongo.

Taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti ya FAO imesema kongamano hilo lililoanza leo Julai 26 mpaka 29, 2022 lenye kauli nbiu “Udongo, mahali chakula kinapoanzia” linalenga kufanya uhakiki wa hali ya udongo duniani na changamoto za ardhi yenye rutuba ikihusisha mazao, wanyama na lishe ya wanadamu.

Kongamano hilo linawaleta pamoja wadau mbalimbali wa udongo wakiwemo wanasayansi, mashirika ya kimataifa, asasi za kiraia, watumiaji wa ardhi ikiwemo watu wa asili. Viongozi wa ngazi za serikali za mtaa, makampuni na wawakilishi wa viwanda nao wanashiriki katika mjadala huo ambapo pia upo wazi kwa watu wote kushiriki kwa njia ya mtandao.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye uratibu wa harakati za kuongeza lishe Gerda Verburg ni mmoja wa wazungumzaji katika kongamano hilo ambaye anaeleza kuwa afya ya udongo ni muhimu sana kwa ajili ya kuzalisha chakula chenye lishe bora kama vile lishe ilivyo kwa Watoto katika siku zao 1000 za kwanza.

“Kama vile lishe bora ni uwekezaji bora katika ustahimilivu wa kimwili wa watoto, ukuaji wao wa utambuzi, ustawi na uwezo wa kuchuma siku zijazo, udongo wenye afya unapswa kuwa msingi wa mfumo wa chakula wa kila nchi. Mfumo wa chakula ambao utazalisha chakula chenye lishe kwa njia inayostahimili hali ya hewa, kuhakikisha ustawi kwa watu wote wanaohusika.”amesema Verburg

Ukataji miti umesababisha mmomonyoko wa ardhi ya mashamba kaskazini mwa Haiti.
WFP Haiti/Theresa Piorr
Ukataji miti umesababisha mmomonyoko wa ardhi ya mashamba kaskazini mwa Haiti.

Katika kuhakikisha udongo unaotumika katika kilimo una rutuba, washiriki watajadili changamoto na ukosefu wa taarifa za msingi ili kusaidia wakulima, wazalishaji mbolea, watunga sera na watendaji wengine wote ambapo mwisho wa kongamano hilo kwa pamoja wataibuka na suluhu zitakazotoa mifumo bora zaidi ya chakula kitokanacho na kilimo kwa afya bora ya binadamu na ustawi wakati huo huo wakilinda mazingira.  

Mkurugenzi Mkuu wa chama cha kimataifa cha wazalishaji mbolea IFA Alzbeta Klein amesema udongo ndio msingi wa Maisha yote duniani.

“Tunapaswa kutambua jukumu kuu la udongo wenye afya kama rasilimali mabyao ni muhimu kwa lishe, maendeleo ya kiuchumi, mabadiliko ya hali ya hewa na maisha ya kustahimili Maisha na kutathamini ipasavyo.” Ameseme Klein

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya FAO wanadamu kama vile mimea na Wanyama wanahitajichakula ili kuhishi. Lakini chakula hicho kinatakiwa kuwa salama na chenye lishe bora sio tu ili kuwapa nguvu bali virutubisho na pia kuwakinga na kutopata magonjwa kwa kula chakula chenye sumu.

Takribani asilimia 95 ya chakula kinatoka kwenye udongo ambao unauwezo wakusaidia ukuaji wa mimea kwa kuiba rutuba kupitia suluhu za udongo.