Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la NERVO latunga wimbo kuelimisha hatari zikumbazo watoto

Watoto wakifanya kazi katika migodi Ouagadougou, Burkina Faso.
© UNICEF/Frank Dejongh
Watoto wakifanya kazi katika migodi Ouagadougou, Burkina Faso.

Kundi la NERVO latunga wimbo kuelimisha hatari zikumbazo watoto

Haki za binadamu

Wachezeshaji maarufu wa muziki duniani kutoka Australia na ambao ni ndugu wameandika wimbo mpya wenye lengo la kuhamasisha kuhusu hatarini wanazokumbana nazo watoto kama vile utumikishaji watoto na usafirishaji haramu wa watoto.

Taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO iliyotolewa leo jiijni New York, Marekani na Geneva, Uswisi inasema wachezeshaji hao wa muziki wasichana Liv na Mim Nervo wamezindua wimbo huo katika onesho lako kwenye jukwaa kubwa la tamasha la muziki huko Tomorroland nchini Ubelgiji.

Wimbo ulitungwa na wasichana hao wawili ambao kundi lao linaitwa NERVO kwa kushirikiana na shirika la kujitolea kwa ajili ya watoto, Hopeland na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO, na uzinduzi unalenga kwenda sambamba na siku ya kimataifa ya kupinga usafirishaji haramu wa  binadamu tarehe 30 mwezi huu wa Julai.

Kichocheo cha kutunga wimbo

“Baada ya kufahamu zaidi kuhusu masuala haya kupitia kazi yetu na Hopeland, tuliamua kuwa tutatunga wimbo, fanya kile unachoweza kufanya kwa ubora, kufungua macho ya watu kwa tatizo hilo la dunia,” amesema Mim.

Ushiriki wa NERVO kwa zaidi ya wiki tatu kwenye tamasha la Tomorrowland utaibua uelewa wa masuala ya msingi, ili watu waweze kuchukua hatua ya kutokomeza utumikishaij watoto na usafirishaji haramu wa watoto duniani kote.

Kwa upande wake Liv amesema, jambo la kwanza wanaloweza kufanya ni kujenga uelewa na kusaidia mashirika sahihi ili waweze kusaidia kuchochea hatua na kusaidia familia, watoto waweze kwenda shule na kumaliza mzunguko wa umaskini na watoto kuwa hatarini.

Watoto wakitumikishwa katika machimbo ya dhahabu kwenye kijiji cha Luhihi kilichoko jimboni Kivu Kusini nchini DRC.
© UNICEF/Patrick Brown
Watoto wakitumikishwa katika machimbo ya dhahabu kwenye kijiji cha Luhihi kilichoko jimboni Kivu Kusini nchini DRC.

Duniani kote hii leo, zaidi ya watoto milioni 160 wanatumikishwa kwenye ajira. Kati yao hao milioni 79 ni kwenye aina hatari zaidi za ajira na milioni 10 katika utumwa wa zama za sasa.

Kwa nini ILO inaunga mkono NERVO

Lieve Verboven ambaye ni Mkurugenzi wa ILO ofisi ya Brussels nchini Ubelgiji amesema, “masuala ya uelewa juu ya hatua za kuchukua yanahitajika sana na ndio maana tunakaribisha nia ya NERVO na ahadi yao. Tunafahamu kile kinachofanya kazi ;hifadhi ya jamii ya kusaidia familia na kutokomeza umaskini, ajira zenye staha na kupatia ujira wazazi sambamba na kupatia watoto elimu.”

ILO inasema serikali zimeazimia kutokomeza umaskini na kumaliza utumikishaji watoto ifikapo mwaka 2025 kama sehemu ya ajenda ya maendeleo endelevu yam waka 2030.

Ahadi hizo zilirejelewa kwenye Mkutano wa Kimataifa wa mwaka 2022 wa kutokomeza ajira kwa watoto kama sehemu ya Azimio la Durban.