Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko yaliyotokea CAR yanaweza kuwa uhalifu wa Kivita: UN

Msaada wa kibinadamu umewafikia katika mji wa Bria, mji mkuu wa mkoa wa Haute-Kotto katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
OCHA CAR
Msaada wa kibinadamu umewafikia katika mji wa Bria, mji mkuu wa mkoa wa Haute-Kotto katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Machafuko yaliyotokea CAR yanaweza kuwa uhalifu wa Kivita: UN

Haki za binadamu

Machafuko yanayoendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya kati -CAR yanaweza kuwa uhalifu wa kivita imeeleza taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za binadamu baada ya kuwasilisha ripoti zake mbili za matukio ya kutatanisha yaliyotokea kati ya mwaka 2020 mpaka mwaka huu wa 2022 nchini humo.

Taarifa hiyo kutoka Geneva Uswisi imetolewa kufuatia uchunguzi uliofanywa na kitengo cha Haki za binadamu cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuimarisha utulivu nchini CAR- MINUSCA.

Mlinda amani wa MINUSCA akiwa katika doria nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR-Kutoka Maktaba
MINUSCA/Herve Cyriauqe Serefi
Mlinda amani wa MINUSCA akiwa katika doria nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR-Kutoka Maktaba

Ripoti ya Mauaji ya raia

Ripoti ya kwanza ni kuhusu tukio lililotokea kati ya tarehe 6 mpaka 13 mwezi Desemba mwaka jana 2021 ambapo wanamgambo, kati yao kukiwa na wapigananaji ambao zamani walikuwa sehemu ya kikundi cha wanamgambo kilichofahamika kama “Wapinga Balaka” walishambulia kijiji cha Boyo kilichoko katika mkoa wa Ouaka nchini humo na kuwaua takribani watu 20, kubaka wanawake na wasichana watano, kuchoma na kupora nyumba 547 nakusababisha zaidi ya wanakijiji 1000 kuyakimbia makazi yao.

Ripoti hiyo ilieleza wanamgambo hao walioshambulia raia kwa mapanga pia walishikilia mamia ya raia kwa siku tatu katika msikiti wa kijiji wakiwatishia kuwaua lengo likiwa ni kuadhibu jamii ya kiislamy ya Boyo ambayo imekuwa ikiunga mkono kikundi kijulikanacho kama “Kitengo cha amani cha Afrika ya Kati” UPC ambacho kinajihusisha kupingana na serikali.

Kwa mujibu wa utafiti wa MINUSCA wakuu wa kanda wa zamani wa kikundi cha “Wapinga Balaka” wanashutumiwa kuhusika na matukio hayo.

“Ninalaani vikali vitendo hivi vya kutisha. Serikali lazima ikomeshe ukiukwaji wote, iwe (unaofanywa) na vikosi vyake, wanamgambo wanaounga mkono serikali au wakandarasi wa kijeshi wa kigeni binafsi na kuwawajibisha wale wote wanaohusika moja kwa moja na kwa njia isiyo ya moja kwa moja” amesema wa Kamishna Mkuu wa Haki zabinadamu wa Umoja wa MataiFA Michelle Bacehelt

Ripoti hiyo inahitisha kuwa vitendo vilivyotelekezwa huko Boyo vinaweza kujumuisha uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Ripoti hii pia imethibitisha mienendo ambayo imekuwa ikirekodiwa na MINUSCA ya wakandarasi wa kijeshi wa kigeni binafsi kufanya kazi chini ya maelekezo au kwa idhini ya serikali ambapo wanakuwa wakitumia washirika wao kuendeleza mashambulizi dhidi ya raia.

Mkurugenzi wa kitengo wa haki za binadamu wa MINUSCA Hana Talbi amesema “kwa vile washirika hawa ni wapiganaji wa zamani kutoka kwenye makundi mbalimbali yenye silaha au wapinga Balaka, matokeo yanayoweza kutokea kwa kuishi pamoja kwa amani yanaweza kitia wasiwasi sana.”

Katika Mkoa wa Haute Kotto, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Wakimbizi wa ndani walioko PK3 wanajaribu kuipa uhai kambi yao. Wengine wanauza mbao au unga wa muhogo na watoto tayari wamepanga uwanja wao wa michezo
OCHA/Yaye N. Sene
Katika Mkoa wa Haute Kotto, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Wakimbizi wa ndani walioko PK3 wanajaribu kuipa uhai kambi yao. Wengine wanauza mbao au unga wa muhogo na watoto tayari wamepanga uwanja wao wa michezo

Ripoti ya Unyanyasaji wa kijinsia

Ripoti ya pili ni kuhusu udhalilishaji wa kijinsia iliyofanywa na misheni nne za uchunguzi kwakushirkiana na idara ya haki za binadamu MINUSCA katika mikoa ya Mbomou na Haute-kotto ambayo imeangazia unyanyasaji wa kijinsia unaohisiana na migogoro uliofanyika kati ya mwezi Desemba 2020 hapo mwanzoni mwa mwezi Machi 2022 ambapo makundi ya FPRC na UPC yote yakihisishwa kushirikiana na kundi la CPC.

Ripoti zimekusanya Matukio ya udhalilishaji huo kwa wanawake na wasichana 245 wenye umri kati ya miaka nane mpaka 55 huku mengi ya Matukio hayo yameripotiwa kutokea katika miji ya Bakouma huko Mbomou ambako kulikuwa chini ya kukundi cha wanamgambo mpaka mwezi Mei 2021.

“Kiwango hiki cha unyanyasaji wa kingono ambacho hakijawahi kushuhudiwa nchini CAR kinashangaza na kuvunja moyo” amesema Kamishna Mkuu Bachelet

Kundi la CPClilifanikiwa kudhibiti mikoa kadhaa ikiwemo wilaya za Mbomou na Haute-kotto eneo ambalo lina utajiri wa maliasili kama vile madini ya Urani, dhahabu na almasi ambako huko wameripotiwa kufanya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria za kimataifa za kibidamu hususan unyanyasaji wa kijinsia pamoja na vurugu.

Ukatishaji wa huduma za kibinadamu unaathiri upatikanji wa maji Basse-Kotto Prefecture, CAR.
© UNOCHA/Virginie Bero
Ukatishaji wa huduma za kibinadamu unaathiri upatikanji wa maji Basse-Kotto Prefecture, CAR.

Vitendo viovu bado vinaendelea lazima kuwe na uwajibikaji

“Kesi za unyanyasaji wa kijinsia zilizoandikwa na MINUSCA katika wilaya hizo zinazothibitisha kwamba FPRC na USP zinahusisha udhalilishaji wa kijinsia katika migogoro kimuundo na kwa ueneaji mpana” imesema ripoti hiyo.

MINUSCA bado inaendelea kukusanya ushahidi wa kesi katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa makundi hayo yenye silaha lengo likiwa ni kuonyesha mtindo huu wa vurugu una uhusiano unaoendelea na vurugu zinazoendelea mpaka sasa.

“Simulizi za kikatili tulizosikia kutoka kwa waathiriwa wa utumwa wa kingono na unyanyasaji wa kingono zinaonyesha uhalifu ambao haukupaswa kutokea kamwe. Inashangaza ingawa, sio tu zilifanyika lakini bado zinaendelea kutendeka. Ukatili huu haukubaliki kabisa na lazima ukomeshwe mara moja” alisema Bachelet

Mkuu huyo wa Haki za binadamu ameitaka Serikali ya CAR kuchukua hatua za haraka, kwa kufuata kikamilifu sheria za kimataifa, ili kurejesha udhibiti wa eneo lote na kuanzisha tena mamlaka ya majimbo chini ya utawala wa sheria.

Mkuu huyo wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa alikiri na kukaribisha hatua zilizochukuliwa na mamlaka za mahakama na taasisi nyingine za Serikali kuchunguza tuhuma hizi, huku akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha wahusika wote wanawajibishwa ili kuvunja mzunguko wa kutoadhibiwa.