WHO yatangaza maboresho ya mkakati wa utoaji chanjo ya COVID19

Mfanyakazi katika uzalishaji wa chanjo ya COVID-19 nchini India
© UNICEF/ Dhiraj Singh
Mfanyakazi katika uzalishaji wa chanjo ya COVID-19 nchini India

WHO yatangaza maboresho ya mkakati wa utoaji chanjo ya COVID19

Afya

Kutokana na kuendea kunyumbulika kwa virusi vya ugonjwa COVID-19 hii leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limechapisha maboresho ya mkakati wa utoaji chanjo ya COVID-19 ili kukabiliana na kuenea kwa virusi vipya ya Omicron, kuendeleza ushahidi unaopatikana kutokana na kutolewa chanjo na kuendelea kujifunza kutokana na matokeo ya programu za utoaji chanjo duniani kote. 

Taarifa ya WHO kutoka jijini Geneva Uswisi imesema lengo la kuu la mkakati huo ni kutumia dozi mbili zinazotolewa za COVID-19 ili kupunguza vifo pamoja na wagonjwa mahututi ili kulinda mifumo ya afya , jamii na uchumi. Hii ni njia mojawapo ya kufikia lengo la utoaji wa chanjo kwa asilimia 70, nchi zikielekea katika utoaji chanjo kwa asilimia 100 kwa wafanyakazi wa sekta ya afya na makundi mengine ambayo yanaweza kuathirika zaidi wakiugua COVID-19 kama wazee na wale wasio na kinga madhubuti. 

Mkurugenzi Mtendaji wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema utoaji chanjo kwa wote walio hatarini zaidi ni njia bora zaidi ya kuokoa Maisha, mifumo ya afya na kuweka jamii na uchumi wazi. 

“Hata pale ambapo chanjo imetolewa kwa asilimia 70, ikiwa idadi kubwa ya wafanyakazi wa sekta ya afya, wazee na watu walio katika makundi hatarishi wakiwa hawajapata chanjo, vifo vitaendelea , mifumo ya sekta ya afya itasalia katika shinikizo kubwa na dunia itashindwa kupona kutoka kwenye hatari hii.” Ameeleza Dkt Tedros

Katika kuhakikisha utoaji chanjo unafikia makundi yanayolengwa zaidi mkakati huo umehimiza haja ya kupima mafanikio ya utoaji chanjo katika makundi hayo pamoja na kutengeneza mbinu zinazolenga kuwafikia. 

Mbinu hizo ni pamoja na kutumia takwimu za kwenye jamii na kuzishirikisha jamii husika katika kuendeleza utoaji wa chanjo na kuwafikia kila kundi ndani ya jamii. 

Mkakati huo pia una lenga kurahakisha maendeleo na kuhakikisha kuna upatikanaji sawa wa chanjo ili kupunguza kiasi kikubwa cha uambukizanaji wa virusi kama kipaumbele cha kwanza lakini pia kinga ya kudumu na kinga kwa jamii kwa ujumla. 

Wafanyakazi wa afya nchini Indonesia wanasaidia jamii kupunguza hatari ya maambukizi ya COVID-19.
© UNICEF/Arimacs Wilander
Wafanyakazi wa afya nchini Indonesia wanasaidia jamii kupunguza hatari ya maambukizi ya COVID-19.

Utoaji chanjo ya COVID-19 ndio umekubwa mkubwa na wa haraka duniani kote katika historia lakini bado watu wengi walio hatarini wanasalia bila kuwa na ulinzi huo kwakuwa ni asilimia 28 pekee ya wazee ndio wamepata chanjo huku wafanyakazi wa sekta ya afya waliopata chanjo wakiwa ni asilimia 37 katika nchi zenye kipato cha chini. Na kati yao wengi bado hawajapokea dozi ya pili ya kinga dhidi ya COVID-19. 

Katika awamu ya kwanza ya utoaji chanjo ya COVID-19 inakadiriwa Maisha ya watu milioni 19.8 yaliokolewa. 
Kupitia mpango wa utoaji chanjo wa pamoja unaosimamiwa na umoja wa Mataifa GAVI zaidi ya chanjo bilioni 12 zilitolewa duniani kote karibu kila nchi duniani na kusababisha nchi kufikia wastani wa asilimia 60 ya idadi ya watu.

Kusoma maboresho hayo bofya hapa