Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio laua Watoto 14 nchini Syria

Wafanyakazi wa mashirika ya misaada ya kibinadamu na magari UN katika kambi ya wakimbizi kaskazini magharibi mwa Syria.
UNOCHA Maafisa wa Umoja wa Mataifa wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA wakivuka kutoka Uturuki kuingia Syria kutathimini mahitaji ya jamii za wakimbizi wa ndani.

Shambulio laua Watoto 14 nchini Syria

Amani na Usalama

Takriban watoto 14 wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio lililotokea hii leo huko magharibi mwa Idlib kaskazini mashariki mwa Syria.

Taarifa hiyo imetolewa kwa vyombo vya habari kutoka Amman, Syria na Adele Khodr ambaye ni  mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto katika ukanda wa mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika.

Khodr ameeleza kuwa “tukio hili ni ukumbusho wa kuhuzunisha kwamba vita dhidiya Watoto havijaisha. Watoto wa kaskazini magharibi mwa Syria na kote nchini wanaendelea kulipa gharama kubwa zaidi ya ghasia zinazoendelea.”

Mwakilishi huyo wa UNICEF amekumbusha pande zote zilizo kwenye mzozo nchini humo kuwa Watoto hawapaswi kulengwa kamwe kwenye mapigano “Wanapaswa kulindwa wakati wote, popote walipo. Watoto wa Syria wanastahili kuishi bila ghasia au woga”

UNICEF imesema mwaka 2017 asilimia 70 ya ukiukaji mkubwa ulirekodiwa dhidi ya wato nchini Syria ambao ulitendeka kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.