Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya hakikisheni uchaguzi ni wa huru, haki na kuna uwajibikaji: Wataalamu wa UN

Miji katika mataifa yanayoendelea kwa mfano Nairobi nchini Kenya yanaendelea kukua kwa kasi.
UN-Habitat/Julius Mwelu
Miji katika mataifa yanayoendelea kwa mfano Nairobi nchini Kenya yanaendelea kukua kwa kasi.

Kenya hakikisheni uchaguzi ni wa huru, haki na kuna uwajibikaji: Wataalamu wa UN

Haki za binadamu

Wakati Kenya inajiandaa kufanya uchaguzi mkuu tarehe 9 mwezi ujao wa Agosti, 2022 wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa mamlaka nchini humo, wagombea nafasi za uongozi pamoja na vyama vya siasa kuimarisha mazingira wezeshi ili kuepuka ghasia na hatimaye uchaguzi huo ufanyike kwa amani. 

Kupitia taarifa yao waliyoitoa leo huko Geneva, Uswisi na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za binadamu, wataalamu hao wamesema “fursa ya kiraia, ushiriki wa umma, mazingira bora ya uhuru wa kukusanyika na kujieleza ni muhimu ili kuweko kwa mchakato shirikishi wa uchaguzi na watu kutekeleza haki yao ya msingi ya kisiasa.”

Wataalamu hao ni Clement Nyaletsossi voule, Irene Khan, Reem Alsalem, Melissa Upreti, Dorothy Estrada Tanck, Elizabeth Broderick, Ivana Rodacic, Meskerem Geset Techane na Diego Garcia Sayan.

Wataalamu hao wameeleza kuwa mvutano wa kisiasa na ghasia wakati wa kampeni sambamba na kauli za chuki na chochezi kutoka kwa wagombea na wafuasi wao vinaweza kuwa hatari katika kuchochea au kuanzisha ghasia. 

Kujifunza kutoka kwenye chaguzi zilizopota

Taarifa ya wataalamu imeeleza kuwa mzunguko wa uchaguzi ulipita nchini Kenya ulikumbwa na ghasia pamoja ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na kupoteza Maisha na unyanyasai wa kingono na kijinsia . Wasiwasi kuhusu madai hayo yameibuliwa na wataalamu kadhaa wa Umoja wa Mataifa katika mawasiliano ya pamoja na serikali ya Kenya kufuatia uchaguzi wa mwaka 2017.

“Wahusika wote wa mchakato wa uchaguzi lazima wajitolee katika kuhakikisha kuna mwenendo w amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Wagombea wa vyama vya siasa lazima wajizuie kutumia lugha za uchochezi ambazo zinaweza kusababisha vurugu na ukiykwaji wa haki zabinadamu , haswa dhidi ya wanawake, watu wenye ulemavu, watu binafsi wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja LGBTQ+ au makabila” wameeleza wataalamu hao.

Na pindi malalamiko ya aina hiyo yanapowasilishwa kwa mamlaka za Kenya wataalamu hao wamesema

“Mamlaka lazima zichukue hatua zote muhimu ili kuzuia ukiukwaji wa haki za bibadamu wakati wa uchaguzi wa sasa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuna uwajibikaji” pia wameeleza wale wote waliohusika na ukiukaji wa haki za binadamu katika uchaguzi uliopita nab ado hawajawajibishwa lazima hatua zichukuliwe juu yao na wawajibishwe.

Mfanayakazi katika kampuni ya Africa Collext Textiles.
UNEP/Ahmed Nayim Yussuf
Mfanayakazi katika kampuni ya Africa Collext Textiles.

Wanawake

Wanawake wamekuwa waathirika katika ghasia zilizopita  ikiwemo kwenye haki ya ushiriki kwenye siasa na hata wale waliojitokeaza kugombea  na wapiga kura na sasa wataalamu hao wameitaka serikali ya Kenya kuhakikisha inawalinda wanawake na wanashiriki kwenye uchaguzi bila kubaguliwa katika ngazi zote na wala kuwa na wasiwasi wa kudhalilishwa kijinsia na kingono kwakuwa vitendo hivyo vinaathari ya muda mrefu.

“Haki ya kushiriki katika Maisha ya uongozi wa umma ikiwa ni pamoja na haki ya kupiga kura na kugombwa ucgayzi bila hofu ya ghasia ni msingi wa utawala wa kidemokrasia. Hotuba za chuki za kijinsia, vitisho vyovyote vya maneno au mtandaoni, vitendo au unyanyasaji dhidi ya wagombwa na wapiga kura wanawake lazima zizuiwe na kushughulikiwa mara moja ili kuhakikisha ushiriki wao wa maana katika mchakato mzima wa uchaguzi.”

Makundi mengine lyaliyozungumziwa na wataalamu hao ni mashirika ya kiraia, watetezi wa haki zabinadamu waangalizi wa uchaguzi na waandishi wa habari ambapo wameshauri waachwe wafanye kazi zao halali kwa uhuru bila vitisho au kulipiza kisasi.

“Watu hawa wanajukumu muhimu wakaati wa uchaguzi ili kuchangia mchakato wa uchaguzi huru na shirikishi na uaminifu wa matokeo”  

Katika hatua nyingine wataalamu hao wamekaribisha dhamira iliyoelezwa na mamlaka ya nchi hiyo ya kujiepusha na kukatika kwa mawasiliano wakati wa uchaguzi wakieleza kuwa kudumisha ufikiaji wa mtandao na mawasiliano ya simu ni muhimu katika kulinda nafasi za raia.

Vyombo vya usalama navyo vimekumbushwa kutekeleza sheria kwa ufanisi na usimamizi Madhubuti wa umma ili kuwawezesha kukusanyika kwa uhuru kwneye mikutano ya kisiasa na kushiriki kwneye mazungumzo.