Taliban endeleeni kushughulikia kuhusu haki za binadamu nchini Afghanistan: UNAMA

Mtoto wa Krushnal's akitembea kwenye mlima ambao zamani ulikuwa ni nyumba yao huko Afghanistan
IOM/Léo Torréton
Mtoto wa Krushnal's akitembea kwenye mlima ambao zamani ulikuwa ni nyumba yao huko Afghanistan

Taliban endeleeni kushughulikia kuhusu haki za binadamu nchini Afghanistan: UNAMA

Haki za binadamu

Baada ya mamlaka ya Taliban kuwepo madarakani kwa zaidi ya miezi 10 sasa, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umetoa ripoti yake kuhusu haki za binadamu na masuala mengine nchini humo.

Taarifa ya UNAMA kutoka Kabul nchini Afghanistan imezungumzia kuhusu masuala ya ulinzi wa raia, mauaji ya kiholela, mateso na dhuluma, kukamatwa na kuwekwa vizuizini, haki za wanawake na wasichana, uhuru na hali ilivyo katika maeneo ya vizuizini. 

Ripoti hiyo pia imetoa ushauri kwa mamlaka ya Taliban na jumuiya ya kimataifa. 

Matumizi ya silaha

Licha ya kupungua kwa ujumla kwa Matukio ya machafuko ya kutumia silaha lakini takwimu za kati ya mwezi Agositi 2021 mpaka katikati ya mwezi Juni 2022 zilizorekodiwa na UNAMA zinaonesha waliozurika ni raia 2106 ambapo kati yao 700 waliuawa na 1406 walijeruhiwa. 

Idadi kubwa ya vifo vya raia vimerekodiwa kufanywa na kundi la Islamic State la Iraw na jimbo la Levant-Khorasan dhidi ya jamii ndogo za kikabila na kidini yaliyofanyika katika shule, maeneo ya kuabudu pamoja na makazi ya jamii hizo. 

“Huu ni zaidi ya muda ambao wananchi wa Afghanistan wanatakiwa kuishi kwa amani na kujenga upya Maisha yao ya baada ya miaka 20 ya vita.” Amesema Kaimu Mwakilishi wa Katibu Mkuu nchini Afgnaistan Markus Portez. 

Wanawake wawili nchini Afghanistan wakitembea karibu na msikiti wa kale kwenye jimbo la Herat
UNAMA
Wanawake wawili nchini Afghanistan wakitembea karibu na msikiti wa kale kwenye jimbo la Herat

Wanawake na wasichana 

Ingawa mamlaka ya Afghanistan tangu ishike madaraka imekuwa ikichukua hatua zinazooensha kulenga kulinda na kukuza haki za binadamu kama vile kutoa msamaha kwa maafisa wa zamani wa serikali na wanachama wa vikosi vya usalama. 

Lakini amri iliyotolewa tarehe 3 mwezi Desemba 2021 juu ya haki za wanawake na kanuni za maadili zinazohusiana na wafaungwa zimebeba nafasi kubwa ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. 

Portez amesema “Katika kufuatilia kwetu tumegundua licha ya kuimarika kwa hali ya usalama tangu tarehe 15 Agosti 2021 watu wa Afghanistan hususan wanawake na wasichana haki zao za kibinadamu zimeminywa” 

Mauaji 

Ingawa mamlaka ya Taliban ilitangaza kutoa msamaja kwa maafisa wa zamani wa serikali na usalama ma wanajeshi wa Afghanistan lakini msamaha huo hauonekani kuzingatiwa mara kwa mara kwakuwa UNAMA imerekodi mauaji yasiyopungua watu 160 ya maafisa wa zamani wa serikali na usalama yaliyofanywa na maafisa wa serikali kati ya tarehe 15 Agosti 2021 na tarehe 15 Juni 2022. 

Ripoti hiyo ya UNAMA pia imeonesha wasiwasi wa uongozi wa Taliban kutojali kuhusu ukiukwaji wa hakai za binadamu wakitaja Matukio kama ya watu kuuwawa kiholela wakihusishwa na makundi ya silaha pamoja na adhabu za kikatili, udhalilishaji pamoja na kuuwawa kwa watu wanaotuhumiwa kwa uhalifu wa kimaadili pamoja na matumizi ya nguvu kupita kiasia ya maafisa wanaotekeleza sheria. 

Katika ushauri wao wameta uchunguzi ufanyike , wahusika wachukuliwe hatua za kisheria na hatimae Matukio yanayopaswa kuzuiwa yasitokee katika siku zijazo. 

Wanahabari Nchini Afghanistan katika siku ya Uhuru wa vyombo na wanahabari mwezi Machi mwaka uliopita
UNAMA/Fardin Waezi
Wanahabari Nchini Afghanistan katika siku ya Uhuru wa vyombo na wanahabari mwezi Machi mwaka uliopita

Wanaharakati na waandishi wa habari

Katika kipindi cha miezi 10 tangu wachukue udhibiti wa Afghanistan, mamlaka ya Taliban imeweka bayana msimamo wake kuhusu haki za uhuru wa kukusanyika kwa amani, uhuru wa kujieleza na uhuru wa maoni. 

Wana upinzani mdogo kwa kukandamiza maandamano na kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na kuwakamata kiholela waandishi wa habari, waandamanaji na wanaharakati wa mashirika ya kiraia na kutoa vikwazo kwa vyombo vya habari.

“Haki za uhuru wa kukusanyika kwa amani, uhuru wa kujieleza na uhuru wa maoni si tu uhuru wa kimsingi, ni muhimu kwa maendeleo endelevu ya taifa. Zinaruhusu mjadala wa maana kushamiri, pia kufaidisha wale wanaotawala kwa kuwaruhusu kuelewa vyema masuala na matatizo yanayowakabili wananacho,” amesema Fiona Frazer, Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa UNAMA.

Kandahar, Afghanistan
Picha: UNAMA
Kandahar, Afghanistan

Watu kuwekwa vizuizini

Jambo la kutia moyo ni kwamba mamlaka ya Taliban imeonekana kutimiza wajibu wake kuhusiana na jinsi wafungwa wanavyotendewa, kiongozi wa Taliban alinukuliwa kutoa mwongozo kuhusu suala hilo mwezi Januari 2022. 

Ingawa nchi hiyo inajitahidi kuwa na maendeleo lakini maendeleo kwa sasa yanazuiwa na matatizo ya kifedhana kusababisha wakati fulani, ukosefu wa chakula, matibabu na vifaa vya usafi kwa wafungwa na kusitishwa kwa programu za elimu ya ufundi stadi na mafunzo kwa wafungwa ambazo hapo awali zilifadhiliwa na jumuiya ya kimataifa.

Nini kifanyike?

Baada ya tathmini hiyi ya miezi 10 ya uongozi wa Taliban mapendekezo yaliyomo katika ripoti yanaakisi maswala mengi yaliyotolewa na UNAMA na mashirika kadhaa katika kipindi cha miezi 10 iliyopita. 

UNAMA imeshukuru na kusifu kiwango cha ushirikiano hadi sasa na imeahidi kuendelea kusalia kujitolea kusaidia mamlaka ya Taliban katika kulinda na kukuza haki za binadamu za wanawake wote wa Afghanistan, wanaume, wasichana na wavulana.

“Kama inavyooneshwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati wa upanuzi wa mamlaka ya UNAMA, Afghanistan kama taifa linasalia kuwa sehemu ya vyombo kadhaa vinavyohusu masuala ya haki za binadamu na uhuru wa kimsingi. Kwa kuzingatia hili, naziomba mamlaka husika kufanya lolote liwezalo kushughulikia maswala yaliyoainishwa katika ripoti yetu na kutimiza majukumu yao ya kimataifa ya kulinda na kukuza haki za binadamu za Waafghanistan wote,” amesema Markus Potzel, Kaimu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Afghanistan wakati akihitimisha taarifa ya ripo hiyo.

Kusoma zaidi kuhusu ripoti hiyo bofya hapa