Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Mtoto mkimbizi nchini Syria

Vita nchini Syria imesababisha vifo vya asilimia 1.5 ya wananchi wa taifa hilo

© UNICEF/Ali Haj Suleiman
Mtoto mkimbizi nchini Syria

Vita nchini Syria imesababisha vifo vya asilimia 1.5 ya wananchi wa taifa hilo

Amani na Usalama

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeeleza raia zaidi ya laki tatu na elfu sitini waliuawa kati ya tarehe 1 mpaka 31 ya mwezi Machi mwaka 2022 nchini Syria kutokana na vita inayoendelea nchini humo ikiwa ni idadi kubwa ya vifo kurekodiwa nchini Syria.

Ripoti hiyo ya baraza la haki za binadamu iliyotolewa leo jijini Geneva Uswisi imeeleza kurekodi taarifa za vifo vya raia 143,350 kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo majina yao kamili na eneo la kifo. 

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Michelle Bachelet amesema idadi ya vifo nchini Syria katika kipindi cha miaka 10 ni takriban asilimia 1.5 ya idadi ya watu wa taifa hilo. 

“Takwimu hizi za waathirka katika ripoti hii sio tu nambari bali zinawakilisha  binadamu mmoja mmoja. Madhara ya mauaji ya kila mmoja wa raia hawa 306,887 yamekuwa na athari kubwa na yamerudisha nyuma familia na jamii walizokuwa nayo,” amesema Bachelet.

Ameongeza kuwa uchunguzi unaofanyika na taarifa zinazorekodiwa na umoja wa Mataifa na wadau wengine zinasaidia kwa familia hizo “Kazi ya mashirika ya kiraia na Umoja wa Mataifa katika kufuatilia na kuweka kumbukumbu za vifo vinavyotokana na migogoro ni muhimu katika kuzisaidia familia na jumuiya hizi kubaini ukweli, kutafuta uwajibikaji na kutafuta masuluhisho madhubuti. Uchambuzi huu pia utatoa hisia wazi zaidi ya ukali na ukubwa wa mzozo nchini humo”

Kamishna huyo wa haki za binadamu katika kuonesha ukubwa wa mzozo nchini Syria ameeleza kuwa takwimu zilizotolewa leo ni watu waliouawa katika matukio ya moja kwa moja ya opesheni za vita. “Hii haijumuishi raia wengi zaidi waliokufa kutokana na kukosa huduma za afya, chakula, maji safi na haki nyingine muhimu za binadamu, ambazo zimesalia kutathminiwa,” amesisitiza Bachelet 


Ripoti hiyo pia imeeleza kukumbana na changamoto wakati wa kukusanya taarifa. 

Kusoma zaidi kuhusu ripoti hiyo bofya hapa.