Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji wa haki za watoto kwenye mizozo umefurutu ada:UNICEF Ripoti

Watoto raia wa Palestina wakiokota vitu katika nyumba yao iliyoharikika huko mjini Gaza
© UNICEF/Eyad El Baba
Watoto raia wa Palestina wakiokota vitu katika nyumba yao iliyoharikika huko mjini Gaza

Ukiukwaji wa haki za watoto kwenye mizozo umefurutu ada:UNICEF Ripoti

Amani na Usalama

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imesema kati ya mwaka 2005 na 2020 visa zaidi ya 266,000 vya ukiukwaji mbaya zaidi wa haki za watoto vimethibitishwa kutekelezwa na pande zote zinazohusika katika mizozo kwenye nchi zaidi ya 30, barani Afrika, Asia, Mashariki ya Kati na Amerika ya Kusini.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo “Miaka 25 ya watoto na vita vya silaha :Kuchukua hatua kuwalinda watoto katika vita” inasema takwimu hizi ni sehemu ndogo tu ya ukiukwaji wa haki za watoto unaoaminika kufanyika kwa sababu changamoto za fursa na usalama, ikiwa ni Pamoja na changamoto zingine kama aibu, maumivu na hofu kuwa watoto na familia zilizonusurika wanateseka ni vikwazo vya kuripoti, kuweka kumbukumbu na kuthibitisha ukiukwaji huo mbaya wa haki dhidi ya watoto katika hali za vita.

Watoto wakiwa wamekaa kwenye ukuta hujo Douma nchini Syria
© UNICEF/Omar Sanadiki
Watoto wakiwa wamekaa kwenye ukuta hujo Douma nchini Syria

Twakimu za ripoti

Ripoti hiyo imebaini kwamba katika kipindi hicho cha kati ya 2005 na 2020 zaidi ya watoto 104,100 wamethibitishwa kuuawa au kulemazwa katika mazingira ya vita, zaidi ya watoto 93,000 wamethibitishwa kuwa wameandikishwa na kutumiwa na pande zinazozozana jeshini, angalau watoto 25,700 wamethibitishwa kuwa wametekwa nyara na pande zinazozozana, pia pande zinazozozana zimebaka, kulazimisha Watoto kuolewa kwa lazima, kuwanyanyasa kingono, na kufanya aina nyinginezo mbaya za ukatili wa kingono dhidi ya angalau watoto 14,200. 

Umoja wa Mataifa umethibitisha kutokea kwa zaidi ya matukio 13,900 ya mashambulizi dhidi ya shule na hospitali na kuthibitisha sio chini ya matukio 14,900 ya kunyimwa haki za kibinadamu kwa watoto yametokea tangu 2005.
Ongezeko la asilimia 185 katika muongo mmoja

Kwa mujibu wa ripoti katika kipindi mcha muongo mmoja pekee kuanzia 2010 hadi 2020, kulikuwa na ongezeko la asilimia 185% ya ukiukwaji wa haki mkubwa uliothibitishwa dhidi ya watoto katika hali ya migogoro.

Ripoti imechunguza jinsi taarifa kuhusu mifumo iliyoandikwa ya ukiukaji mkubwa wa halki za watoto inavyotumiwa kuchukua hatua kukidhi mahitaji ya watoto. 

Pia imetathimini jinsi ushirikiano na wahusika kwenye migogoro  wakiwemo watendaji wa serikali na wasio wa serikali jinsi wanavyowezasha kumaliza na kuzuia ukiukaji mkubwa wa haki za watoto.

UNICEF inasema tathimini ya ripoti hii inaonyesha kwamba licha ya miongo kadhaa ya juhudi kubwa za kuhamasisha wahusika kwenye mizozo na wale wanaowashawish pamoja na kuimarishwa kwa mbinu za ufuatiliaji, kuripoti na kukabiliana na ukiukaji wa haki mbay, watoto wanaendelea kubeba mzigo mkubwa wa vita. 

Kila siku, wasichana na wavulana wanaoishi katika maeneo yenye migogoro huvumilia mambo ya kutisha ambayo hakuna mtu anayepaswa kupitia.

Maeneo yaliyoathirika zaidi

Ripoti imeweka bayana kwamba kati ya mwaka 2016 na 2020 asilimia 82 ya vifo vyote vya watoto vilivyothibitishwa na mejeruhi vimetokea katika hali tano za mizozo ambazo ni Afghanistan, Israel na Palestine, Syria, Yemen, na Somalia.  

Pia ripoti imesema ni muhimu kutambua kwamba watoto wengi hupitia ukiukwaji zaidi ya mmoja, na hivyo kuongeza uwezekano wao kuwa hatarini zaidi. 

Kwa mfano, utekaji nyara mara nyingi huunganishwa au husababisha ukiukaji mwingine, kama vile kuajiri watoto na kuwatumia na kuwanyanyasa wa kijinsia.

Watoto wakicheza katika gari lililo harika huko Douma , Syria
© UNICEF/Omar Sanadiki
Watoto wakicheza katika gari lililo harika huko Douma , Syria

Mapendekezo

Kama sehemu ya mapendekezo ya ripoti hiyo, UNICEF inaendelea kutoa wito kwa pande zinazohusika na mizozo zilizoorodheshwa katika ripoti ya mwaka ya Katibu Mkuu kuhusu watoto na migogoro ya silaha kushirikiana na Umoja wa Mataifa ili kuandaa na kutekeleza mipango ya utekelezaji ambayo itaweka hatua endelevu na madhubuti za kuwalinda watoto kutokana na ukiukwaji na athari zake. 

Mipango hii ya utekelezaji inaweza kuchukua nafasi muhimu katika kuleta mabadiliko chanya kwa watoto limesema shirika hilo.

Pamoja na kutoa wito kwa pande zinazozozana, na mataifa, kutii wajibu wao chini ya haki za binadamu za kimataifa na sheria za kibinadamu, ripoti hiyo inajumuisha mapendekezo ya kutoa huduma za matunzo na hatua kwa watoto, ukusanyaji na ujumlishaji wa takwimu na ufuatiliaji.