Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara ndogo ndogo na za kati ni tegemeo la uchumi duniani:Guterres

Winnie Kakunta, msimamizi wa uendelezaji wa kampuni ndogo za kati katika Idara ya uhusiano wa jamii ya kampuni ya madini ya Barrick. Kampuni hii imeshirikiana na idara ya ajira bora nchini Zambia kujenga makazi kwa ajili ya wakazi na wafanyakazi wake.
ILO/Crozet M.

Ukuaji wa Kiuchumi

Biashara ndogo ndogo na za kati SME, zinawakilisha karibu asilimia 90 ya biashara za kimataifa, zaidi ya asilimia 60 ya ajira na nusu ya pato la taifa duniani kote na ndio tegemeo la kiuchumi la jamii kote ulimwenguni amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. 

Katika ujumbe wake wa siku ya biashara ndogondogo na za kati hii leo Antonio Guterres amesema biashara hizo kama zilivyokuwa nyingine zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na changamoto nyingi ambazo zinavuruga uchumi kuanzia janga la mabadiliko ya tabianchi, COVID-19 hadi athari za kimataifa kutokana na vita huko Ukraine. 

Kauli mbiu ya siku ya mwaka huu, ni "Mnepo na kujijenga upya", ambayo inaangazia jukumu muhimu la biashara ndogo ndogo na za kati kwa kujikwamua kwa nnjia endelevu na ya haki. 

Katibu mkuu ameendelea kusema katika ujumbe wake kwamba “kuimarisha biashara ndogo ndogo kunasaidia kupambana na umaskini, kuunda ajira na kulinda maisha, hasa kwa watu maskini wanaofanya kazi, wanawake na vijana. Ni lazima sote tufanye juhudi zaidi kusaidia biashara hizi katika kujenga uwezo wa kuhimili mishtuko ya nje na kufuata mifumo endelevu ya biashara.” 

Katika Siku hii ya Kimataifa ya biashara ndogo ndogo na za kati, ambayo huadhimishwa kila mwaka Juni 27 Guterres ametoa wito akisema “Hebu  tufufue upya dhamira yetu ya kutumia uwezo wao kamili, kuokoa malengo ya maendeleo endelevu na kujenga dunia yenye ufanisi na haki kwa wote.”