Manusura wa mateso wakipata ushauri katika moja ya vituo vilivyoko Senegal. Kituo hiki kinafadhiliwa na mfuko wa UN wa hiari wa manusura wa mateso.

Watesaji wasiruhusiwe kukwepa sheria kwa uhalifu wao:UN

OHCHR
Manusura wa mateso wakipata ushauri katika moja ya vituo vilivyoko Senegal. Kituo hiki kinafadhiliwa na mfuko wa UN wa hiari wa manusura wa mateso.

Watesaji wasiruhusiwe kukwepa sheria kwa uhalifu wao:UN

Haki za binadamu

Katika siku ya kimataifa ya kusaidia waathirika wa utesaji Umoja wa Mataifa unataka hatua Madhubuti zichukuliwe ili kuhakikisha watesaji wanahukumiwa kutokana na uhalifu huo.

Akinukuliwa katika ujumbe wake wa siku hii ambayo huadhimishwa kila mwaka Juni 26 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “Watesaji wasiruhusiwe kamwe kutowajibika kwa uhalifu wao na mifumo ambayo inawawezesha watesaji ni lazima isambaratishwe au kubadilisha.” Utesaji ni uhalifu dhidi ya ubinadamu Umoja wa Mataifa unasema mateso yanatafuta kuangamiza utu wa muathiriwa na kukataa utu wa asili wa mwanadamu. Licha ya kupingwa kabisa kwa mateso chini ya sheria za kimataifa, mateso yanaendelea katika maeneo yote ya dunia. “Wasiwasi kuhusu kulinda usalama wa taifa na mipaka unazidi kutumiwa kuruhusu mateso na aina nyingine za ukatili, udhalilishaji na unyanyasaji wa kinyama.” umeonya Umoja wa Mataifa Umeongeza kuwa matokeo yake ya utesaji huo huenda mbali zaidi ya tendo la pekee kwa mtu binafsi na unaweza kuambukizwa kupitia vizazi na kusababisha mzunguko wa vurugu usiokwisha. Umoja wa Mataifa unalaani mateso tangu awali kuwa ni miongoni mwa vitendo viovu vinavyofanywa na binadamu kwa binadamu wenzao. [scald=251882:sdl_editor_representation] Utesaji ni uhalifu chini ya sheria za kimataifa Umoja wa Mataifa umesisitiza kwamba utesaji ni uhalifu chini ya sheria za kimataifa. “Kwa mujibu wa vyombo vyote muhimu, ni marufuku kabisa na hauwezi kuhesabiwa kuwa ni haki kwa hali yoyote.” Marufuku hii ni Umoja huo umesema ni sehemu ya sheria ya kimila ya kimataifa, ambayo ina maana kwamba inambana kila mwanachama wa jumuiya ya kimataifa, bila kujali kama taifa limeidhinisha mikataba ya kimataifa ambayo mateso yamepigwa marufuku waziwazi. Matendo ya utaratibu au yaliyoenea ya mateso yanajumuisha uhalifu dhidi ya ubinadamu. Tarehe 12 Desemba 1997, kwa azimio namba 52/149, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza tarehe 26 Juni kuwa Siku ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya Kuwaunga mkono waathirika wa mateso, kwa nia ya kutokomeza kabisa mateso na utekelezaji mzuri wa mkataba dhidi ya mateso na adhabu zingine za ukatili wa mateso, kinyama au wa kudhalilisha. Umoja wa Mataifa unasema tarehe 26 Juni ni fursa ya kutoa wito kwa washikadau wote ikiwa ni pamoja na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, mashirika ya kiraia na watu binafsi kila mahali kuungana na kuunga mkono mamia ya maelfu ya watu duniani kote ambao wamekuwa wahanga wa mateso na wale ambao bado wanateswa hadi leo.