Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Muhudumu wa afya katika hospitali ya Al Thawra mjini Hudaidah akimchunguza mtoto anayetibiwa kutokana na utapiamlo mkali.

Hakuna wito mkubwa zaidi ya ule wa kuhudumia wengine: Guterres

UNICEF/Ahmed Abdulhaleem
Muhudumu wa afya katika hospitali ya Al Thawra mjini Hudaidah akimchunguza mtoto anayetibiwa kutokana na utapiamlo mkali.

Hakuna wito mkubwa zaidi ya ule wa kuhudumia wengine: Guterres

Masuala ya UM

Wakati hii leo dunia ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya Utumishi  wa Umma, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema siku hii isitumike kusherehekea pekee watumishi wa umma duniani kote bali pia kujitoa kwao kufanya kazi kwa ushirikiano ili kujenga Maisha bora ya baadae ya watu wote. 

Katika ujumbe wake aliotoa kwa ajili ya maadhimisho ya siku hii,  Guterres amesema “Hakuna wito wa juu Zaidi ya kuwahudumia wengine.”

Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku hii inasema “kujijenga upya baada ya COVID-19: Kuimarisha ubunifu na ushirikiano ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.”

Guterres amesema kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyoeleza watumishi wa umma wamekuwa wakifanya kazi bega kwa bega na mashirika ya ndani ya nchi na kimataifa katika kufufua upya maendeleo ya nchi na maendeleo ya jamii zao. 

“Kila mwaka katika siku hii ya Umoja wa Mataifa ya utumishi wa umma tunawaheshimu wanawake na wanaume wote ulimwenguni wanaojitolea kwa ufahari mawazo yao, uvumbuzi na nguvu zao ili kutumikia jamii na wanadamu wenzao.”

Ameenda mbali zaidi na kueleza namna watumishi wa umma wanavyotoa ushirikiano kuanzia kwenye sekta binafsi hadi kutafuta suluhu za kiteknolojia ili kuimarisha utoaji huduma kwa umma, kuunganisha nguvu na asasi za kiraia ili ili kuwa na uwiano wa ujumuishi wa sauti za watu wote kwenye jamii katka sera za umma na programu za kusaka majibu kwa jamii, “ushirikiano ni muhimu katika kubuni na kutoa huduma jumuishi.”