Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Kumbukumbu ya mishumaa kwa wale waliopoteza maisha kwa VVU na UKIMWI, Yerevan, Armenia.

Nchi wanachama zaanza kuongeza ufadhili UNAIDS

Photo IOM Armenia 2018
Kumbukumbu ya mishumaa kwa wale waliopoteza maisha kwa VVU na UKIMWI, Yerevan, Armenia.

Nchi wanachama zaanza kuongeza ufadhili UNAIDS

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI, UNAIDS limeshukuru mataifa yaliyoanza kuongeza fedha za ufadhili kwa ajili ya shughuli za uwekezaji ili kumaliza UKIMWI duniani.

Taarifa iliyotolewa na UNAIDS kwa waandishi wa Habari kutoka Geneva Uswisi imemnukuu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Winnie Byanyima akieeleza shida kubwa walizokumbana nazo wakati ufadhili ulipokuwa mdogo na kueleza ufadhili wenye nguvu na unaotabirika ni muhimu kwa kuokoa Maisha na kumaliza janga la UKIMWI.

“Ni gharama zaidi kutokomeza janga la UKIMWI kuliko kumaliza UKIMWI wenyewe, mamia ya maelfu ya vifo na mamilioni ya maambukizi mapya yote yanaweza kumalizika.” Alisema Byanyima

Nchi zilizotangaza kuongeza ufadhili ni Uingereza na Ujerumani. Uingereza imetangaza ufadhili wake kwa mwaka huu kwa UNAIDS dola milioni 9.8 ikiwa ni ongezekoa la zaidi ya dola milioni 3 ikilinganishwa na mwaka 2021.

Ujerumani nayo imetangaza itafadhili UNAIDS na dola milioni 7.3 ikilinganishwa na dola milioni 6.1 walizofadhili mwaka jana ikiwa ni njia moja wapo ya kuipongeza UNAIDS kwa kazi nzuri ya kusaidia wagonjwa wenye Virusi Vya UKIMWI VVU pamoja na huduma nyingine za afya hususan katika maenep yenye migogoro duniani kote ikiwa ni pamoja na Ukraine n anchi jirani.

Akizungumza katika maandalizi ya mkutano wa saba wa nchi wanachama Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa ufadhili Peter Sands amesema “ili kuwezesha mfuko wa ufadhili wa kimataifa kutimiza malengo yake tunahitaji kuongeza fecha na tunahitaji UNAIDS iwe imefadhiliwa kikamilifu. Hatuwezi kufanya hivyo bila kuwa na fecha na hatuwezi kufanya mazingaombwe ili kuwa na matokeo bora bila kuongeza rasilimali.”

Nchi ya Kenya ikiwakilisha kundi la nchi za Afrika katika mkutano huo ilisema nchi zote ulimwenguni zinategemea UNAIDS ili ziweze kufikia mwisho wa UKIMWI. 

UNAIDS ni Mpango pekee wa pamoja wa Umoja wa Mataifa, wa kipekee unaoleta pamoja mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo ni UNICEF, UNESCO, UN Women, UNHCR, WFP, UNDP, UNFPA, UNODC, ILO, Benki ya Dunia na WHO ili kwa pamoja UNAIDS inachanganya aina mbalimbali za utaalamu wa kiufundi, na kazi za sekta mbalimbali ili kuweza kumaliza janga la UKIMWI.