Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamia ya watu wapoteza maisha kwenye tetemeko la ardhi Afghanistan UN yajipanga kusaidia

Mtoto majeruhi wa tetemeko la ardhi nchini Afghanistan akipata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Urgun.
© UNICEF Afghanistan
Mtoto majeruhi wa tetemeko la ardhi nchini Afghanistan akipata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Urgun.

Mamia ya watu wapoteza maisha kwenye tetemeko la ardhi Afghanistan UN yajipanga kusaidia

Msaada wa Kibinadamu

Wadau wa kimataifa wa misaada ya kibinadmu yakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa wanajiandaa kusaidia maelfu ya familia zilizoathirika zaidi na tetemeko kubwa la ardhi lililokubwa majimbo ya Paktika na Khost nchini Afghanistan mapema leo, mamia ya watu wameripotiwa kufariki dunia, wengi kujerihiwa wengine vibaya sana huku miundombinu ikiharibiwa vibaya.

Kwa mujibu wa taarifa ya OCHA iliyotolewa mjini Geneva Uswisi tetemeko hilo lililotokea usiku wa manane kuamkia leo kwa saa za Afghanistan lilikuwa na ukubwa wa vipimo vya Richa 5.9 na lilitikisa pia maeneo mengine ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, halikadhalika huko Islamabad nchini Pakistan pamoja na India.

Juhudi za misaada limesema shirika hilo zinaijumuisha pia ofisi ya Afghanistan ya masuala ya kibinadamu na kudhibiti majanga ANDMA. 

Wilaya nyingi za majimbo hayo mawili zimeathirika sana ikiwemo Bermal, Zerok, Nika na  Gayan jimboni Paktika na Spera jimboni Khost.  

Wilaya ya Gayan Paktika ndio iliyoathirika Zaidi ambako hadi sasa kumeripotiwa watu zaidi ya 200 wamekuwa na idadi ikitarajiwa kuongezeka , wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa wengi vibaya sana. 

OCHA inasema idadi kamili ya waliokufa au kujeruhiwa haijapatikana lakini inatarajiwa kubwa kubwa zaidi. Mbali ya barambara na miundombinu mingine pia nyumba zaidi ya 1800 zimeripotiwa kubomoka katika wilaya ya Gayan ikiwa ni asilimia 70 ya nyumba zote. 

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linasema shughuli za uokozi zinaendelea.

Shehena ya tani 9.8 za vifaa vya matibabu vikielekezwa kwenye meaneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi lililokumba Afghanistan alfajiri ya tarehe 22 Juni 2022. Vifaa ni pamoja na dawa na vifaa vya upasuaji.
WHO Afghanistan
Shehena ya tani 9.8 za vifaa vya matibabu vikielekezwa kwenye meaneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi lililokumba Afghanistan alfajiri ya tarehe 22 Juni 2022. Vifaa ni pamoja na dawa na vifaa vya upasuaji.

Kwa upande wake shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limetuma salamu za rambirambi kwa familia zilizopotelewa na wapendwa wao na kuwatakia ahuweni ya haraka majeruhi.

Pia limesema serikali ya Taliban imeomba msaada kwa UNICEF na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa ambayo yanajiunga na juhudi za taifa hilo na wadau wengine kutathimini hali na kuchukua hatiu za kukidhi mahitaji ya dharura ya jamii zilizoathirika. 

UNICEF imeshatuma timu zinazozunguka za afya na lishe ili kwenda kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi.