Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Mali, MINUSMA, umeunga mkono juhudi za amani na upatanisho nchini humo. ( Maktaba)

Mlinda amani kutoka Guinea auawa nchini Mali

MINUSMA/Harandane Dicko
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Mali, MINUSMA, umeunga mkono juhudi za amani na upatanisho nchini humo. ( Maktaba)

Mlinda amani kutoka Guinea auawa nchini Mali

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio la bomu lililofanywa leo mjini Kidal  nchini Mali dhidi ya msafara wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kuleta Utulivu nchini Mali (MINUSMA). Msafara huo ulikuwa kwenye operesheni ya kusaka na kugundua mabomu.

Taarifa iliyotolewa leo jijini New York Marekani na msemaji wa Umoja wa Mataifa, imesema mlinda amani mmoja kutoka Guinea aliuawa katika shambulio hilo. Katibu Mkuu anatuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu na wanajeshi wenzake pamoja na wananchi na mamlaka ya Guinea. Katibu Mkuu anakumbusha kwamba mashambulizi yanayolenga walinda amani wa Umoja wa Mataifa yanaweza kuwa uhalifu wa kivita chini ya sheria za kimataifa. Anatoa wito kwa mamlaka ya Mali kufanya juhudi zote katika kuwabaini wahusika wa shambulio hilo ili waweze kufikishwa mahakamani haraka. Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kuwa na mshikamano na wananchi pamoja na mamlaka ya Mali katika harakati zao za kutafuta amani na usalama.