Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika mizozo Pramila Patten  akihutubia Baraza la Usalama kuhusu Ukraine

Kinga ndio njia bora ya ulinzi kwa waathirika wa unyanyasaji wa kingono katika maeneo ya migogoro

UN /Eskinder Debebe
Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika mizozo Pramila Patten akihutubia Baraza la Usalama kuhusu Ukraine

Kinga ndio njia bora ya ulinzi kwa waathirika wa unyanyasaji wa kingono katika maeneo ya migogoro

Amani na Usalama

Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya kwa Masuala ya Kigeni na Sera ya Usalama, Josep Borrell, na Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Unyanyasaji wa Kijinsia katika Migogoro, Pramila Patten, wamehimiza nchi zote duniani hasa zile yenye vita  kuhakikisha wanaweka kinga ya kuzia unyanyasaji wa kingono kwakuwa “Kinga ni njia bora ya ulinzi”

Taaraifa hiyo ya pamoja kutoka Brussels Ubelgiji na New York Marekani imetolewa maalum kwa ajili ya siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Unyanyasaji wa Kijinsia katika Migogoro ambapo wamesema Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya tunaungana na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuharakisha juhudi zake za kutokomeza ukatili wa kingono unaohusishwa na migogoro, na kuokoa vizazi vijavyo dhidi ya janga hili. “Ujumbe wetu uko wazi: ni wakati wa kusonga mbele zaidi ya mbinu tendaji na kushughulikia sababu za msingi na vichochezi visivyoonekana vya unyanyasaji wa kijinsia, kama vile ubaguzi wa kijinsia, ukosefu wa usawa na kutengwa, pamoja na kanuni hatari za kijamii zinazohusiana na heshima, aibu na kuwalaumu waathirika.” Wameeleza kusimama kwa umoja na kwa dhamira yao isiyoyumba ya kuunga mkono manusura na kukomesha hali ya kutoadhibiwa kwa wahalifu. “Ni lazima tuhakikishe kwamba hawasahauliki katika mazingira ya mizozo, hii ikijumuisha kuwapatia ahueni ya janga la kimataifa, na katika kipindi hiki chenye rasilimali zilizobanwa.” Wameongeza kuwa ni lazima kuhakikishwe kuwa sheria ya kimataifa si ahadi tupu kwakuwa mashtaka yanaweza kusaidia kubadilisha utamaduni wa karne nyingi wa kutokujali kwa uhalifu huu kuwa utamaduni. “Walionusurika lazima waonekane na jamii zao kama wamiliki wa haki, zinazopaswa kuheshimiwa na kutekelezwa, wakati wa vita na amani.” Wamekumbusha kuwa katika mwaka uliopita kumekuwa na kuongezeka kwa kuchukua madaraka kijeshi ikiwa ni pamoja na janga la mapinduzi na unyakuzi wa kijeshi, kutoka Afghanistan, hadi Guinea, Mali, Myanmar, na kwingineko, ambayo yamerudisha nyuma haki za wanawake. Hata wakati machafuko mapya yanapoongezeka, vita havijakoma kwingineko, zikiwemo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Somalia, Sudan Kusini, Syria au Yemen. Inaelezwa kuwa viwango vya kutisha vya unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro unatumiwa kama mbinu ya vita na ugaidi, chombo cha ukandamizaji wa kisiasa na aina ya vitisho na kulipiza kisasi dhidi ya wahusika na wanaharakati walio mstari wa mbele. Taarifa hiyo ya pamoja imesisitiza ni muhimu kukuza mazingira ya ulinzi ambayo huzuia na kuzuia unyanyasaji wa kijinsia mara ya kwanza na kuwezesha kuripoti salama na kuwepo na majibu ya kutosha.