Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Hassan Sheikh Mohamud, Rais wa Somalia

Hongera Rais wa Somalia tutakupa ushirikiano:UN

UN Photo/Devra Berkowitz
Hassan Sheikh Mohamud, Rais wa Somalia

Hongera Rais wa Somalia tutakupa ushirikiano:UN

Masuala ya UM

Umoja wa Mataifa umempongeza Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud aliyeapishwa hii leo mjini Mogadishu nchini Somalia na kuahidi kutoa ushirikiano kwa serikali yake katika kutimiza vipaumbele vya nchi hiyo.

Aliyewakilisha Umoja wa Mataifa ni Adam Abdelmoula, Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa na Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu nchini Somalia.

Sherehe za kuapishwa kwa Rais huyo wa kumi zimefanyika katika eneo la  hangar katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Aden Adde na kuhudhuriwa na wawakilishi mbalimbali wa kitaifa, kimataifa ikiwemo wakuu wanchi na wadau wengine wa nchi hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ni miongoni mwa marais walioudhuria uapisho huo sambamba na Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh. 

Wengine ni Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Makamu wa Rais wa Sudan Kusini Taban Deng Gai na Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Kamal Madbouly. 
Nchi nyingine zilizowakilishwa katika sherehe hizo za uapisho ni Umoja wa Falme za Kiarabu, Saudi Arabia, Uganda, Burundi na Turkiye.