Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yaitaka Guinea kuondoa mara moja marufuku ya maandamano 

Conakry, mji mkuu wa Guinea
World Bank/Dominic Chavez
Conakry, mji mkuu wa Guinea

UN yaitaka Guinea kuondoa mara moja marufuku ya maandamano 

Haki za binadamu

Ofisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Jleo imeitaka mamlaka ya mpito nchini Guinea kuondoa mara moja marufuku ya maandamano ya umma. 

Kwa mujibu wa ofisi ya kamishna mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, OHCHR, hatua hizi zinakiuka kanuni na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu na kurudisha nyuma njia ya kuimarisha demokrasia na utawala wa haki. 

"Hatua zilizotangazwa za kuzuia mikusanyiko ya watu na maandamano hazizingatii kanuni za umuhimu na uwiano," amesema Seif Magango, msemaji wa Ofisi ya OHCHR barani Afrika, katika taarifa yake. 

Kamati ya kitaifa ya maendeleo ya mkutano wa hadhara (CNRD) ilitangaza siku ya Ijumaa Mei 13 kupiga marufuku "maandamano yote kwenye barabara kuu za umma, ambayo yana uwezekano wa kuathiri utulivu wa kijamii na utekelezaji sahihi wa shughuli zilizo kwenye mpangilio hadi wakati wa vipindi vya kampeni za uchaguzi. 

Kwa hivyo Conakry iliamuru "vyama vya kisiasa na watendaji wa kijamii kuandaa aina zote za maandamano ya kisiasa ndani ya majimbo yao pekee". Uamuzi huo ulichukuliwa siku mbili baada ya kutimia miezi 36 tangu kuwekwa kwa serikali ya mpito. 

Jukumu la haki katika shughuli za kurejesha mali ya serikali 

Kwa huduma za Kamishna Mkuu Michelle Bachelet, mamlaka za Guinea lazima zirudishe mara moja haki ya uhuru wa kukusanyika kwa amani. 

UNICEF na wadau katika mitaa ya Conakry Guinea ili kutoa taarifa ya jinsi ya kukabiliana na Ebola na pia kugawa sabuni na dawa za chlorine
UNICEF /Guinea
UNICEF na wadau katika mitaa ya Conakry Guinea ili kutoa taarifa ya jinsi ya kukabiliana na Ebola na pia kugawa sabuni na dawa za chlorine

Kujiondoa huku kutoka kwa OHCHR kunakuja wakati miungano kadhaa ya kisiasa na watendaji wa mashirika ya kiraia nchini Guinea tayari wameelezea wasiwasi wao kuhusu "hatua hizi za vikwazo". 

"Tunatambua kuwa uamuzi huu umekuja wakati wadau wa kisiasa na asasi za kiraia nchini wameonyesha kutoridhishwa kwao baada ya tangazo la mamlaka ya kijeshi juu ya kipindi cha mpito cha sasa, ambacho kingechukua miezi 36", limeongeza ofisi ya Kamisha mkuu. 

OHCHR inahimiza mamlaka za mpito kuhakikisha ulinzi halisi na wa maana wa nafasi ya kidemokrasia.  

Hii ni pamoja na kuhakikisha "Kuheshimu haki za uhuru wa kujieleza, kujumuika na kukusanyika kwa amani".  

Kwa Umoja wa Mataifa, haki hizi ni muhimu kwa "kudumisha jamii iliyojumuishi, yenye amani na uthabiti". 

Aidha, ofisi ya kamishna mkuu Bachelet imeonyesha wasiwasi wake kuhusu hatua nyingine iliyochukuliwa hivi karibuni na mamlaka ya mpito, hasa inayohusiana na kurejesha mali isiyohamishika ya Serikali.  

Kwa Umoja wa Mataifa, ubomoaji huu wa mali za kibinafsi huko Conakry, Siguiri na Nzérékoré unafanywa wakati "rufaa zikiwa bado hazijashughulikiwa mbele ya mahakama". 

Kwa upana zaidi, Umoja wa Mataifa unanuia kuendelea kuunga mkono mamlaka ya Guinea katika juhudi zake za kuhakikisha "mabadiliko yenye mafanikio yanayoheshimu haki za binadamu na kupiga hatua kuelekea kurejea kwa utaratibu wa kikatiba".