Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Kamishna Mkuu Michelle Bachelet wakati wa ziara yake nchini China, huko Ürümqi, Xinjiang Uyghur China.

China pitieni upya sera zenu dhidi ya ugaidi – Kamishna Haki za Binadamu

OHCHR
Kamishna Mkuu Michelle Bachelet wakati wa ziara yake nchini China, huko Ürümqi, Xinjiang Uyghur China.

China pitieni upya sera zenu dhidi ya ugaidi – Kamishna Haki za Binadamu

Haki za binadamu

Kufuatia ziara ya siku sita nchini China, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesema ana wasiwasi na serikali ya China kuhusu jinsi wanavyotendewa Waislamu wa Uyghur huko Xinjiang na kuzuiliwa kwa wanaharakati na waandishi wa habari huko Hong Kong.  

Kwa msingi huo Bi Bachelet, ameitaka China kupitia upya sera zake za kupambana na ugaidi ili kuhakikisha zinazingatia viwango vya kimataifa vya haki za binadamu. 
Mwishoni mwa ziara yake nchini humo, Bachelet ameeleza kwamba safari yake ya siku sita, iliyomalizika hii leo Jumamosi na kujumuisha ziara ya eneo linalojitawala la Xinjiang, haikuwa uchunguzi: "ziara rasmi za Kamishna Mkuu ni, kwa asili yake, za hadhi ya juu na zisizofaa kwa aina ya kazi ya uchunguzi wa kina," amefafanua.  

Ziara hii, ya kwanza kufanywa na afisa kama huyo katika miaka 17, "ilikuwa fursa ya kufanya mazungumzo ya moja kwa moja  na uongozi wa juu zaidi kuhusu haki za binadamu, kusikilizana, kuibua mambo yanayotia wasiwasi."  
"Nimeibua maswali na wasiwasi kuhusu matumizi ya hatua za kupambana na ugaidi nah atua za kuondoa itikadi kali na matumizi yake mapana, hasa athari zake kwa haki za Uyghur na Waislamu wengine walio wachache." Bachelet amesema. 

Michelle Bachelet (kushoto), Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, akutana na Waziri wa Mambo ya Nje Wang Yi na maafisa wengine wa China mjini Guangzhou.
© OHCHR
Michelle Bachelet (kushoto), Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, akutana na Waziri wa Mambo ya Nje Wang Yi na maafisa wengine wa China mjini Guangzhou.

China imekanusha madai yote ya unyanyasaji huko Xinjiang 

Kamishna Mkuu amekiri kwamba hakuweza "kutathmini ukubwa" wa kile kinachojulikana kama vituo vya elimu na mafunzo ya ufundi (VETC)" lakini alizungumza na serikali ya China ukosefu wa usimamizi huru wa mahakama juu ya uendeshaji wa programu na tuhuma za matumizi ya nguvu, unyanyasaji na vikwazo vikali kwa utendaji wa kidini. 

“Katika ziara yangu, Serikali imenihakikishia kuwa mfumo wa VETC umevunjwa. Nimeibimiza serikali kufanya mapitio ya sera zote za kupambana na ugaidi na itikadi kali ili kuhakikisha kwamba zinazingatia kikamilifu viwango vya kimataifa vya haki za binadamu na, hasa, kwamba hazitumiki kwa njia ya kiholela na ya kibaguzi.” ameongeza Bachelet. 

Bi Bachelet ambaye amwwahi kuwa Rais wa Chile pia amesema kwamba huko Hong Kong "kukamatwa kwa wanasheria, wanaharakati, waandishi wa habari na watu wengine chini ya Sheria ya Usalama wa Taifa kunatia wasiwasi sana." Zaidi ya hayo, anatumai kuwa "China itajiunga na msukumo unaokua wa kimataifa kuelekea kukomesha hukumu ya kifo." 

Michelle Bachelet, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, anahudhuria mkutano wa mtandaoni na Makamu wa Waziri Du Hangwei wa Wizara ya Usalama wa Umma, katika ziara yake huko Guangzhou, China.
© OHCHR
Michelle Bachelet, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, anahudhuria mkutano wa mtandaoni na Makamu wa Waziri Du Hangwei wa Wizara ya Usalama wa Umma, katika ziara yake huko Guangzhou, China.

Nafasi ya China katika ushirikiano wa kimataifa 

Bachelet amesema "kupunguza umaskini na kutokomeza umaskini uliokithiri, miaka 10 kabla ya muda uliopangwa," ni "mafanikio makubwa ya China." 
Pia amekuna na wawakilishi wa jumuiya ya wafanyabiashara wa China, na ametiwa moyo kuona "makampuni na sekta za China zinapitisha viwango vya haki za binadamu kwa shughuli zao na minyororo ya ugavi." 
Mikataba ya ushirikiano 
Katika ziara hiyo, makubaliano yamefikiwa ya kuanzisha mawasiliano ya mara kwa mara kati ya Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa na Serikali ya China, "ikiwa ni pamoja na kupitia mkutano wa kimkakati wa kila mwaka wa ngazi ya juu wa kujadili masuala yenye maslahi kwa taifa, kikanda au dunia".