Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika siku 3 zijazo tuna fursa ya kipekee ya kutoka katika hatari kwenda kwenye mnepo - Amina J. Mohammed 

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja w Mataifa akiwa Bali Indonesia.
© UNDRR
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja w Mataifa akiwa Bali Indonesia.

Katika siku 3 zijazo tuna fursa ya kipekee ya kutoka katika hatari kwenda kwenye mnepo - Amina J. Mohammed 

Masuala ya UM

Jukwaa la kwanza la kimataifa kuhusu kupunguza hatari za majanga limeanza leo mjini Bali, Indonesia ikiwa ni fursa ya kipekee ya kuweka njia kwa "hatima salama na endelevu.” 

Tukio hilo, ambalo linaleta pamoja serikali, mfumo wa Umoja wa Mataifa na wahusika wakuu wengine ili kubadilishana maarifa na mwelekeo katika kupunguza hatari ya majanga, unafanyika baada ya janga la ugonjwa wa Covid-19 kurudisha nyuma maendeleo katika kila eneo la maendeleo ya ulimwengu kuanzia kwa mabadiliko ya tabianchi hadi usawa wa kijinsia. 

Ripoti ya hivi karibuni ya Tathmini ya ulimwengu inaeleza kuwa kulikuwa na majanga 350 hadi 500 ya kiwango cha kati hadi kikubwa mwaka jana, na idadi ikitarajiwa kufikia 560 au sawa na janga 1.5 kwa siku ifikapo mwaka 2030 ikiwa hakutakuwa na kufikiria upya katika namna ambavyo majanga yanadhibitiwa na kufadhiliwa.  

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina J. Mohammed ambaye amehudhuria mkutano huo amesema, "matendo na maamuzi yetu yanaweza kuchochea hatari na kuwa kwetu katika hatari bila kukusudia.”  

Bi Mohammed ameongeza kusema, "katika siku tatu zijazo, tuna fursa ya kipekee ya kuzingatia chaguzi bora zaidi za sera za kuondoka katika hatari hadi mnepo, na kuchukua hatua muhimu ili kuhakikisha uponaji kutoka kwa Covid-19 unaturudisha kwenye mstari kwa mustakabali salama na endelevu. Tunahitaji pia kuangazia upunguzaji wa hatari ya maafa katika mifumo yetu ya kifedha, ili 'kufikiria mnepo' katika uwekezaji wote wa kifedha." 

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Tathmini ya Ulimwengu, ambayo mwezi uliopita, Aprili iliibua hofu kwamba ubinadamu uko kwenye "mwelekeo wa kujiangamiza", imejadiliwa wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Ulimwenguni pamoja na taarifa rasmi kutoka kwa Nchi Wanachama. 

Naye Rais wa Jamhuri ya Indonesia ambao ni weneji wa mkutano amesema, "Indonesia ni taifa ambalo linakabiliwa sana na majanga. Mnamo mwaka 2022, hadi kufikia Mei 23, mwaka huu wa 2022, maafa 1,300 yametokea na katika mwezi mmoja, kwa wastani, matetemeko 500 yalitokea. Kwa hivyo katika Jukwaa la Kimataifa la Kupunguza Hatari za Maafa, leo, serikali ya Indonesia inatoa kwa ulimwengu dhana ya mnepo kama suluhisho la kupunguza aina zote za majanga, yakiwemo magonjwa ya milipuko.” 

Naye Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Kupunguza Hatari za Majanga, Mami Mizutori amesema, "mkusanyiko wetu ni dhibitisho kwamba ubinadamu haujakata tamaa. Lazima tuutumie wakati huu kubadilisha jinsi tunavyoona na kudhibiti hatari." 

Jukwaa hili likiwa limeandaliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza madhara ya majanga, UNDRR na kusimamiwa na Serikali ya Indonesia, Jukwaa la Kimataifa pia litachukua tathmini ya utekelezaji hadi sasa wa Mkataba wa Sendai wa Umoja wa Mataifa, kupendekeza hatua kwa watunga sera, kuangazia mazoea mazuri n​a kuongeza ufahamu. Matokeo yataunganishwa katika muhtasari wa Wenyeviti-wenza na yatachangia katika mapitio ya kati ya serikali kati ya muhula wa Mpango wa Sendai uliopangwa kwa mwaka 2023.