Skip to main content
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres atunukiwa shahada ya heshima kutoka Chuo Kikuu cha Seton Hall kilichopo New Jersey nchini Marekani.

Msifanye kazi kwa waharibifu wa mazingira : Guterres

UN Photo/Evan Schneider
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres atunukiwa shahada ya heshima kutoka Chuo Kikuu cha Seton Hall kilichopo New Jersey nchini Marekani.

Msifanye kazi kwa waharibifu wa mazingira : Guterres

Tabianchi na mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia wanafunzi wanaohitimu katika Chuo Kikuu cha Seton Hall kilichoko Newark, New Jersey, nchini Marekani  amewaambia “kutofanya kazi kwa waharibifu wa tabianchi” na badala yake watumie talanta zao “kusukuma kuelekea mustakabali unaoweza kurejesha uharibifu uliofanyika.”

Katika Mahafali hayo Guterres amesema wanafunzi wanaohitimu leo lazima wawe kizazi kinachofaulu kushughulikia dharura ya sayari ya mabadiliko ya tabianchi ambayo kizazi chake kimeshindwa kuizuia.

“Licha ya kuwepo kwa ushahidi mwingi wa janga la tabianchi linalokuja, bado tunaona milima mingi ya ufadhili wa makaa ya mawe na mafuta ya kisukuku ambayo yanaua sayari yetu. Fedha hizo zinaendelea kutoka kwa baadhi ya majina makubwa ya wenye uwezo wa kiuchumi na usawa wa kibinafsi,” ameongeza Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.

Licha ya hali hiyo Guterres amesisisitiza kuwa “kuwekeza katika nishati ya mafuta ya kisukuku ni mwisho uliokufa wa kiuchumi na kimazingira.” Na hivyo uwajibikaji unakuja kwa wale wanaoharibu mustakabali wa dunia ndio maana ameona nijukumu lake kuwataarifu wanafunzi hao “juu ya ulimwengu iliojaa hatari” 

Akielezea ukubwa wa changamoto za mazingira duniani kote Guterres amewaeleza wanafunzi waliohitimu leo katika chuo hicho kikuu cha Seton Hill ambacho ni moja ya vyuo vikuu vikongwe na vya kifahari vya Kikatoliki nchini Marekani kilicho karibu na jiji la New York kwamba ulimwengu unakabiliwa na “migogoro na mgawanyiko kwa kiwango ambacho hakijaonekana katika miongo kadhaa - kutoka Yemen hadi Syria, kutoka Ethiopia hadi Sahel na kwingineko.”

Aliangazia pia hali ya Ukraine, akisema “inasababisha mateso makubwa ya wanadamu, uharibifu, vifo na pia inazidisha shida ya chakula, nishati na kifedha kote ulimwenguni.”

Katibu Mkuu kwa masikitiko amewaeleza “kila changamoto ni ishara nyingine kwamba ulimwengu wetu umevunjika sana na haya majeraha haya hayatajiponya yenyewe.”  

Amehitimisha hotuba yake kwa kutoa changamoto kuwa ili kujenga mustakabali bora na wenye amani kunahitajika ushirikiano na uaminifu, mambo ambayo yanakosekana sana katika dunia ya sasa.